Hakuna shule hakuna chuo utafundishwa kuhusu dark side of anything,Kuna njia mbili tu za kujua wasichokijua watu wengi,njia nyepesi zaidi ni kujua kupitia shuhuda za watu waliopita kwenye kivuli cha mauti na wakatoka salama na njia ngumu zaidi ndio Kama niliyopitia Mimi,i dip my feet into the ways of darkness.
Angalizo
Hiki ninachoandika ni experience ya miaka mingi nyuma, now mimi ni mtu safi,i believe in G-d na kwa kila nnachofanya i pray for his guidance.
Lengo la uzi
Nataka ujue upande wa pili wa shilingi,the dark side of business,uujue ulimwengu wa kiroho wa Biashara kwasababu huko ndio karata zinachezwa huko ndio kete zinasukumwa,sitaki upite dark side nataka upite light side(G-d side) kwasababu mafanikio bila giza yanawezekana.
This is my story
Nikiwa advance kwenye mkoa mmojawapo wa kanda ya ziwa,hapo shule nilipangwa room moja na machalii wawili kutoka A town na Kama unavyojua spirit ya wachaga wengi ni Biashara so ikawa story nyingi ni kuhusu biashara,chalii mmoja(tumwite fabi)ndio alikuwa moto sana na issue za biashara,kwasbb baba yake alikuwa mfanyabiashara mkubwa sana huko chuga,so jamaa alitamani kuvaa viatu vya baba yake.
Mzee wa fabi alikuwa ana hardware mbili kubwa town na nyumba za kutosha,alikuwa ni realestate guru,simply huyu mzee alikuwa tajiri,Kuna likizo tulienda chuga ili nipate mawili matatu kuhusu biashara.
Mzee fabi:ahaa wewe ndio rafiki yake fabi
Mm:ndio mzee,
Fabi:huyu ndio yule rafiki yangu niliyekuambia anapenda kufanya biashara
Mzee fabi:sawa,karibu sana kijana ila someni hizi Biashara mtazikuta tu,sisi hatukusoma lkn hesabu za Biashara tunazijua...(wote tukacheka)then mzee akaondoka akaenda kwenye mishe zake.
siku iliyofuata fabi alinizungusha kwenye miradi ya mzee,alikuwa na lodge 3,semi mbili na nyumba za wapangaji za kutosha,I was amazed!nikasema hakika business is a sure way onto riches,nilitamani nianze mishe za biashara hata kabla sijamaliza shule,kichwa iliwaka moto,baada ya likizo tulirudi shule nikiwa na vibe la kutosha.
Tukiwa shule
Tukawa tunaulizana tukimaliza shule tufanye issue gani!,fabi akawa anasema akimaliza anataka kuuza vocha za jumla(vocha za mitandao ya simu)mimi nikawa nasema nataka kuuza mafuta(dealer wa hizi cooking oil) so siku moja tukaenda town(shule yetu ilikuwa porini,ndani ndani) lengo la kwenda town ilikuwa ni kufanya utafiti wa hizo mishe tulizoplan kuzifanya,hapa nieleze ujanja flani aliotufundisha mzee wake fabi"
ukitaka upate wazo zuri la Biashara angalia customer Queueing" akimaanisha angalia biashara inayotengeneza foleni ya wateja,isee huyu mzee hajasoma lkn alikuwa na nondo Kama za rich dady😃
Sasa huwezi kuamini tulizura pale town kucheki hizo mishe Kama zinatengeneza foleni ya wateja,kwanza tuliona maduka mengi yanayofanya mishe hizo ni ya wahindi(huko mbele nitakuja kueleza dark side ya hawa jamaa hapa bongo,Wana hadi kitabu maalumu cha namna ya kumpiga pin mtu mweusi awe Kama working machine)hawa jamaa kwa sehemu wametuzidi kete(kete za kiroho)....maduka mengi makubwa yalikuwa yao na kweli ile mishe ya vocha tuliona ina foleni si ya kitoto hadi na mm nikashawishika ku abort mishe ya mafuta!niingie kwny vocha.
