The earth is flat and is not rotating

The earth is flat and is not rotating

bado dunia haijakibali kutoa siri zake... Ni sisi Tu tunaotunga tunga hizi assumptions

Hakuna siri tena.
Kwa wale waliojifunza biblia watatundua kuwa mambo yaliyokuwa yamefichwa yote sasa yanaweza kupatikana na kuwekwa hadharani.
Mungu anawaonyesha wanadamu mambo makubwa na magumu wasiyoyajua tangu awali.
Yesu aliitwa Emanueli maana yake Mungu pamoja nasi. Kwa hiyo jama Mungu yupo pamoja nasi hakuna siri tena mana yeye ni Engineer Mkuu wa yote.

Kwa wale wakristo wanafahamu kuwa kuna Roho wa maarifa. Hii ni roho inayovumbua mambo yasiyoonekana kwa macho na kuyafanya yaonekane.From nothing to something.
Mfano miaka 3000 iliyopita hapakuwa na simu au tv na haikuwahi hata kuzungumziwa. Lakini wanadamu leo wanaona ni kitu cha kawaida japo ukimwambia mtu hebu tengeneza na wewe simu anashindwa kwani ile ni Roho ya maarifa iliyowekwa kwa baadhi ya wanadamu ili walete mabadiliko na kuwafundisha wengine.
Maarifa ni ya Mungu nwenyewe.

Hata kujua kuwa ndani ya kina kirefu kuna nini na nini pia ni kazi ya maarifa .Kuna utaalam mkubwa wa kutumia mawimbi au wave na kutambua aina za layer zilizopo ardhini.
UKIMTAFUTA PROF.Mhongo atakupa data za kitafiti kuhusu mambo ya layer mbalimbali chini ya ardhi.Na wametumia elimu hiyo hiyo kugungua gesi,mafuta ,madini n.k.

Mpaka sasa hakuna mbadala wa elimu hiyo ya sayansi ya maumbile ya dunia. Na huo mbadala hauna faida yoyote kisayansi na waliotumia elimu tofauti na hii ya leo walishindwa kuwa na maendeleo makubwa ya kisayansi kwa karne nyingi.
 
Ungedokeza hizo "overwhelming " evidence tuone namna zinavyojibu maswali yetu ya kijinga.

Duara likoje kwa mujibu WA huo utafiti ? Au dunia inayohusika kuwa duara mabonde na milima haimo ?
Ama kuhusu ukweli usio shaka ? Ni ukweli gani katika sayansi ambao unakuwa hauna Shaka ?
Hauna Shaka kwa nani ? Ina maanisha baada ya kupata huo ukweli usio na Shaka utafiti kwenye eneo husika umefungwa ?
Ni kweli yaweza kuwa ni Ujinga Tu au sababu zingine kwa upande WA wanaopinga dunia kuwa duara na kuzunguka kwake.
Vivyo hivyo yaweza kuwa pia ni Ujinga au sababu za kimkakati kusema dunia ni duara na inszunguka kutoka upande WA wamasayansi ni ukweli ulio wazi mno kwamba kuna taafiti za kisayansi ambazo matokeo yanatangulia utafiti ili kukidhi haja ya wadhamini WA tafiti husika.
Focus hapa ni dunia tuache kile astrology walichofocus

Nitakujibu kwa ufupi maana kuhusu hili unaweza kuingia library au kutumia search engines tofauti, journals, reliable web sources etc. kufanya utafiti binafsi au unaweza "kuignore" na kuendelea na msimamo wako. Haina shida kabisa. Note nilisema Astronomy sio Astrology.

Ufahamu wa umbo la Dunia unathibitishwa si kwa njia moja bali nyingi zaidi ya mia moja ambazo baadhi ni rahisi la logical hivyo kuzikataa it lead to ignorance as I said before.

Zamani sana kabla sayansi, technolojia na logical reasoning hazijapevuka, maswali mengi yanayohusiana na umbo la Dunia yalikosa majibu kwa kuwa mtazamo wa Flat Earth ama Dunia bapa ulikuwa ndio msingi mkuu. Hata hivyo taratibu evidence za mtazamo tofauti zilianza kuingia kutokana na kupanuka kwa uelewa na kuongezeka kwa vifaa vinavyosaidia "uwezo mdogo wa macho" pekee.

Jielimishe kwa kupitia vizuri mbinu mpya na zamani za kufahamu umbo la Dunia. Mfano Lunar eclipse - Katika geometry solid object yenye umbo la mviringo tu ndio linaweza kusababisha kivuli cha mviringo. Hozion - kaa ufukweni uangalie meli inavyopotelea kazika horizon. Take a geometry class - kuna mambo mengi mfano kupima urefu wa vivuli kutoka katika pande mbili za Dunia, hapo utathibitisha kama ni flat au sphere. Na mbinu na evidence nyingine nyingi sana.

Lakini pia angalia time zones, 24 hrs how do they work? Kwamba sisi kwetu Tanzania mchana na kule Canada ni usiku..jaribu kufafanua kwa flat Earth hiyo inatokeaje? Sasa kubwa zaidi ni picha na observation kutoka angani. Kweli hapo sasa unapopinga unakuwa na sababu maalum. Kuna sattellites maelfu, za nchi mbali mbali zenye uwezo mbali mbali na majukumu tofauti picha na vipimo vyote vinakupa spherical Earth sasa wapi unaipata hii flat one? Umefanikiwa kuipiga picha Dunia kutoka mbali nje, bado unasema ni flat? Kuna kituo cha anga cha kimataifa astrophysicists wanaenda kule kwa shifts wanaiona Dunia usiku na mchana kwa macho yao, bado tunasema Dunia ni flat?

Kuhusu milima na mabonde naweza kukupa mfano mdogo wa kukufikirisha. Mpira wa basketball ni wa mviringo (spherical). Lakini mpira huu ukiuangalia kwa karibu sana katika surface una vipele flani. Kama ukitumia darubini basi surface ya mpira huu ni rough yenye miinuko midogo na mibonyeo. Thus, surface ya Dunia iko hivyo ingawa kuna milima na mabonde ni vitu vidogo sana kwa umbo zima hivyo havibadili umbo hilo. kama ungejua pia kitu ambacho kina smooth surface mfano karatasi ikiangaliwa kwa microscope basi surface yake ina milima na mabonde basi ungejua kwa nini hoja yako haina nguvu kuhusu umbo la Dunia.

Picha hiyo chini ni sehemu ya karatasi iliyopigwa picha na kukuzwa kwa electron microscope. Hiyo ndio ile smooth surface ya karatasi.

12scent.jpg
 
Bado hoja za picha ni za kusadikika zaidi na mfano WA nyumba na dunia ni sawa na mfano WA usiku kwa mchana. Unakuwa upande gani wa dunia unapoipiga picha sides au wewe unasimama angani kusubiri mzunguko WA dunia ukulete sides tofauti ?

Satelite zipo nyingi mno angani .
Kuna maelfu ya satelite huko angani sinapiga picha kutokea pande zote za dunia na kila upande unaonyesha umbo la mviringo.

Mfano niliokupa ni dhahiri kabisa kama umesoma kidigo mambo ya Engineering drawing.

Hata hizi kamera tunazotumia ukimsimulia mtu wa karne 22 zilizopita kuwa binadamu amegundua kitu kinachoweza kunakili sura ya kitu kingine kama kilivyo ataona kuwa ni ndoto na haiwezekani kabisa. Ila hiyo ndiyo sayansi haitangazwi na kufundishwa bila kuthibitishwa na tafiti mbalimbali tena kwa muda mrefu.
 
