The Emperor Jean-Bedel Bokassa

MaxShimba

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2008
Posts
35,771
Reaction score
4,065
Jean Bedel Bokassa alikuwa dikteta wa CAR, alikuwa na wake 17 na watoto hamsini. Alifanywa yatima wafaransa walipomuua baba yake akiwa na miaka 6.

Baada ya baba yake kufa mama yake naye alijiua.Alipigana WW2 chini ya wafaransa.

Baadaye alikuja kumpindua rais aliyekuwa ndugu yake mwaka 1965.Alijipa cheo cha field marshall na kutengeneza uniform maalumu sababu ya wingi wa medals alizojipa. Akienda kutembelea nchi alikuwa anagawa almasi.

Alikuwa ana majumba zaidi ya sita Ufaransa. Jumba yake la CAR lilikuwa na bwawa la mamba na simba wa kufugwa. alitumia mamba hao na simba kuulia wapinzani wake.

Wake zake walikuwepo mchina, mjerumani, msweden, mtunisia na mromania waliekutana club. Aliwaweka nyumba tofauti na alikuwa akiwatembelea daily na kusababisha jams.

Alijitawadha kuwa mfalme kwa sherehe ya 22m USD huku akipanda farasi kama wafalme wa ulaya.

Alipinduliwa na wafaransa baada ya kuua wanafunzi waliokua wanaandamana. Alifungia wanafunzi 30 kwenye jela ya mtu mmoja.

Walipompindua kwenye friji yake walikuta nyama za watu.

mwishoni mwa maisha yake alitumia kusoma bible na alikuwa anajiita mtume wa yesu. alifariki 1996.




NOTRE AMI L'EMPEREUR BOKASSA 1er PART 1 - YouTube

NOTRE AMI L'EMPEREUR BOKASSA 1er PART 2 - YouTube

NOTRE AMI L'EMPEREUR BOKASSA 1er PART 3.0 - YouTube

NOTRE AMI L'EMPEREUR BOKASSA 1er PART 4. - YouTube


Miongoni mwa watawala waliokuwa na visa na vituko vingi katika bara hili la Afrika ni mfalme wa kujipachika wa Afrika ya Kati, Jean-Bedel Bokassa.

Huyu bwana akiwa anaongoza nchi masikini kabisa duniani, alifanya sherehe ya kujisimika kama mfalme mwaka 1977 kwa kutumia kiasi cha sawa na shilingi trilioni 32. Lile taji lake la Ufalme peke yake liligharimu kiasi cha shilingi bilioni tatu!

Lakini yuko wapi hivi sasa na ameacha kitu gani duniani? Ujinga mtupu ambao unatusumbua sisi wanaadamu, hasa baadhi yetu tulio madarakani leo...
 
On 4 December 1977, the dictator Jean-Bedel Bokassa, 53, proclaimed himself "Emperor of the Central African Republic", a small country of two million people. It reproduces, for the occasion, the coronation of Napoleon Bonaparte in the Palais Omnisport de Bangui. This page exuberant history of post-colonial Africa, where excess borders on ridiculous, is also a concentration calculations, issues and abuse of "Françafrique". For the son who agitate this sinister puppet lead directly to the Elysee Palace and the President of the French Republic, Valéry Giscard d'Estaing. France has not only sanctioned, but funded in part Bokassa's whim.





Bokassa Ier Empereur De Françafrique (LCP 2011) - YouTube
 
Bora ulivyotufahamisha kuna mfalme huyu duniani
 




Miongoni mwa watawala waliokuwa na visa na vituko vingi katika bara hili la Afrika ni mfalme wa kujipachika wa Afrika ya Kati, Jean-Bedel Bokassa. Huyu bwana akiwa anaongoza nchi masikini kabisa duniani, alifanya sherehe ya kujisimika kama mfalme mwaka 1977 kwa kutumia kiasi cha sawa na shilingi trilioni 32. Lile taji lake la Ufalme peke yake liligharimu kiasi cha shilingi bilioni tatu!

Lakini yuko wapi hivi sasa na ameacha kitu gani duniani? Ujinga mtupu ambao unatusumbua sisi wanaadamu, hasa baadhi yetu tulio madarakani leo.............
 
Unamaanisha Jakaya madaraka yamempanda kichwani na yeye au?
 
Huyu si ndiye niliyepata kusikia alikkuwa carnibal (alikuwa anakula nyama za watu).? Ama ni mwingine.?
 
Acha uchonganishi, nimezungumzia vituko vya huyo mfalme wa Afrika ya Kati na si vinginenvyo.....
Itabidi ukaedit mstari wako wa mwisho ili post yako iendane na msimamo uliouonyesha hapa ama sivyo wengi watapotoka alafu uwaite wachonganyishi.Katika utawala wetu wa sasa unapotoa mfano wa rais au mfalme wa taifa lingine,unamaanisha unatuambie tumuangilie na rais wetu pia,
 
Acha uchonganishi, nimezungumzia vituko vya huyo mfalme wa Afrika ya Kati na si vinginenvyo.....

sa lengo lako nini hapo kama c uchonganish... kila mtu atakufa, bt death is nt a purpose as to why we ar livin in this world, we hav sthing to accomplish!!! kuna m2 alisema this lif is nt about length, bt how deep u liv it!! ni muhimu kuwatendea binadam wenzako hak.. .il uish milele coz rightous never die.. see Nyereres, mandelas, Nkurumah etc..
 
Wewe una agenda yako, ulikuwa unatafuta pakuipitishia tu.....
 
Mkuu Mtambuzi

Haujaandika jina la nchi aliyokuwa anaitawala Bokassa.
 
Viongozi wa africa wengi ni wabinafsi
"Vox popoli vox dei"
 
kuna kalenda fulani hivi ya "the world's worst dictators" km sikosei na huyu jamaa nilimuona kwenye picha za madikteta wale kwenye ile kalenda
 
Mkuu
Kiongozi siyo Rais tu hata mimi nikiongozi wa familia yangu, labda angesema (watawala walioko madarakani.......) hapo tungekuwa na sababu ya kumrushia virungu. La sivyo maelezo yake yanajitosheleza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…