Mlalahoi
JF-Expert Member
- Aug 31, 2006
- 2,182
- 885
Wa vijijini ndio worse off!
Nime generalize? Afadhali wa mjini wanashinda wanakunywa chai chapati kazini na kusoma "Sani," wa vijijini hata kazini hawaji, hawagusi kitu, kazi wao ni kunywa pombe, kukalia vigoda. Wanachojua ni kusimamia tohara za vi teenager vya kike na kushinda kwenye ngoma, hususan wanaume. Unasema walipigania uhuru? Angalia hawa waliopigania uhuru wanavyo walaani wazee wa vijijini walivyolegalega toka enzi za uhuru the '60s:
``Ukweli wenyewe ni kwamba vijijini kina mama hufanya sana kazi. Pengine hutimiza saa 12 au 14 kutwa. Hawana Jumapili, na hawana livu. Kina mama wa vijijini hufanya kazi zaidi kuliko mtu mwingine ye yote katika Tanzania.
Lakini kina baba wa vijijini (na baadhi ya kina mama wa mijini) nusu ya maisha yao ni livu. Nguvu hizi za mamilioni ya kina baba vijijini na maelfu ya kina mama wa mijini ambazo hivi sasa hazifanyi kazi yo yote ila kupiga soga, kucheza ngoma na kunywa pombe, ni hazina kubwa yenye manufaa zaidi kwa maendeeo ya nchi yetu kuliko hazina za mataifa matajiri`` TANU, ARUSHA, Januari 29, 1967
Kwa hiyo, si mjini si vijijini, wavivu, tusisafishane. Tena wa vijijini nusu yao nzima ni wafanyakazi wafu. Shughuli za mjini ni send off, shughuli za vijijini ni ngoma. Mdundiko na Sindimba na Rythm and Blues na Mayenu. Difference without distinction.
Mtanzania akikwambia "naenda kwenye shughuli" usidhani anaenda kupima kiwanja au shamba. Tafrija. "Kikao" ni get-together ya mikakati ya tafrija ya kipaimara cha mtoto. Akisema anaenda kwenye rehearsal usidhani ni practice ya kitu cha maana zaidi ya upambe wa tafrija. Kama sio ndoa ya mke wa pili basi ni Iddi pili. Maulidi haziishi. Kuna Pasaka mpaka Jumatatu. Na Jumatano za Majivu, na Ijumaa za Mateso. Na Ubarikio wa vinjiti.
Hizo ndizo "shughuli," ukisikia Mtanzania anakwambia anaenda kwenye "shughuli." Sote na Kikwete wetu ni slow.
Makabila 120+,watu milioni 40+,na wote wawe na tabia moja.Hivi inahitaji rocket science ku-prove how wrong your thesis is?
Kwa taarifa yako,huwezi kuijadili (and kuihukumu,for that matter ) jamii pasipo to take into consideration power relations ndani ya jamii husika.Kuna tofauti kati ya matokeo na chanzo,kupenda/kutaka na kulazimishwa,nk.Labda tusaidie basi kutueleza chanzo cha hiyo "slowness",uvivu,uzembe,majungu,umbea,nk vinavyokwanza maendeleo yetu nikiamini kwamba unakubaliana nami kuwa HAVIJATOKEA TU GHAFLA.Is it Genetics?Superstition?
Halafu ni vigumu kufikia mwafaka,au hata to agree to disagree,na mitizamo kama "...Tena wa vijijini nusu yao nzima ni wafanyakazi wafu...".That's not overgeneralization ila ni sheer abuse of anaytical skills.Vijiji gani unavyozungumzia?Gezauleole na Kazimzumbwi,au Msolwa Ujamaa?Of course,baadhi ya mababu na mabibi zetu huko vijijini ni wafu (kwa mapenzi ya Mungu na wakati mwingine lack of medical facilities) lakini kuwaita wafu katika uhai wao....anyway,ndio freedom of speech!
Last edited: