The dark side of business

The dark side of business

mimi kama mchaga nishaelewa anakoelekea.
Kuna nguvu kubwa sana katika sadaka ya kafara (sadaka ya kuchinja). Yesu alitolewa kama kondoo wa kafara kwa wanadamu....

Hii code ina garama, coz inatakiwa utoe kafara kwa mtu unayempenda sana kutoka moyoni. Ibrahimu alipotii agizo la kumtoa Isaka kafara...ndipo Mungu akasema sasa nimetambua.....

Kinachotafutwa siyo kafara, bali hiyo kafara ina upekee? ina umuhimu kwa mtoaji? Jinsi unavyompenda mtu na moyo wako huwa juu yake, maana yake kinachotafutwa kwenye kafara ni moyo wa mtoaji ulio juu ya ile sadaka yake ya kipekee. ......kwa maana jinsi Mungu alitupenda hata akamtoa mwanaye wa kipekee....

Ubora/wingi wa sadaka/kafara huamuliwa na sababu ipi inayompelekea muhusika kutoa hiyo sadaka. KWA NINI NATOA HII SADAKA?...

Hakuna sadaka bila madhabahu, ili iitwe ni sadaka/kafara lazima ipitie madhabahuni ndipo itumike na wengine. Madhabahu inaweza kuwa eneo/mahali fulani sacred... lakini pia inaweza isiwe ni physical place....
 
Ilipoishia
Baada ya mzee fabi kunipa kitabu, nilirudi kuendelea na haso zangu Kama kawaida,hiko kitabu kimebeba Siri gani...........
Tuendelee Sasa

Nilisoma kile kitabu Kama nakunywa maji,kilielezea zaidi kuhusu ulimwengu wa kiroho kwenye masuala ya biashara na maendeleo ya sayansi na technolojia,kilieleza nguvu ya technologia dhidi ya uchawi,M-ngu alileta tech ili kuondoa uchawi,hii ni mada ndefu ningeweza hata kuiandikia uzi lakini itoshe kusema Kuna Siri kubwa sana nyuma ya tech,kitu ambacho kilinivutia zaidi kwny kile kitabu ni issue ya mitaji"yaani kutengeneza na kulinda mtaji"kwenye ulimwengu wa roho mtaji una matter zaidi kuliko faida,ndio maana maguru wanasema"the rule number one,don't lose money,'kupoteza hela ya mtaji kwa njia yoyote ile ni ishara ya kutokuwa na ulinzi rohoni,issue ya mitaji ni complex sana ndio maana huku mitaani,kilio cha sina mtaji ni kikubwa,mara mtaji umekata mara mtu amefilisika,hii issue ya mitaji kwa mbongo ni kipengele,kuna watu wana million dollar ideas ila tatizo ni mtaji.
Humo ndani wamegusia concept ya capital dimensions,yaani viwango vya mitaji na ulinzi wa kiroho,alitoa mfano wa bank,ni kwann?wachawi wasiende kuchota hela benki?zimeandikwa sababu kubwa tatu
1)bank zina ulinzi mkali kiroho,(ni dark au light wamiliki ndio wanajua),
2)bank zinatumia technology kupanga hesabu zao(technolojia ina nguvu kiliko uchawi)
3)bank wanahifadhi fedha zao kwenye strong room ya chuma(Kuna mdau aligusia hii issue,huu sio uchawi ni kanuni ya kiroho)

Hizo dimensions ni kama mstari umechorwa kwamba aina flani ya mfanyabiashara asiweze kuvuka kiwango flani cha mtaji,kwenye hicho kitabu waliongelea dimensions 3,ya kwanza ni milioni moja(kwa kifupi tuseme 1M)ya pili 10M na ya tatu ni 100M,yaani mtaji wako ukiwa chini ya milioni moja basi utapata shida sana kuivuka hiyo 1M na Kama ukivuka vita nyingine ni kwny 10M,hapo kuvuka ni kipengele na ukiona mfanyabiashara amevuka mtaji wa milioni 100,huyo rohoni sio mwenzako,kuna dimensions huwezi kuzivuka if you know nothing about spirituality,yaani ni lazima awe nondo sana either darkside au light side nje ya hapo utakuwa unapiga double march time.

Nilimaliza kusoma kile kitabu cha "The dark path"kilichoandikwa na mganda ambaye alikuwa tajiri baadaye alianguka vibaya but later on alirudi juu tena,ameandika mambo aliyopitia na namna alivyo rise to the top again,hicho kitabu kwa sehemu kilinisaidia kujua abc za upande wa pili,na nikajiona sina ulinzi wowote wa maana kiroho,na mfanyabiashara makini ni lazima ujikoki kisawasawa la sivyo wajanja watakuzidi kete.

