Mnajuaje kwamba UAE haijaipa Dubai Mamlaka ya kuingia IGA kwa kutumia article 120 ya katiba yao?
Mnafikiri wale wanasheria wa kimataifa wa DPW ni wajinga sana kuingia mkataba mkubwa hivi bila ya kupata clearance ya UAE?
Kama Dubai hawana nguvu ya kuingia IGA na hawajaruhusiwa na UAE, mbona hatujasikia UAE kulalamika?
Huu mkataba wa IGA tumeuona kwa kuvuja tu, na una kifungu cha kusema kuwa mikataba itakuwa ya siri, sasa mnajuaje makubaliano mengine ya siri kati ya Dubai na UAE, ambayo hayajavuja, yako vipi?
Hamuoni kwamba hii hoja
1. Ina utata sana.
2. Hatuna habari kamilifu kuhitimisha kuwa Dubai haijapewa nguvu za kusaini IGA.
3. Hata uchambuzi wa TLS umesema kwamba suala hili lInahitaji mwanasheria anayejua mambo ya uhusianinwa Dubai na UAE.
Kwa nini Madeleka anachagua jambo ambalo hana habari zake kamili kuupinga mkataba, wakati kuna mambo mengi ambayo tuna habari zake kamili anaweza kuyatumia?