The earth is flat and is not rotating

Bado mtoa mada ana hoja za kufanyia kazi. ndege inaporuka inakua imeacha uso wa dunia hivyo ni kweli kama inaelekea mashariki basi umbali ungeongezeka na kama ingeelekea magharibi umbali ungepungua.

Mkuu nimewahi jiuliza swali kama lako kuhusu mvua/hali ya hewa!! Kwanini mvua inanyesha 24 hours au pengine zaidi ya hapo katika eneo moja? Jibu nililopata ni kwamba atmosphere pia pia inamove...ingekuwa tofauti na hivyo mvua inayonyesha tz saa 2 asubuhi ikiendelea itanyesha USA pia baada ya masaa 8!!

kuhusu ndege wengi washaeleza dunia inamove na vyote vikivyomo, mpaka pale gravitation force inapoishia!! Achana na mawazo duni ya kwamba dunia ni flat, shahidi ni nyingi mpaka sasa na aerial photography imeprove hili achilia mbali ship visibility na nuinginezo!!
 

ndugu usiite mawazo duni ni bora uonyesha hoja nzito kuelezea kuliko kubeza moja kwa moja...
haya mambo ya ushahidi wa picha mimi siyakubali sana...ni vema tukapewa ushahidi zaidi ya huo.
mimi nimewasikia watu wakisema hata ukiangalia meli inapozidi kwenda mbali unaona kama inazama kwamba huo pia ni ushahidi,lakini unaangalia meli inaelekea zanzibar haijafika zanzibar inaonekana kama inazama, kweli huo ni ushahidi ?
hivi namna jicho la binadam linavyoona halina athari katika maumbo ya vitu vikiwa mbali ? isije kuwa tunahitimisha kwa kudanganywa na macho.
 
Nilicho kiona mimi ni kwamba ,jua ndio linaizunguka dunia ,na dunia imesimama ,ila inajizungusha yenyewe palepale iliposimama, kwenye huo mhimili wake ndio tunapata usiku na mchana ,issue hapa ni jua kuzunguka dunia
 

We ndio unatuchanganya kabisaaa, ngoja waje.
 
Hivi hizi commercial Jet zinazokumbwa na masaibu angani zinakuwa nje ya atmosphere au zenyewe sio sehemu ya inzi kwenye ndege ?
Mfano ni AirAsia
Hata mimi nahisi ile ndege ya Malaysia iliyopotea na Abiria ilikumbwa na masaibu ikatoka NJE YA DUNIA. kama hoja hapa ni kwamba dunia ipo flat
 
Mkuu jaribu kuangalia ramani ya dunia katika bendera ya UN... dunia sio flat as rectangle au mraba ni "duara flat" labda niseme hivyo

Ndugu yangu ngoja nikupe darasa kidogo kuhusu mambo ya ramani. Unatolea mfano ramani ya dunia iliyoko kwenye UN emblem/logo. Ile ramani ni projection kutoka 3D curved surface kwenda 2D plain surface. Sasa kwa nini hiyo ramani ni ya mduara? Ramani imekuwa ya mduara kwa kuwa katika kubadilisha kutoka 3D kwenda 2D imetumika projection inaitwa 'Azimuthal equidistant projection". Hii projection imekuwa applied kwenye ncha ya kaskazini mwa duniua (projection centred on the North Pole".

Kwa hiyo unachokiona kwenye ramani iliyoko kwenye UN logo ni ramani ya dunia ikiwa imechorwa kwenye plain surface (2D) kimahesabu imebadilishwa kutoka umbile la duara kuwa kwenye uwanda ulio sawa katika 2D. Projection hiyo hiyo uki-apply kwenye maeneo ya equator ramani ya dunia itatoka tofauti kabisa na ulivyozoea. Labda fanya home usome Map projections kuna materials mengi tu online au hii hapa Map Projections: A Working Manual
 
Hata mimi nahisi ile ndege ya Malaysia iliyopotea na Abiria ilikumbwa na masaibu ikatoka NJE YA DUNIA. kama hoja hapa ni kwamba dunia ipo flat

dunia ni mviringo lakini watu wote dunia nzima tuko juu yake maana wote tunaliona anga kwa mchana hata usiku.
anyway siwajibiki kuamini kila kisemwacho na wanasayansi.
 