*****************************
Wadau itabidi nigusie issue muhimu tu ili gazeti lisiwe refu,Sasa nini kitajiri baada ya kumaliza six na kuingia rasmi mtaani..........nitarudi
***************************
Inaendelea.................
Kuna uzi wangu niliutupia hapa unasema"experience ya miaka 15 ya kijiajiri(nadiriki kusema business is a sure way onto true riches)"kwenye huo uzi sikuelezea hiyo miaka 15 nilikuwa nafanya mishe gani, simply ilikuwa ni mishe ya vocha(wholesale)
Sasa baada ya kumaliza six,nilirudi mtaani na harakati za biashara zikaanza rasmi,kuna biashara ndogo nilianzisha lkn mawazo yangu yalikuwa ni mishe ya vocha za jumla, sema mtaji ulikuwa kipengele,so nikavutavuta siku mpk naingia chuo,ile biashara mdogo ilienda poa kimtindo,kuna dogo nilikuwa namwacha shop,mm naendelea na kitabu,nikapata boom(kwny intake yetu tulichelewa kupata,so tukapewa lumpsum ya mwaka mzima ilikuwa Kama 2.4M),chap nikaigeuza kuwa mtaji wa Biashara ya ndoto zangu,hii biashara ya vocha ni kama Biashara ya mafuta,faida yake ni ndogo sana lkn ukiuza mzigo mkubwa faida unaiona,kipindi hicho hii mishe ilikuwa 🔥 🔥 ila now days ni ya kawaida sana,kuuza mzigo wa milioni 5 kwa siku ilikuwa ni jambo la kawaida,nilichanganya shule na biashara kwasababu sikuwa na gutts tena za kusubiri mpk nimalize.
Chuo kilipoisha,
Kwa kweli sikuwa hata na chembe ya kutafuta ajira ijapokuwa matokeo yalikuwa mazuri,washkaji niliomaliza nao walikimbilia ajira,mimi nikaingia rasmi kwenye biashara ya vocha za jumla, wakati namaliza chuo mtaji ulikuwa kama 3M hv lkn ndani ya miezi sita mtaji ukafika 10M miezi sita mingine ikafika 20M,kwa waliofanya mishe hii backdays wanajua kama ukiuza mzigo wa milioni basi faida ni elfu 20,nilikuwa nauza mpk 8M kwa siku,kukunja laki hadi laki na nusu perday ilikuwa kawaida,dat time nikanunua kiwanja,nikajenga maflemu kama nane,then kwa nyuma niliplan kujenga apartments za kupangisha,nilinunua hiace(daladala)ili nitanue wigo,it was amazingl!coz I was just 23,nikazidi kusema "business is a quickest way onto riches" ila sikujua kuwa business is also a riskiest way onto riches,kwa ufupi ile side A ya biashara niliimaster ipasavyo,nilipiga kazi sana mpk watu wakahisi natumia ndumba,kwasababu ofisini watu walikuwa wanajaa,foleni kama nmb,hakika biashara na maisha kwa ujumla viliniendea poa,mtaani kila mtu alitamani afanye biashara kwakile alichokiona kinatokea kwangu,nilitengeneza jina kwa muda mfupi sana ghafla yakaanza mapicha picha,mara nikute damu kwny kiti ninachokalia pale ofisini,Mara hirizi,pesa zikawa zinapotea kimazingara,hua siamini uchawi lkn hiki kilichokuwa kinatokea ni uchawi bila chenga,nilifukuza wafanyakazi lkn haikusaidia(nilihisi wananipiga)nilipiga moyo konde lkn changamoto zilizidi to the extent nikaanza kuogopa biashara,kwa kweli nilibaki njia panda,ila Kuna wazo likanijia,juu ya nini cha kufanya......................
*****************************
Biashara zina ups and downs,niliona upande mmoja,sasa dunia inanionyesha upande wa pili,nini kitaendelea baada ya kupata wazo.............usikose
Sasa tuendelee
Mawazo ya kuhisi nalogwa yalitawala kichwani mwangu na ni kawaida ya mbongo kuwaza hivyo,nilipata wazo la kumtafuta mzee wake fabi,nimwelezee hii changamoto ya pesa kupotea kimazingara,nasema kimazingara kwasababu nilifukuza wafanyakazi nikabaki mwenyewe lkn kila nikipiga hesabu mtaji unakata tu,hata ungekuwa wewe ungehisi kuna namna Kuna mchezo unachezewa,ikabidi nimtafute mzee fabi,yeye ni mzoefu kwny biashara na mambo kama hayo itakuwa amepitia.
Mm:habari mzee wangu za siku.
Mzee fabi:salama,nani mwenzangu
Mm:ni Mimi,rafiki yake na fabi(nikajieleza mzee akanikumbuka,nikamweleza changamoto ninayopitia)
Mzee fabi:kijana mambo hayo Ni kawaida sana kwenye biashara,kwani fedha zako hapo dukani hua unaziweka kwenye nini?
Mm:naziweka kwenye draw
Mzee fabi:usiweke fedha kwenye draw ya mbao,nenda mjini kanunue safe.
Mm:mzee ninapitia changamoto za fedha kupotea kimazingara,hiyo safe itanisaidia kweli?(niliuliza kwa mshangao)
Mzee fabi(huku akicheka):kijana nimefanya biashara zaidi ya miaka 30,ninajua mengi,fanya nilichokuambia..
Kwa kweli sikutaka kuuliza sana nikaonekana ni much know,nikashindwa kusaidika.
Nilienda town,nikanunua safe ya kilo 50 nikaanza kuweka fedha zangu humo na u can't believe,sikupoteza tena fedha baada ya kufanyahivyo.
Nilijaribu kutafuta uhusiano wa kupoteza fedha na kuziweka kwny safe then hazipotei,sikupata jibu,kumuuliza mzee nilishindwa,niliogopa kumkera kwa maswali,hii kitu mpk leo bado inanifikirisha,nilijaribu ku Google walau nitaambulia chochote,sikupata kitu,nikajua Kuna elimu nyingine zimefichwa ni wachache wanajua,wadau tupo hapa kujifunza sijui kila kitu so kama kuna mdau hapa jf anajua atumegee kuhusu hiyo elimu,inakuaje uchawi ushindwe kupenya kwny safe?hii ni sayansi ya namna gani?
In short hii changamoto iliisha kiihivyo,nikaendelae na business zangu Kama kawaida,lakini baadaye kidogo ikaibuka changamoto nyingine iliyonitikisa kibiashara..................
******************************
Nilichojifunza kwa mzee fabi ni kwamba kupata changamoto kwny biashara ni kawaida ila tatizo ni namna unavyozitatua,hebu tuone changamoto ya safari hii nitatoka vp..........let's keep diving
Ilipoishia..........
Ile changamoto ya kupoteza fedha iliisha kiivyo nikaendelea na business zangu Kama kawaida,lkn baadaye kidogo iliibuka changamoto nyingine Tena,iliyonitikisa kibiashara........
Sasa tuendelee
Baaba ya mzee fabi kunipa ujanja wa kuweka hela kwenye safe,nilijiona mshindi,Kuna siku ambayo sitakuja kuisahau,siku hiyo nafika dukani simkuti mlinzi,mimi hua nawahi sana kufika ili nionane kwanza na mlinzi ndio mambo mengine yaendelee,sasa siku hiyo sijamkuta,piga simu hapatikani,nikaenda dukani nakuta geti imerudishiwa tu,kuingia ndani naona paa imevunjwa,nikajua jamaa wameingia,isee mapigo ya moyo yalienda mbio,akili ikanijia nicheki ile safe, nayo haipo😭jamaa wameibeba kabisa,dah!hapo ndio nikajua sijui,kwenye ile safe kulikuwa na zaidi ya 10M,hiyo ilikuwa my saddest day tangu nianze biashara,nilitetemeka all the day,nilitafuta yule mlinzi bila mafanikio,hiyo kazi nikawaachia polisi,mpaka leo hajaonekana,sitamsahau yule mzee alinifanyia umafia wa kiwango cha kasusura!wadau sijui nisemeje ila kuna wakati unaweza kujiona the luckiest guy in the world and within a minute ukajiona the most cursed person in the world,ile daladala nayo ilipata ajali(nilikuja kuiuza kwa hasara kama screpa)it was sad time,nilitafuta ushauri kwa watu sikupata msaada wa maana na wengi walinishauri niende kwa wataalamu nikasafishe nyota,niondoe mikosi,nikawapuuza,nilipata wazo la kumtafuta mzee wake fabi lkn nilijishtukia ikabidi nimtafute kwanza fabi(fabi baada ya kumaliza six,mzee wake alimpeleka kwenda kusoma nje,lkn kipindi hicho alikuwa ameshamaliza yupo chuga kusimamia buss za mzee wake)
Mm:habari fab,za kitambo hiyo,mishe vp?
Fabi:isee mambo safi chalii yangu,niko chuga,nasimamia biashara za mzee,vp ww,upo kwny ajira au umejiajiri?
Mm:nimejiajiri,ajira zinachelewesha kaka(tukacheka then mazungumzo yakaendelea)
Nilimweleza fabi changamoto ninazopitia,so akaniambia usijali,we njoo chuga tutayajenga.
Chuga town
niliingia chuga,mida ya saa mbili usiku,fabi akaniambia nimemweleza mzee wangu changamoto unazopitia,amehaidi atakusaidia,nilifurahi sana,siku hiyo mzee fabi hakuwepo(kila siku ya ijumaa halali nyumbani,analala ofisini) akaingia asubuhi
Mzee fabi:vp kijana mbona umepungua sana?
Mm:kawaida tu mzee wangu si unajua vijana ni kupambana
Nikaendelaea kusema
😛ole na kazi maana niliambiwa umelala ofisini.
Mzee fabi:yah,wakati mwingine kazi zinakuwa nyingi huna budi kulala ofisini,anyway kuhusu suala lako,tutakwenda baadaye kuzungumzia ofisini.
Huyu mzee kwny duka lake moja la hardware ni jengo la ghorofa moja kwa juu ndio ameweka ofisi yake.
Nikafika ofisini kwake,yeye akaelekea dukani,mm akanipa funguo nitangulie ofisini,nikaingia ndani,nikaona kuna shelfu kubwa imejaa vitabu,kwa ukutani Kuna picha kubwa ya triangle ndani ya kiooa,nikiwa nashangaa shangaa,mzee akaingia akaniambia hivyo vitabu vyote nimevisoma,najua vitu vingi kuliko ww ijapokuwa sikusoma kama ninyi akimaanisha(mm n fabi)akaendelea kusema"elimu ya maisha haifundishwi shuleni,ipo katika kusoma vitabu"narudia tena kusema,huyu mzee alikuwa na nondo sio za nchi hii,ameniachia hazina kubwa sana kwny akili yangu,mzee aliongea mengi lkn alinisisitiza niielewe biashara kiroho la sivyo nitakuwa napiga double march time,sikuwa nimemwelewa hasa alimaanisha nn kuhusu kusoma vitabu na hasa alimaanisha vitabu gani,maana Mimi pia ni msomaji mzuri wa vitabu,nilikuwa na maswali mengi ya kumuuliza sema sikutaka kumchimba sana,mzee akainuka kwenye kiti akaenda kwenye shelfu akachomoa kitabu kimoja,akasema nenda kasome hicho,akanipa nauli na 2M ya kuboost mtaji,kwaana niliyumba vibaya,nikamshukuru sana mzee,then nikarudi zangu,kuendelea na haso.
******************************
Hiko kitabu kimebeba Siri gani....tunaelekea patamu,hii si ya kukosa...............