Angani ni wapi ? Kwenye dunia ya mviringo
 
Na pia niwakumbushe kuwa kama dunia ingekuwa ni flat kama CD basi isingekua na balance na tungetegemea pawe na mikakati ya watu na vitu vilivyoko kwenye nchi mbalimbali kuangalia namna ya kubalance mzunguko wa watu na vitu.
Bila shaka ingefikia wakati ambapo dunia ingepindukia upande mwingine kutokana na upande mwingine kuzidiwa uzito.

Ni umbo la duara pekee lenye balance kubwa isiyozidiwa na upande wowote.
 
Nitakujibu kwa ufupi maana kuhusu hili unaweza kuingia library au kutumia search engines tofauti, journals, reliable web sources etc. kufanya utafiti binafsi au unaweza "kuignore" na kuendelea na msimamo wako. Haina shida kabisa. Note nilisema Astronomy sio Astrology.

Ufahamu wa umbo la Dunia unathibitishwa si kwa njia moja bali nyingi zaidi ya mia moja ambazo baadhi ni rahisi la logical hivyo kuzikataa it lead to ignorance as I said before.

Zamani sana kabla sayansi, technolojia na logical reasoning hazijapevuka, maswali mengi yanayohusiana na umbo la Dunia yalikosa majibu kwa kuwa mtazamo wa Flat Earth ama Dunia bapa ulikuwa ndio msingi mkuu. Hata hivyo taratibu evidence za mtazamo tofauti zilianza kuingia kutokana na kupanuka kwa uelewa na kuongezeka kwa vifaa vinavyosaidia "uwezo mdogo wa macho" pekee.

Jielimishe kwa kupitia vizuri mbinu mpya na zamani za kufahamu umbo la Dunia. Mfano Lunar eclipse - Katika geometry solid object yenye umbo la mviringo tu ndio linaweza kusababisha kivuli cha mviringo. Hozion - kaa ufukweni uangalie meli inavyopotelea kazika horizon. Take a geometry class - kuna mambo mengi mfano kupima urefu wa vivuli kutoka katika pande mbili za Dunia, hapo utathibitisha kama ni flat au sphere. Na mbinu na evidence nyingine nyingi sana.

Lakini pia angalia time zones, 24 hrs how do they work? Kwamba sisi kwetu Tanzania mchana na kule Canada ni usiku..jaribu kufafanua kwa flat Earth hiyo inatokeaje? Sasa kubwa zaidi ni picha na observation kutoka angani. Kweli hapo sasa unapopinga unakuwa na sababu maalum. Kuna sattellites maelfu, za nchi mbali mbali zenye uwezo mbali mbali na majukumu tofauti picha na vipimo vyote vinakupa spherical Earth sasa wapi unaipata hii flat one? Umefanikiwa kuipiga picha Dunia kutoka mbali nje, bado unasema ni flat? Kuna kituo cha anga cha kimataifa astrophysicists wanaenda kule kwa shifts wanaiona Dunia usiku na mchana kwa macho yao, bado tunasema Dunia ni flat?

Kuhusu milima na mabonde naweza kukupa mfano mdogo wa kukufikirisha. Mpira wa basketball ni wa mviringo (spherical). Lakini mpira huu ukiuangalia kwa karibu sana katika surface una vipele flani. Kama ukitumia darubini basi surface ya mpira huu ni rough yenye miinuko midogo na mibonyeo. Thus, surface ya Dunia iko hivyo ingawa kuna milima na mabonde ni vitu vidogo sana kwa umbo zima hivyo havibadili umbo hilo. kama ungejua pia kitu ambacho kina smooth surface mfano karatasi ikiangaliwa kwa microscope basi surface yake ina milima na mabonde basi ungejua kwa nini hoja yako haina nguvu kuhusu umbo la Dunia.

Picha hiyo chini ni sehemu ya karatasi iliyopigwa picha na kukuzwa kwa electron microscope. Hiyo ndio ile smooth surface ya karatasi.

12scent.jpg

OK.wewe umesoma na kuamini, nami nimesoma nimeona picha bado akili yangu haikubaliani. Naona mapungufu mengi mengi mno ambayo picha na maelezo hayajibu. Dunia inazunguka ni maelezo yasio na mashiko pia.hata satellite ziwe nyingi Kama nyota zipige picha tokea pande zozote bado satellite haziwezi kuniambia kuwa dunia inazunguka au ni Kama Mpira WA basket.
Haya ya huku kuwa mchana na huku kuwa usiku bado hakuelezi ukweli WA dunia ama kuwa mviringo ama kuwa dunia inazunguka. What if miale ya jua inakuja Kama ya tochi na jua. Likawa ndilo linazunguka ?
 
Na pia niwakumbushe kuwa kama dunia ingekuwa ni flat kama CD basi isingekua na balance na tungetegemea pawe na mikakati ya watu na vitu vilivyoko kwenye nchi mbalimbali kuangalia namna ya kubalance mzunguko wa watu na vitu.
Bila shaka ingefikia wakati ambapo dunia ingepindukia upande mwingine kutokana na upande mwingine kuzidiwa uzito.

Ni umbo la duara pekee lenye balance kubwa isiyozidiwa na upande wowote.

Hii ya mviringo wewe ndiye umeiweka iwe na balance ?
 
It does make a difference. One
way the speed of the plane is
added to Earth's rotation, one
way it's subtracted from Earth's
rotation. Special relativity says
t' = t*sqrt(1-v^2/c^2). Going with the rotation you have a
higher v and thus time passes
slower.
 
OK.wewe umesoma na kuamini, nami nimesoma nimeona picha bado akili yangu haikubaliani. Naona mapungufu mengi mengi mno ambayo picha na maelezo hayajibu. Dunia inazunguka ni maelezo yasio na mashiko pia.hata satellite ziwe nyingi Kama nyota zipige picha tokea pande zozote bado satellite haziwezi kuniambia kuwa dunia inazunguka au ni Kama Mpira WA basket.
Haya ya huku kuwa mchana na huku kuwa usiku bado hakuelezi ukweli WA dunia ama kuwa mviringo ama kuwa dunia inazunguka. What if miale ya jua inakuja Kama ya tochi na jua. Likawa ndilo linazunguka ?

Mkuu sayansi na majaribio yote hayakubali kuwa mivutano iliyopo baina ya jua na dunia na ukubwa na uzito wa jua haliwezi kuzunguka dunia.

Kama kuna wanasayansi mahiri ambao leo hii wanatufanya tunauweka ulimwengu kiganjani basi ujue Mungu ni zaidi ya wote .
Na ameumba na kuweka vitu vyote kisayansi. Na Mungu alitambua kuwa kama angeweka dunia katika hali ya kusimama bila kuzunguka tena kwa speed kubwa basi maji yote yaliyoko baharini yangemwagikia kusikojulkana.Vinginevyo dunia ingekua kama ndoo au pipa.

Kwa sayansi hii ya kumuiga Mungu wale waliopata maarifa ya kimungu wameweza kurusha satelite zinazozunguka angani kwa speed kubwa bila kutumia engine zaidi ya mvutano uliopo kati ya dunia na hizo satelite.Udogo wa satelite na uzito wake ukilinganisha na dunia ndio unaozifanya zizunguke dunia badala ya dunia kuzizunguka.

Haya yote Mungu aliyafanya kwa sayansi na maarifa ya hali ya juu sana.
 
Kwa nini iwe ndani ya basi linalokimbia Tu na sio nyuma ya Lorry semi-kichanja ? Inzi anaweza kukimbia akiwa kwenye trailor wazi la semi liendalo kasi ?

Kinachoangaliwa ni uwiano kati ya Mass M1 na mass m2. Ndege ingekua ni kubwa kuliko au karibia na ukubwa au uzito wa dunia bila shaka ingekua inaachwa na dunia wakati wa kuruka angani.

