Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,540
- Thread starter
- #161
Rev. Kishoka:
Mimi sipo Tanzania. Lakini nikichukua posts za JF kama public sentiment ya watanzania, maoni yangu yangekuwa sawa na mwandishi wa Economist kuhusu JK.
Kuna uwezekano mkubwa mwandishi ali-compile maoni yaliopo JF au watu wenye fikra za wana JF na kuyatolea article kwenye Economist.
Swali je watanzania ambao wanapiga kura na kumchagua rais wana-sentiment gani kuhusu JK?
Zakumi,
Nimekuwa nikijiuliza hili swali kuwa Economist wameandika ambacho tukitumia mahisabati hewa, tutasema ni wale 20% ambao hawakumpa kura Kikwete.
Sasa katika kutafakari hili, najiuliza wale wote waliomshangilia Kikwete na kumfanya tegemeo, wako wapi leo hii?
Nilipoandika "Thanks God for giving us Kikwete" wengi hawakunielewa, kwa kuwa walishajifunga kwa kuamuakuwa kwa kuwa Kikwete hana uwezo, basi hana manufaa.
Jibu langu kwako ni nyota na mbegu mpya iliyonguruma Busanda. Kama watu wameisikiliza hotuba ya Zitto na kuitafakari, basi itakuwa rahisi kwao kuamua kama wameridhika na walichopata kutokana na hizo kura 80% na uwakilishi wake pamoja na tabasamu au waamke.
Ikiwa hao 80% watasema wameridhika, hatuwezi kuwalazimisha wabadilishe utashi wao, lakini sisi tutaendelea na safari ya kujiendeleza na kujitegemea na kuwaacha wao waking'ang'ania Siasa Chafu na Uongozi Dhaifu mpaka siku machungu yatakapowazidi nao wakakata shauri na "kuokoka"!