Mwelewa
JF-Expert Member
- Jan 5, 2011
- 2,343
- 3,284
Mleta mada alileta observation yake kama ndiyo final say ndiyo maana wakatokea wengine kusema hakuna lolote hapo.Kila mtu ana mtazamo wake ndio maana hatufanani akili wala maarifa.
Mtu mwingine anaweza kuona The bold amna kitu ana-tafsiri tu kutoka kwenye kiingereza kuleta kwenye kiswahili pengine ni kweli au ni uongo vyovyote iwavyo lakini kusoma kitu ukakielewa na kuweza kumuelewesha mtu mwingine kile ulichokisoma na akaelewa ni kipaji kikubwa mno.
Kuna walimu kibao mashuleni pamoja ya kuwa wamesomea uhalimu ila hawana kipaji cha kumuelewesha mwanafunzi na mwanafunzi akamuelewa.
Mi nampa Credit The bold kwa kile anachokifanya....Uwezo wake wa kuandika ni mkubwa mno sio Kila mtu Ana Uwezo wa namna ile kama unadhani ni kitu rahisi ingia uko mitandaoni mnaposema anapata habari na wewe soma na uje hapa kutafsiri tuone kama utaufikia ubora wake!!!!!
Kwangu mimi naungana na mtoa mada....Na naungana na wale waliotaja watu wengine pia maana kila mtu Ana mtazamo ila mtazamo wako usifanye uone juhudi za The bold ni amna kitu tusiwe wanafiki.
Si ndiyo mjadala unavyokuwa?
Kwamba ukiwasilisha mawazo yako kwa hadhira basi tegemea maoni zofauti.
Na hapa ndipo walipoibuka wanaosema no.....wapo wajuvi zaidi.
Usipokuwa free thinker huwezi ona hili.