Hapo kwa Zizou hakuna ubishi, kwa hizi karne mbili sijamuona kiungo kama Zizou
Neymar anacheza vizuri akitokea pembeni, Ronaldo alikua mshambuliaji wa kati, no.9, Ronaldo pamoja na skills alikua na nguvu na stamina ya ajabu kupasua kuta ngumu bila kuangukaanguka hovyo kama huyu dogo, ungesema Neymar kafanana mpira na Christina labla
Pele ni siasa tu, hamgusi hata Ronaldo de Lima huyo kigagula, alikua mshambuliaji design ya kina Inzaghi, Van Nesterooy, pele hakua na uwezo wa kupasua ukuta na skills kama za de Lima, alikua muoteaji tu kazi kubwa ilifanywa na wachezaji wasiopewa sifa leo hii kama Carlos Alberto na Garrincha na alifunga magoli mengi sana ambayo otherwise yalikua offside kutokana na sheria za kipuuzi za kipindi chake.
Mungu wa soccer anaitwa Diego Armando 'D10S' Maradona, hakuna pele wala upele. Kila skills unayoiona leo kwenye soka ilikua invented na Dios including ile chenga ya Zidane 360 au helicopter kwa jina jingine, what Pele could do with a football, Maradona could do it better with a golf ball