Turudi nyuma kidogo
kuna mzee mmoja ambaye tulifahamiana siku za nyuma,huyu mzee alikuwa ni fundi wa seat cover za magari,yeye ndiye aliniwekea cover kwny ile hiace yangu,so tulifahamiana kwa njia hiyo.
yule mzee(tumwite mzee sudi) alijenga ukaribu flani na mimi,kwasababu aliniona bwn mdogo harafu namiliki gari ya biashara,so akawa ananifungukia mambo mengi ya gizani(alidhani na mm nitakuwa konki wa hizo kitu) mzee sudi aliwahi kufanya kazi kwenye kampuni za mabasi ya wahindi zaidi ya miaka 20,niliijua dark side ya hao jamaa pitia huyu mzee,akawa ananifungukia mambo mengi sana..
,"Pale kazini ilikuwa kila alhamisi wanachinja mbuzi 20 na damu inamwagwa kuzunguka eneo lote na kila mwaka lazima mfanyakazi afe(hii kwa mtu wa kawaida ni ngumu kujua mpk uwe na spiritual intelligence kama za mzee sudi)
Jamaa walikuwa wanatoa kafara,wafanyakazi,abiria mpaka watu baki ilimradi damu imwagike biashara zao ziende,mtu akifa tu huyo mmiliki wa mabasi anaongeza basi zingine,"nimewafanyia kazi zaidi ya miaka 20 Sina cha maana nilichopata na Kama ningekuwa sijajikoki wangenitoa kafara( aliongea mzee sudi kwa uchungu)
Huyu mzee ndio alinionyesha kitabu wanachokitumia kujitajirisha kupitia jasho,damu na nafsi ya mtu mweusi,wana kunyonya jasho lako,wanakuibia nyota yako then lastly wanakutoa kafara,they are building wealth upon our sweats&bloods.

Zile story za mzee sudi ziliniogopesha Sana kuhusu biashara na hasa hizi za vyombo vya usafiri,yaani bila kupuliza mambo hayaendi😜,huyu mzee alinipa namba za mtaalamu wake aliyemsaidia tangu kipindi yuko kwa mhindi,nilisave namba zake lkn sikuwa na mpango wa kumtafuta,kwasbb mpk muda huo sikuwa naamini Katika ushirikina.

Turudi sasa kwny kile kitabu
Kuna mahali ameandika "kuwa tajiri ni rahisi,kigumu ni kuulinda utajiri wako,matajiri wana siri kubwa sana namna wanalinda utajiri wao,hiki kitabu kilinifanya nijione niko naked kiroho,sasa baada ya kumaliza kusoma,sikutaka kumsumbua mzee fabi,kwasababu msaada alioutoa kwangu ni mkubwa,nikaona nijiongeze kivyangu.
Nikachukua simu nikamtafuta mtaalamu wa mzee sudi,nilichokuwa nakitafuta mimi ni ulinzi sio utajiri,njia za utajiri nilisha zi master ila kwny suala la protection ya kiroho nilikuwa empty.

Nilifika kwa mtalaamu,asubuhi na mapema,hapo kwake nilikuta nyomi ya watu,kila mtu na changamoto yake,nikakaa foleni Kama masaa mawili hv,ilipofika zamu yangu nikaitwa nikazama ndani.............

Kwa mara ya kwanza naanza kulisogelea giza...................
******************************
Nilienda kwa huyu mtaalamu kwa lengo la kutafuta ulinzi na si kitu kingine,lkn nilichokutana nacho hutaweza kuamini..................nini kitajiri? Stay there!
 
Huu ujinga ungefaa kwenye majukwaa mengine.

Like seriously sasa hapa kuna mjadala wa biashara au ujinga tu.

Yaani jukwaa la biashara badała ya kuongelea business objectives, strategies, monitoring of strategies, budgets, marketing.

Tuzungumzie huu upuuzi kama mambo ya biashara.
 
Huu ujinga ungefaa kwenye majukwaa mengine.

Like seriously sasa hapa kuna mjadala wa biashara au ujinga tu.

Yaani jukwaa la biashara badała ya kuongelea business objectives, strategies, monitoring of strategies, budgets, marketing.

Tuzungumzie huu upuuzi kama mambo ya biashara.
We kima hujalazimishwa kuendelea kufuatilia uzi huu
 
Back
Top Bottom