'The Economist' Takes Gloves off on Kikwete...


Makabila 120+,watu milioni 40+,na wote wawe na tabia moja.Hivi inahitaji rocket science ku-prove how wrong your thesis is?

Kwa taarifa yako,huwezi kuijadili (and kuihukumu,for that matter ) jamii pasipo to take into consideration power relations ndani ya jamii husika.Kuna tofauti kati ya matokeo na chanzo,kupenda/kutaka na kulazimishwa,nk.Labda tusaidie basi kutueleza chanzo cha hiyo "slowness",uvivu,uzembe,majungu,umbea,nk vinavyokwanza maendeleo yetu nikiamini kwamba unakubaliana nami kuwa HAVIJATOKEA TU GHAFLA.Is it Genetics?Superstition?

Halafu ni vigumu kufikia mwafaka,au hata to agree to disagree,na mitizamo kama "...Tena wa vijijini nusu yao nzima ni wafanyakazi wafu...".That's not overgeneralization ila ni sheer abuse of anaytical skills.Vijiji gani unavyozungumzia?Gezauleole na Kazimzumbwi,au Msolwa Ujamaa?Of course,baadhi ya mababu na mabibi zetu huko vijijini ni wafu (kwa mapenzi ya Mungu na wakati mwingine lack of medical facilities) lakini kuwaita wafu katika uhai wao....anyway,ndio freedom of speech!
 
Last edited:

Wanaposema 44% ya budget ni pesa kutoka kwa wahisani, unafikiri wanasema bila kujua inatoka wapi? The pledged funds were 44 percent of $6 billions. Na karibia 44% [$2.4 billions] ya $6 billions haikutolewa na walioahidi. Kama takribani pesa zote zilizoahidiwa hazikutolewa, hii ina maana kuwa utegemezi ni asilimia takribani sifuri.

The good thing ni kwamba, angalau sasa unakubali kuwa $2.4 billion kati ya zilizoahidiwa hazikutolewa [na si kwamba zilitolewa halafu hazikutumika]. Unachotakiwa kuelewa sasa ni kuwa, kiasi kilichoahidiwa ni 44% ya $6 billion. Then, we will be on the same page.

"Sisi ni tegemezi karibia nusu ya bajeti yetu, tunaishi na kufa na misaada, period."

Yes. Sisi ni tegemezi karibia nusu ya bajeti [44%], at least on papers. Ukweli ni kwamba, hii misaada haipokelewi na Serikali. If I am wrong, then The Economist is also wrong. And since this debate stems from the article by The Economist , you will also be wrong.
 
Last edited:

umeona Barack Obama aliamuru ile kampuni ya bima kama sikosei warudishe bonases!! Kwahiyo bado kikwete anastahili lawama, kashindwa kufanya kile watu walicho kitegemea.
 
Lakini jamani hayo maisha bora ya wakenya yako wapi?? Katika 40m ya wakenya ni wangapi wanamaisha bora zaidi kutuzidi?? Kama ni usharp.... na ujambazi wa kutumia silaha nzito ni usharp??

Ni kweli serikali yetu ina matatizo hasa ya kuyumbishwa na mafisadi, ukiangalia walivyo uza TIPPER, mikataba ya madini, TICTS, ATC, TRC, n.k. ni ufisadi tu na kama tukipata rais kama magufuli mambo yatabadirika!!

Si kweli kwamba watanzania wote ni wavivu, mfumo wetu wa kazi katika ofisi nyingi ndo mbovu. Mambo mengi yana endeshwa kisiasa. Angalia wananchi na wasomi mbali mbali walivyo pinga kubinafsishwa kwa ATC, si ni sisi watanzania tulipinga lakini kwa kuwa rais mkapa alikuwa na azima yake ya ufisadi, alitumia mabavu akauza na je leo iko wapi?? Hao economist mbona hawa kulisemea hilo?? nani asiyejua kwamba nao ni wakoloni tu! World Bank na IMF walishabikia, uzeni benki, uzeni reli, uzeni ATC,..leo wako wapi na sera zao??

Watanzania tunacho hitaji sasa hivi ni rais na waziri mkuu kama magufuli (kama hata badirika) na enzi ya sokoine au mrema.
 

Sahihi kabisa nimekupata, tukiamua inawezekana. umetolea mfano wa kama tunataka kujenga barabara ya km 100 na inahitaji bil.200 kwa nini tusijenga hado hado km 10 kila mwaka?? Kawambwa uko wapi?? wewe ni mhandisi au unatuambia kwamba kile kibanda chako cha mbezi ulijenga kwa mkupuo?? mbona ulijenga aste aste?? hivyo hivyo kwenye miradi ya serikali, tutafika. Napinga hoja eti watanzania ni wazembe, niko kwenye ki-nchi fulani hapa watu ni wazembe mpaka basi lakini nchi inaendelea, issue hapa ni mipango na kuondoa ufisadi.
 
Sawa,sie wavivu,wazembe,watu wa majungu,nk according to Dilunga et al.Hawa je:

The Speaker's scapegoat: Official who signed off MPs' expenses didn't even have accountancy qualification
 
Sawa,sie wavivu,wazembe,watu wa majungu,nk according to Dilunga et al.Hawa je:




Ndo maana mimi nasema TZ bado we can still do better kama tukiamua kila mtu kwa nafasi yake tubadilike. Kama unaona bosi analeta mambo ya siasa ni kumpasha live na kazi inaendelea.

Hasa upande wa kuendeleza miradi ya maendeleo, tubajeti kulingana na uwezo na kama mradi unagharimu pesa nyingi basi tuutekeleze kwa awamu. Niliuliza kwa ndg. kawambwa mbona yeye alijenga kakibanda kake pale mbezi kwa awamu?? mbona kwenye miradi ya serilaki anataka aibuke na bil. 200?? kwa nini tusijenge kwa awamu (km 10 kwa mwaka?)
 
1. Mlalahoi, UK transparency ndo imefichua hayo madudu, na vema wameadmit watayafanyia kazi! Taabu ya Madudu ya Viongozi Tz ni usiri, na hata Slaa alipozungumzia maslahi ya wenzake, wao walimzomea!

2. JK wakati wa IMF meeting dar, aliulizwa na Bob kwa nini anasema anawajua wakwepa kodi Port ya dar na hawachukulii hatua ..kama raisi? Je JK ni mwoga naye? Ndo Jk alijiumauma tu.. na kutabasamu tu..hakuwa na jibu!
 

susuviri thanks for the good piece. Inabidi vilevile tuelewe kuwa "an efficient government" according to wazungu ni ile ambayo ina wafanikishia "looting of resources". Kenya haijawahi kukata mifija ya kinyonyaji ya wazungu tangu wapate uhuru, ndio maana, kila siku wanaisifia, na hawawezi kuibeza kamwe. After having said that, serikali ya kikwete ni kweli ni bomu sana. Kwanza sio serikali bali genge la wahumi, majangali na majambazi.
 
Wakuu zangu msilumbane kwa kitu kilichozungumzwa nusu nusu hapa.. Mnapozungumzia hizo 2.4/m ambazo hazikutumika iwe hazijatolewa au zimetolewa hakuna mahala economist wamesema hizo fedha ni asilimia 40 ya Budget ya mwaka unaohusika.. Yawezekana kabisa kuwa hizi fedha ni limbikizo toka mwaka 2006 au 2007 au 2008 kwani mara nyingi fedha hizi hutolewa/huahidiwa ktk jumla ya miaka fulani inaweza kuwa mitano, kumi au ishirini..

Kwa hiyo sioni sababu kabisa ya kuweka maneno zaidi ktk tafsiri ya maneno haya:- Tanzania is not even spending all the aid it is given. Last year, $2.4 billion of pledged funds were not disbursed. Na yawezekana kabisa hili neno disbursed tunalitafsiri vibaya kulingana na sentesi hii kwani yawezekana hiyo pay off inayozungumziwa hapa ni toka serikalini kwenda ktk Ujenzi wa nchi na sio kutoka kwa Wahisani...Nje ya hapo sentesi nzima ya maelezo ya economist hayaeleweki kabisa..
La muhimu kwetu ni kufahamu kwamba The economist wamezungumza kitu kile ambacho wengi hapa JF huwa hawaamini wanataka ushahidi na nadhalika toka kwa wananchi ambao maisha yao wenyewe ndio ushahidi unaotafutwa..
 
Tatizo letu ni kuwa tunapenda mno majibu mepesi. Majibu ambayo kila wakati tunaonyeshwa kuwa sisi ni victims! Majibu ambayo yanawanyooshea vidole wengine kwa matatizo yetu na sio sisi.

Leo tunawatolea macho watanzania wenye asili ya kiasia watano ati wao ndio chimbuko la ufisadi! Conveniently tunasahau kuwa Rais wetu, waziri wetu wa fedha, gavana wetu na bila shaka hadi tarishi anaebeba mafaili katika ofisi zote hizo ni mmatumbi. Tunasahau kuwa waziri Mkuu aliyepita, Waziri wa nishati na madini, Katibu Mkuu wake, Attorney General, mawakili na wataalamu wengine katika mawizara mengine na mashirika ya umma ni wamatumbi wenzetu. Lakini tunamuandama mtanzania mwenzetu tuliyetofautiana nae rangi kana kwake yeye ndiye aliyetushinikiza kuingia kwenye mkenge wa Richmond!

Leo Attorney General aliyepita na Gavana wa benki aliyepita wameonekana kuwa na vijisenti huko nje ambavyo inasemekana kuwa ni sehemu za mgao wao kutokana na mauzo ya rada! Lakini hapana, sisi tunamuona tena mtanzania mwenye asili ya asia kuwa ndio mhusika mkuu!

Leo wote tunajua kuwa waziri wetu wa madini alisaini miataba mibovu hotelini KWAKE! Mikataba ambayo ilikataliwa na wataalam wake. Lakini leo tunajaza thread tukiwasema hao wageni kuwa wao dio wanaotumalizia urithi wetu.

Leo tunalalamikia mgao wetu katika madini lakini hatujiulizi kuhusu athari ya matumizi mabaya ya mercury yanayofanywa na hao ndugu zetu tunaowaita wachimbaji wadogo wadogo!

Leo tunalilia urithi wetu wakati ni sisi wenyewe tunaotoa vibali kujenga mahoteli, viwanja vya ndege kwenye mbuga zetu. Tunang'ang'ania kujenga kiwanda katika mazalio pekee ya aina fulani ya flamingo DUNIANI. Tunatoa vibali kuubomoa mji wetu na kujenga maghorofa ambayo hatuna infrastructure ya kuhudumia!

Leo, wakati wenzetu wote wanabana mikanda, sisi tumo mbioni kutumia mabilioni kwa mradi hewa wa vitambulisho.

Leo wakati watoto wetu wanakufa kwa utapia mlo, tuliowachagua wanadai mamilioni tunayowalipa hayatoshi! Badala ya kujilinganisha na huyo wanaemwakilisha, waheshimiwa hawa wanajilinganisha na wezi wenzao wa taifa jirani! Na mbaya zaidi, mwakani tutawarudisha tena bungeni kuendeleza libeneke!

Hapana, ndugu zangu. Mpaka hapo tutakapoweza kuangaliana wenyewe na kudai majibu yasiyo na kificho, majibu ambayo yatatueleza kinaga ubaga matatizo yetu sisi raia wa nchi hii bila kujali rangi, jinsia au kabila, hatutatoka hapa tulipo!

Amandla.......
 
Last edited:

" Matatizo yanayotutatiza yanajulikana, njia za kuyatatua zipo, kwa nini hayatatuliwi ? "

ni kwasababu tumekosa agent of change ambaye/ambao watatumia njia hizo kutatua matatizo!
 

Fundi Mchundo:

Unayosema ni kweli lakini punguza kutumia kabila la wamatumbi katika mifano yako.

Tanzania ina makabila zaidi 120. Zinapofanyika shughuli za mafanikio Rungwe, mmatumbi hatajwi kama na yeye anaweza kufanya mafanikio hayo.

Yanapotokea makosa na mhehe au mzigua, mmatumbi anakuwa wa kutolewa mfano.

Hilo ni kabila la watu na si vizuri kuwa-victimize kwa makosa yanayofanywa na watu wengine ambao wamesoma na ambao walishasahau mila na desturi za makabila yao.
 
Rev. Kishoka:

Mimi sipo Tanzania. Lakini nikichukua posts za JF kama public sentiment ya watanzania, maoni yangu yangekuwa sawa na mwandishi wa Economist kuhusu JK.

Kuna uwezekano mkubwa mwandishi ali-compile maoni yaliopo JF au watu wenye fikra za wana JF na kuyatolea article kwenye Economist.

Swali je watanzania ambao wanapiga kura na kumchagua rais wana-sentiment gani kuhusu JK?
 
Mkuu watanzania gani tena si ndio wenye mawazo kama haya yetu tu yaani mawazo ya kimapinduzi zaidi na kukataa rasilimali za hii nchi kutumika ovyo
 

Nawaomba msamaha wamatumbi wenzangu wote kwa kutumia kabila letu kama mfano wa watanzania weusi. Tofauti na anavyodhani Zakumi, matumizi yangu ya kabila letu si victimisation bali kufanya suala la uasili kuwa karibu zaidi. Matumizi yangu ya neno mmatumbizi hayahusiani na kabila la mmatumbi. Katika mifano yangu mtu yeyote ambae ni mweusi Tanzania ni mmatumbi! Sasa badala ya neno mmatumbi sijui Mkuu Zakumi ungependekeza niwatofautishe watanzania weusi na wale wasio weusi? Neno mtanzania mweusi linakubalika?

Amandla.....
 

Vipi mijitu myeusi?
 

Call a spade a spade.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…