Freiston
JF-Expert Member
- Oct 25, 2020
- 302
- 340
Katika pitapita yangu mitandaoni, nikakutana na taarifa hii kwenye gazeti maarufu la THE GUARDIAN yenye kichwa cha habari: South Korea's population falls for first time in its history | South Korea | The Guardian ambayo inaongelea kuhusu kushuka kwa idadi ya watu nchini Korea ya Kusini kwa mara ya kwanza katika historia.
Taarifa hii inasema mpaka kufikia mwaka 2067, asilimia 46 ya wakorea watakuwa watu wa umri wa zaidi ya miaka 64 na idadi ya watu kushuka kutoka 51 milioni mpaka 39 milioni endapo hali ya sasa inachagiza kushuka kwa idadi yao itaendelea kuwa hivyo. Na kwa wakati huo huo idadi ya watu kwa bara Africa kuongezeka na umri wa wastani kuwa ni miaka 25 (sikumbuki chanzo cha taarifa hii nilikiona wapi maana sikitilia maanani mpaka nilipoona taarifa ya SK). Sasa tatizo hili sio kwa taifa hilo tu bali ni kwa mataifa mengi ya Ulaya kama Ufaransa.
Sasa mimi kama kijana mtanzania, nikaona hiyo ni fursa kwetu na kwa kizazi chetu katika mitizamo miwili.
1. Mataifa mengi ya Ulaya na Asia yanazidi kupoteza nguvukazi na hivyo kuwa tegemezi kwa Africa katika masuala mengi hasa mazao ya chakula.
USHAURI:
Naiomba serikali na mashirika binafsi itoe mafunzo kwa vijana na watoto wetu tangu elimu ya awali mbinu mpya na za kisasa za kilimo ili uzalishaji wa mazao mbalimbali kuongezeka kwa matumizi ya ndani na nje ya nchi hasa katika mazao ya kimkakati.
Kuwe na mashamba ya serikali/watu binafsi watakaowezeshwa na serikali au taasisi binafsi ambayo yaweza kutoa internship kwa vijana kwenda kujifunza kilimo kwa vitendo na baada ya hapo vijana kuunganisha kimakundi na kuanzisha miradi yao binafsi kwa maslahi ya Taifa. Mkazo ukiwa zaidi katika kushikilia mnyororo mzima wa kuongeza thamani ili bidhaa iende kwa mlaji moja kwa moja.
2. Nguvukazi. Vijana wengi wa mataifa ya Africa wanatoka katika nchi zao na kwenda kufanya kazi kwenye mataifa ya Ulaya, Asia na Marekani kisha fedha wanazopata hutuma nyumbani. Fursa hii bado haijachangamkiwa sana na watanzania wengi labda ni kutoka na Taifa kutokuwa na mipango thabiti ya kutafuta fedha za kigeni kupitia diaspora au ipo lakini watendaji bado wamelala mpaka baba aseme kama kawaida yao ya kupenda kusukumwa au labda mimi sina uelewa sana juu ya kinachoendelea.
Yote kwa yote, ninaishauri serikali yetu iweke mipango ya muda mfupi na muda mrefu katika kutengeneza nguvukazi itakayoenda kuvuna fedha hizi za kigeni katika mataifa ambayo nguvu kazi yao inapungua kwa kasi. Ni muhimu vijana wakafuzwa maadili mema ya nchi yetu na uzalendo kwa taifa letu ili watakapokuwa huko waendelee kuwa watiifu kwa taifa letu na kwa uamini wao na uchapaji kazi basi Taifa lipate sifa. Lugha za kimataifa zitiliwe mkazo mashuleni kwetu ili iwe rahisi kuingia katika soko la ajira la nchi hizo.
Kwa leo naomba niishie hapo.
Disclaimer: Mimi sio shabiki wa chama chochote cha siasa ila ni muumini wa serikali iliyo madarakani kwa sababu ya imani yangu kunifundisha kuheshimu mamlaka zilipo, kwa kuwa zote zatoka kwa Mungu. Kwa ambao nimewakwaza kwa maoni yangu, waniwie radhi.
Ahsanteni
Mwisho