Ukiwa nyuma ya lori kinalokimbia huwezi kurusha mpira juu na ukarudi kwako ukaudaka kwani nidhahiri kuwa mpira utadondoka huku lori likiwa limepita. Hii ni kutokana na ukubwa wa lori na mpira havikuachana kama ilivyo ndege na dunia.
Hali hiyohiyo inakuwa tofauti kwenye Meli kubwa kama Manowari za kijeshi ambazo unaweza kupanga magoli na kucheza soka bila kupoteza malengo ya mpira. Tafakari kwa mifano yakwako mwenyewe utapata jibu.
 
Mkuu sayansi na majaribio yote hayakubali kuwa mivutano iliyopo baina ya jua na dunia na ukubwa na uzito wa jua haliwezi kuzunguka dunia.

Kama kuna wanasayansi mahiri ambao leo hii wanatufanya tunauweka ulimwengu kiganjani basi ujue Mungu ni zaidi ya wote .
Na ameumba na kuweka vitu vyote kisayansi. Na Mungu alitambua kuwa kama angeweka dunia katika hali ya kusimama bila kuzunguka tena kwa speed kubwa basi maji yote yaliyoko baharini yangemwagikia kusikojulkana.Vinginevyo dunia ingekua kama ndoo au pipa.

Kwa sayansi hii ya kumuiga Mungu wale waliopata maarifa ya kimungu wameweza kurusha satelite zinazozunguka angani kwa speed kubwa bila kutumia engine zaidi ya mvutano uliopo kati ya dunia na hizo satelite.Udogo wa satelite na uzito wake ukilinganisha na dunia ndio unaozifanya zizunguke dunia badala ya dunia kuzizunguka.

Haya yote Mungu aliyafanya kwa sayansi na maarifa ya hali ya juu sana.

Hakuna ushahidi wa dunia kuzunguka yote uliyoyaongea ni imani tu tena isiyo na mashiko.
Ni kweli Mungu aliumba kwa njia zake na wale watafutao kwa njia zao za kibinadam huku wakimbeza Mungu wataishia kuhitimisha pasipo yakini. Ili waijue kweli ni budi kwanza waikubali kweli ya Mungu. Kinyume chake ni kufukuza upepo.
Dunia kuzunguka ni story mpaka sasa.
Ama kuhusu wamasayansi ni wazi kwa sasa wanaongozwa nini wafikiri na nini wasifikiri kwa kuwa wamewekea wigo WA kucheza na fikra zao.
Nakubali tecnolojia imekuwa kiasi chake lakini hiyo technolojia yenyewe imejengwa kwenye imani ya dunia kuzunguka kwa kasi Sana Kama ulivyoandika the end have justified the means
 
mkuu hebu angalia .... je jibu litafanana endapo mtu akitoka kiti cha nyuma na kwenda kiti cha dereva kwa kutembea .... na mti akitoka kiti cha nyuma kwenda kenywe kiti cha dereva kwa kupaa?
Kama speed ya kupaa ni kubwa kuliko ya kutembea obvious atachukua muda mfupi, ni sawa na kwenda sehemu kwa gari na mwingine akaenda kwa ndege.

Mkuu nina maswali yangu.

Kama dunia ni duara flat kama ilivyo CD au sarafu kwa maana kwamba ina pande mbili je kila upande wa dunia kuna maisha yanaendelea na kama yapo unaweza kusema ni nchi zipi zipo upande gani na kama upande mmoja hakuna maisha kuna vitu gani huko?

Ni rahisi kupima unene wa duara flat je unene wa hii dunia yako ni kiasi gani?
 
OK.wewe umesoma na kuamini, nami nimesoma nimeona picha bado akili yangu haikubaliani. Naona mapungufu mengi mengi mno ambayo picha na maelezo hayajibu. Dunia inazunguka ni maelezo yasio na mashiko pia.hata satellite ziwe nyingi Kama nyota zipige picha tokea pande zozote bado satellite haziwezi kuniambia kuwa dunia inazunguka au ni Kama Mpira WA basket.
Haya ya huku kuwa mchana na huku kuwa usiku bado hakuelezi ukweli WA dunia ama kuwa mviringo ama kuwa dunia inazunguka. What if miale ya jua inakuja Kama ya tochi na jua. Likawa ndilo linazunguka ?

Hii ya mviringo wewe ndiye umeiweka iwe na balance ?

Sidhani kama unaweza kuangusha mpira kwa kuusukuma na ukaonekana umeanguka.
Lakini CD ukiiweka kwa kuilaza unaweza ukaigeuza kwa kuongeza uzito upande mmoja.
 
Hakuna ushahidi wa dunia kuzunguka yote uliyoyaongea ni imani tu tena isiyo na mashiko.
Ni kweli Mungu aliumba kwa njia zake na wale watafutao kwa njia zao za kibinadam huku wakimbeza Mungu wataishia kuhitimisha pasipo yakini. Ili waijue kweli ni budi kwanza waikubali kweli ya Mungu. Kinyume chake ni kufukuza upepo.
Dunia kuzunguka ni story mpaka sasa.
Ama kuhusu wamasayansi ni wazi kwa sasa wanaongozwa nini wafikiri na nini wasifikiri kwa kuwa wamewekea wigo WA kucheza na fikra zao.
Nakubali tecnolojia imekuwa kiasi chake lakini hiyo technolojia yenyewe imejengwa kwenye imani ya dunia kuzunguka kwa kasi Sana Kama ulivyoandika the end have justified the means

Nadhani unapoongelea wanasayansi unasahau kuwa nao ni mfano wa uumbaji wa Mungu.

Na zaidi kwa wale wanaoamini biblia wanajua kuwa Mungu ni Roho na anafanya kazi zake ndani ya Mioyo ya watu. Ndio maana watu wanajazwa Roho ya maarifa na Mungu Mwenyewe kwa makusudi yake na wanafikiri na kutamka mambo ambayo hayakufahamika tangu mwanzo.
Kumjua Mungu sio kutoa pepo tu bali pia kuonyesha kwa vitendo kuwa binadamu ni kiumbe bora chenye uwezo wa kufikiri jambo kwa usahihi wake bila kuliona kwanza.
Fikra ndiyo iliyotengeneza ndege zisizo na rubani,simu inayofanya kazi kwa uhakika wa kumfikia mtu kwa namba yake aliyowekewa bila kukosea.

Wanasayansi wote mahiri walimjua Mungu na walisoma sana vitabu vya dini.
Sisi tunaojifunza na kusoma nmna ya kufanya application tu ya wanasayansi ndio tunaokuwa na debate za kupinga uwepo wa Mungu.
Uvumbuzi wote mkubwa unatokana na imani na maono.
Hapa nazungumza kiimani zaidi ili kuonyesha kuwa mtu wa imani asije akajisahau na kufikiri kwamba yeye ndiye kila kitu.La hasha Mungu pia alifunua roho ya maarifa kwa watu wake waliokesha usiku na mchana na wengine kupoteza maisha yao kwa ajili ya kuweka misingi sahihi ya elimu ya sayansi .

Nitatoka nje ya mada kwa kukupa mfano wa radi. Karne nyingi watu walidhani kwamba radi ni kitu kana uchawi au kiumbe fulani lakini sayansi ikavumbua kuwa radi ni umeme wenye chaji chanya(+ ) na hasi(-). Huu ndio usahihi wa kisayansi ili kumtoa mwanadamu kwenye fikra potofu juu ya uumbaji.
Mwezi,nyota na jua vilidhaniwa kuwa ni viumbe vyenye uwezo wa kuamua kama baba mama na watoto. Na viliabudiwa kwa karne nyingi leo hii sayansi imethibitisha kuwa vile sio viumbe hai na havina mamlaka yoyote na ni viumbe viumbe tu kama mawe n.k.
Huo ndio usahihi wa sayansi.
Sasa ni kwa nini tukatae picha za satelite zinazoonyesha kuwa dunia ina umbo la tufe?
 