Hata mimi nahisi ile ndege ya Malaysia iliyopotea na Abiria ilikumbwa na masaibu ikatoka NJE YA DUNIA. kama hoja hapa ni kwamba dunia ipo flat

nilikuwa ninajibu hoja ya vitu vyote ndani ya atmisphere vinazunguka pamoja.na.dunia huku mfano ukitolewa wa au msafiri kwrnye.ndege akiwa na.uwezo wa kwenda pasipo kuayhiriwa na speed ya ndege
nimehoji kwamba AirAsia rubani aliomba kubadili route kwa kuwa hali ya hewa ilikuwa imechanganyikiwa.
kama vitu vyote katika atmosphere vinazunguka pamoja.na dunia iweje ajali.za.ndege zinatokea zikisababishwa na hali mbaya ya hewa.
hiyo hali.ya hewa yenyewe haizunguki sawa na dunia ?
ni.hoja.dhidi ya dunia kuzunguka...
binafsi sijapata sababu.nzito kuthibitisha dunia kuzunguka..
 
Naomba Nichangie Kidogo....

Sayansi Ya Fizikia Inasema Ukikaaa Ndan Ya Gari Na Ukarusha Kajiwe Kutoka Kwny Mkono Wako Wakat Gari Inatembea( Rusha Umbal Wa Wastan) Kile Kijiwe Kitarud Kwenye Mkono Wako, Hivyo Hivyo Na Ndege Kwa Sababu Inapoanza Kuruka (Projected) Kifizikia Inafanya Considerations Pia Za Speed Ya Dunia.

Pili Iyo Raman Kwenye Bendera Ni Kwamba Wameichora As If They Are In One Of Earth's Pole (Nahis Iyo Ni Arctic) Na Umeona Kabisa IYo Line Margin Ya Dunia Ni Ellipse. Sio Kwamba Iko Tofaut Kama Ulivodai.
 

kama ushahidi wa picha huutaki, unataka ushahidi gani basi?
 
Hivi hizi commercial Jet zinazokumbwa na masaibu angani zinakuwa nje ya atmosphere au zenyewe sio sehemu ya inzi kwenye ndege ?
Mfano ni AirAsia
Commercial jet hizi ni bahati mbaya Mbaya zaid ni kwamba kuna eneo hapo mashariki ya mbali ni mabaya yana mikondo mibaya ya hali ya hewa kuna moja wanaita bermuda Triangle pale ni ndege na meli kwa mamia zimepotea
 

Hebu Mchukue Huyo Inzi/mende Muweke Kwenye Chungu Au Kitu Chochote Cha Duara Then Kizungushe Tuone Kama Atatembea Au Kupaa Usitoe Mifano Kwenye Magari Toa Mifano Kwenye Vitu Vyenye Mzunguko Kuprove
 

Ufunuo 7:1 ni figure of speech inayomaanisha North, South, East and West....kisha inaeleza kuhusu upepo (wind) as wind comes from east, or west or north and south.

Soma Ayubu 26 uone inavyoeleza namna dunia inavyoning'inia na mzingo wa duara uliochorwa juu yake kuzuia maji yaliyo juu.



10 Amechora mviringo juu ya uso wa maji,+
Mpaka mahali ambapo nuru huishia katika giza.


*********************************************************

Luka 4:8 Yesu akamjibu, "Imeandikwa: Utamwabudu Bwana Mungu wako, na utamtumikia yeye peke yake."

kama dunia ingekuwa duara basi ingekuwa haiwezekani kwa falme zote za ulimwengu kuonekana kwa mara moja.

Hii comment yako ni ya kipuuzi kabisa. Kwako wewe haiwezekani kuiona dunia yote kwa mara moja....hata hivyo hakuna mahali ambapo Biblia inasema alimwonyesha mara moja....hii mara moja ni yako wewe......pia Ikiwa Yesu is deity kuuona ulimwengu wote kwa wakati mmoja is not an issue ni issue kwako wewe mwanadamu 'a mortal' unless unataka kuanzisha hoja ya 'Yesu si Mungu'.
 

gari lipo naamini umewahi kipanda,umewahi kurusha kijiwe kikarudi mkononi mwako ?
 
Commercial jet hizi ni bahati mbaya Mbaya zaid ni kwamba kuna eneo hapo mashariki ya mbali ni mabaya yana mikondo mibaya ya hali ya hewa kuna moja wanaita bermuda Triangle pale ni ndege na meli kwa mamia zimepotea

una maana eneo husika atmosphere haizunguki na dunia ? au nini kinatokea angani wakati tunaambiwa dunia inaxinguka na atmosphere yote ?
 
Commercial jet hizi ni bahati mbaya Mbaya zaid ni kwamba kuna eneo hapo mashariki ya mbali ni mabaya yana mikondo mibaya ya hali ya hewa kuna moja wanaita bermuda Triangle pale ni ndege na meli kwa mamia zimepotea

hiyo Triangle ipo bahari ya Antlantiki na siyo mashariki ya mbali, unaweza orodhesha angalau ndege/meli kumi zilizopotea kwenye hicho kimachoitwa bermuda triangle!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…