unajua picha ya kwanza ya dunia kuwa tufe ilikuwa Ni 1969.... Lakin iliibua maswali mengi Sana... Kuhusu nyota hakuna anaeijua nyota asili yake lakin Ki sayansi unaambiwa Iko umbali wa millions of miles Na zingine kubwa kuliko jua letu.. Lakin no one have been there karibu Na nyota... Mie binafsi navojua science Ina pinga uumbaji maana Kuna maelezo kwamba dunia ilitokana Na sayari inaitwa tiamat ambayo ilipigwa Na another heavenly body ikameguka Na kutengeneza planet ya earth Na mars Na kuacha belt ya mawe kati ya mars Na Jupiter... Hivyo hii inakuwa proved Na basement ya pacifi ocean rock formation
 
Dunia ni round, hilo hata halihitaji ubishi, picha zipo nyingi zinapigwa kila siku kutoka angani.

Kila kitu kilichomo ndani ya atmosphere, binadamu na ndege vyote wakati dunia inazunguka, inazunguka navyo pia kwa hiyo usidhani ndege itaruka afu umbali upungue, ingekua hivo basi hata chini hapa tungekua tukiruka tunatua kwingine.. For as long as kitu kimo ndani ya atmosphere basi dunia inavozunguka na chenyewe kinazunguka vilevile kwa speed ileile...

Afu angalia satellites zilizoko angani, kuna satellite zinaitwa geostationery ambazo zenyewe hua zinaonekana kama zimesimama, zile satellite kwa kua ziko nje kiasi kwamba haziwezi kuzungushwa na dunia, hua zinapewa speed sawa na speed ya dunia, sasa kiukweli ni kama zinaanguka vile sema zinaonekana stationery sababu zinaenda kwa speed sawa na speed ya mzunguko wa dunia..

kama dunia ingekua flat hivi inategemea jua lingeonekana kama linazama kwenda chini?? si lingeonekana linapita tu kutoka kulia kwenda kushoto, sio kuonekana linatoka chini linakuja juu afu linaenda chini tena...

Afu watu NASA mnawaona kama mashetani, wanaofanya kazi pale ni watu ka wewe na mimi, yaweza kua ndugu yako au rafiki, sio watu walioletwa kutoka kuzimu wale kusema wanazuia ndege kupita Antarctica, mbona watu wanaenda kule kila mwaka, we aliyekwambia wanazuia ni akina nani?? hakuna evidence yoyote kule kua dunia haizunguki wala si duara..

Jamani nunueni hata telescope basi za bei nafuu mtumie kuangalia mwezi au sayari nyingine za karibu muone kua ni duara na hivi vitu vipo kweli sio kwamba vinaandikwa tu.. huwezi danganya science ambayo ndo leo hii inakusaidia wewe unatumia jamiiforums

Good an nice answer of all of the time!!!!!!
 
OK.wewe umesoma na kuamini, nami nimesoma nimeona picha bado akili yangu haikubaliani. Naona mapungufu mengi mengi mno ambayo picha na maelezo hayajibu. Dunia inazunguka ni maelezo yasio na mashiko pia.hata satellite ziwe nyingi Kama nyota zipige picha tokea pande zozote bado satellite haziwezi kuniambia kuwa dunia inazunguka au ni Kama Mpira WA basket.
Haya ya huku kuwa mchana na huku kuwa usiku bado hakuelezi ukweli WA dunia ama kuwa mviringo ama kuwa dunia inazunguka. What if miale ya jua inakuja Kama ya tochi na jua. Likawa ndilo linazunguka ?
Nkwesa Makambo, ulivyoniuliza kuhusu "overwhelming evidence" nilidhani una hoja ambayo naweza nikajadili nawe. Kutokubaliana ni haki yako ya msingi kabisa, plan ni kujibu hoja si kukabiliana na akili yako ikubaliane na maoni yangu, huo ni utashi wako.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom