The Guardian: Kuhusu kushuka kwa idadi ya watu wa Nchi ya Korea Kusini

Mkuu kashasema "fyatueni tu" ameona mbali sana! Hayo kwa wakolea ni mazao ya uzazi wa mpango!
Lakini hakuwa na maana hiyo... strategic planning na sio ile planning nyingine. Wanatutesea mama zetu tu bure. Halafu ushawahi kujiuliza ni kwanin kwa wanawake na sio wanaume... most scientists are men.... haki sawa
 
Hao ni wapumbavu, kwani duniani ardhi imeisha hadi wahangaike kote huko angani?
Hahhahahhahaha na ujue ya hapa yamewashinda. Ardhi zetu zenye rutuba zinazidi kuharibiwa tu in the name of science and technology.
 
Katika pitapita yangu mitandaoni, nikakutana na taarifa hii kwenye gazeti maarufu la THE GUARDIAN yenye kichwa cha habari: South Korea's population falls for first time in its history | South Korea | The Guardian ambayo inaongelea kuhusu kushuka kwa idadi ya watu nchini Korea ya Kusini kwa mara ya kwanza katika historia.

Taarifa hii inasema mpaka kufikia mwaka 2067, asilimia 46 ya wakorea watakuwa watu wa umri wa zaidi ya miaka 64 na idadi ya watu kushuka kutoka 51 milioni mpaka 39 milioni endapo hali ya sasa inachagiza kushuka kwa idadi yao itaendelea kuwa hivyo. Na kwa wakati huo huo idadi ya watu kwa bara Africa kuongezeka na umri wa wastani kuwa ni miaka 25 (sikumbuki chanzo cha taarifa hii nilikiona wapi maana sikitilia maanani mpaka nilipoona taarifa ya SK). Sasa tatizo hili sio kwa taifa hilo tu bali ni kwa mataifa mengi ya Ulaya kama Ufaransa.

Sasa mimi kama kijana mtanzania, nikaona hiyo ni fursa kwetu na kwa kizazi chetu katika mitizamo miwili.
1. Mataifa mengi ya Ulaya na Asia yanazidi kupoteza nguvukazi na hivyo kuwa tegemezi kwa Africa katika masuala mengi hasa mazao ya chakula.

USHAURI:

Naiomba serikali na mashirika binafsi itoe mafunzo kwa vijana na watoto wetu tangu elimu ya awali mbinu mpya na za kisasa za kilimo ili uzalishaji wa mazao mbalimbali kuongezeka kwa matumizi ya ndani na nje ya nchi hasa katika mazao ya kimkakati.

Kuwe na mashamba ya serikali/watu binafsi watakaowezeshwa na serikali au taasisi binafsi ambayo yaweza kutoa internship kwa vijana kwenda kujifunza kilimo kwa vitendo na baada ya hapo vijana kuunganisha kimakundi na kuanzisha miradi yao binafsi kwa maslahi ya Taifa. Mkazo ukiwa zaidi katika kushikilia mnyororo mzima wa kuongeza thamani ili bidhaa iende kwa mlaji moja kwa moja.

2. Nguvukazi. Vijana wengi wa mataifa ya Africa wanatoka katika nchi zao na kwenda kufanya kazi kwenye mataifa ya Ulaya, Asia na Marekani kisha fedha wanazopata hutuma nyumbani. Fursa hii bado haijachangamkiwa sana na watanzania wengi labda ni kutoka na Taifa kutokuwa na mipango thabiti ya kutafuta fedha za kigeni kupitia diaspora au ipo lakini watendaji bado wamelala mpaka baba aseme kama kawaida yao ya kupenda kusukumwa au labda mimi sina uelewa sana juu ya kinachoendelea.

Yote kwa yote, ninaishauri serikali yetu iweke mipango ya muda mfupi na muda mrefu katika kutengeneza nguvukazi itakayoenda kuvuna fedha hizi za kigeni katika mataifa ambayo nguvu kazi yao inapungua kwa kasi. Ni muhimu vijana wakafuzwa maadili mema ya nchi yetu na uzalendo kwa taifa letu ili watakapokuwa huko waendelee kuwa watiifu kwa taifa letu na kwa uamini wao na uchapaji kazi basi Taifa lipate sifa. Lugha za kimataifa zitiliwe mkazo mashuleni kwetu ili iwe rahisi kuingia katika soko la ajira la nchi hizo.

Kwa leo naomba niishie hapo...

Disclaimer: Mimi sio shabiki wa chama chochote cha siasa ila ni muumini wa serikali iliyo madarakani kwa sababu ya imani yangu kunifundisha kuheshimu mamlaka zilipo, kwa kuwa zote zatoka kwa Mungu. Kwa ambao nimewakwaza kwa maoni yangu, waniwie radhi.

Ahsanteni

Mwisho
Natamani mawaziri na Rais akusikie ushauri bora sana kwa uzalendo wako
 
Naona haujanielewa, hamna cha kubadilishana siti hapo, mimi binafsi n mtaalam wa hayo makitu ya software development, kwa mfumo kama huo mtu mmoja aliyekaa nyuma ya computer atafanya kazi ya hao wakata tiketi kama 1,000 pia kumbuka sio hao tu, kuna makampuni yaliyokua yanachapsha hizo tiketi ikiwemo na familia zao, yaani watu wengi tu watabak bila ajira.
Nilikuelewa vizuri tu ndugu. Labda nikuulise swali, kuna haja kweli kwa nchi kuacha kuboresha teknolojia zetu kwa minajili ya kuwa kuna watu watakosa ajira??? Tufikirie kwanza ndani ya box tukimaliza tuangalie na nje... majibu mbona yapo.

Mfano coaster moja inaweza kubeba abiria zaidi 20 kwa wakati mmoja (kama siko sahihi nirekebishe) lakini taksi inaweza beba abiria maaybe wa3 kwa wakati mmoja, sasa je ili tusiue soko la taksi basi na tupige marufuku uingizwaji wa coaster nchini, vipi kuhusu bajaji vs bodaboda... vipi kuhusu trakta vs jembe la mkono... kupoteza ajira kwa hao kutasababisha wengine wapate ajira pia (sisemi hivi kama mtu asiye na huruma ila competition katiak dunia yetu ni jambo lililo vizazi na vizazi).

Kuna wakati sisi kama vijana tuliosoma kwa kodi za watanzania wenzetu kuonesha mfano katika kukubali mabadiliko ya teknolojia iwe kwa hiari au lah. Tukiwa tunaangalia upande mmoja tu wa shilingi tutakuwa tunakosea. Let's weigh the pros and cons, kisha tuamue. Nauli na muda ambao ningeutumia kwenda kukata tiketi sasa naweza kuutumia kufanya shughuli nyingine za uzalishaji mali. Kama unaishi dar (mimi sipo huko) unaweza ukaelewa thamanj ya muda vs kwenda kukata tiketi.

Ahsante
 
Natamani mawaziri na Rais akusikie ushauri bora sana kwa uzalendo wako
Ahsante sana kwa kuliona hilo... natumai utawaelimisha vijana wengine pia nao waelewe kuwa duniani kuna opportunity nyingi ili tuendelee kuishauri serikali yetu kutunga sera zinazoendana na karne ya sasa hasa katika kuhakikisha vijana wanapata ajira za nje ya nchi hasa barani Ulaya na America lakini pia zifanyiwe kazi na sio kuwekwa kabatini.
 
Mkuu umenena vyema sana. Dunia ya sasa inakimbizana na inventions and innovations alafu mtu anakuja kuongelea swala la idadi ya watu as tuko 16th Century.
Hata hiko kilimo anachokiongelea kama hatutahamasisha kilimo chenye kutumia dhana bora, njia za kisiasa tukiachana na hiki cha mazoea tutabaki hapahapa tukiendelea kupeana takwimu za kufoji na kuaminishana ujinga.
Labda ngoja nikuambia kwanini idadi ya watu ni kitu muhimu sana. Kwa mfano ushawahi kujua kwanini mapato ya nchi hukusanywa zaidi dar es salaam kuliko mikoa mingine, vipi kuhusu population yao... na ndo sehemu inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watu... ni coincidence ama. Siku zote soko lazima liendane na idadi ya watu (supply and demand), kama unazalisha huna pa kuuza then what...? Soko la Afrika mashariki na SADC huoni watu huungana kwa sababu ya kuincrease number...
 
jibu
Swali ni moja tu, je kujua ndio kutenda???
Jibu mbona liko wazi... kupanga sio kutenda. Ila kutenda ni matokeo kupanga kutokupanga kupanga. 🙂

Samahani kama nimekuchanganya.
 
Na africa kizazi wanawake wasiotaka kuzaa kinaongeza pia wale wa kuzaa watoto watano wamepungua, na pia kushika mimba miaka ya karibuni imekuwa ngumu na pia gharama za kujifungua vipo juu
 
Nilikuelewa vizuri tu ndugu. Labda nikuulise swali, kuna haja kweli kwa nchi kuacha kuboresha teknolojia zetu kwa minajili ya kuwa kuna watu watakosa ajira??? Tufikirie kwanza ndani ya box tukimaliza tuangalie na nje... majibu mbona yapo.

Mfano coaster moja inaweza kubeba abiria zaidi 20 kwa wakati mmoja (kama siko sahihi nirekebishe) lakini taksi inaweza beba abiria maaybe wa3 kwa wakati mmoja, sasa je ili tusiue soko la taksi basi na tupige marufuku uingizwaji wa coaster nchini, vipi kuhusu bajaji vs bodaboda... vipi kuhusu trakta vs jembe la mkono... kupoteza ajira kwa hao kutasababisha wengine wapate ajira pia (sisemi hivi kama mtu asiye na huruma ila competition katiak dunia yetu ni jambo lililo vizazi na vizazi).

Kuna wakati sisi kama vijana tuliosoma kwa kodi za watanzania wenzetu kuonesha mfano katika kukubali mabadiliko ya teknolojia iwe kwa hiari au lah. Tukiwa tunaangalia upande mmoja tu wa shilingi tutakuwa tunakosea. Let's weigh the pros and cons, kisha tuamue. Nauli na muda ambao ningeutumia kwenda kukata tiketi sasa naweza kuutumia kufanya shughuli nyingine za uzalishaji mali. Kama unaishi dar (mimi sipo huko) unaweza ukaelewa thamanj ya muda vs kwenda kukata tiketi.

Ahsante

Ndio maana nimesema hukunielewa, hamna sehemu nimepinga wala kusema Afrika tuache teknolojia, nimekuambia mimi ni mtaalam wa masuala ya teknolojia hivyo huwa nipo mstaari wa mbele kwenye kupigia debe mifumo, japo na yenyewe huwa inaathiri pakubwa soko la ajira, lakini pia inaboresha ufanisi na pia kuongeza mapato, ni shilingi yenye sura mbili, inaboresha ila inaacha wengine wakiwa hoi, hata hivyo muhimu twende tu hivyo.

Issue yangu ilikua kwa hizo kauli za kusema watu wafyatue watoto ili kuongeza nguvu kazi, sio kwa ulimwengu wa leo.
 
Now we are good. Hata mimi siungi mkono, ila mtoto ni baraka kutoka kwa Mungu akija mpokee... mkumbuke Sara wa kwenye Biblia.
 
Na africa kizazi wanawake wasiotaka kuzaa kinaongeza pia wale wa kuzaa watoto watano wamepungua, na pia kushika mimba miaka ya karibuni imekuwa ngumu na pia gharama za kujifungua vipo juu
Ni kweli hata takwimu zao zinaonyesha hivo. Ila shida ni kuwa kwa wenzetu birth rate ni below 1 wakati kwetu ni above 1.5 unaona tofaut hapo.
 
jibu

Jibu mbona liko wazi... kupanga sio kutenda. Ila kutenda ni matokeo kupanga kutokupanga kupanga. 🙂

Samahani kama nimekuchanganya.

Kujua na kutenda ni sawa??
 
Yeah wewe ndo umemfanya aibe ikiwa unataka kufikiria hivyo.... ila kama unataka tuelimishane niruhusu.

Huwa tunafundishwa ya kuwa kila jambo hufanyika katika ulimwengu wa roho kabla ya kujidhihirisha katika mwili. Ukijiambia wewe kuwa utaenda kuiba na ukadhamiria kufanya hivyo basi utaiba kweli. Lakini pia inawezekana pia ukamuombea mtu mabaya na yakamkuta.

Mfano mtu anaweza kwenda kwa mganga kumfanya mwingine awe chini ma inakuwa. Sasa je ukipanga kumuwazia mwenzio kuiba je nani kamfanya mwingine aibe kama akiende kuiba kweli hapo? Spiritual power - usimnenee mwenzako mabaya kwanini?... Majibu unayo.

Hata hivo dhana ya kuhusu mpango wa Mungu inahitaji kiongozi wa kiroho aweze kuongelea juu ya hilo lasivyo unawezaleta mkanganyiko kwako na kwa wengine. Ila kama unabisha ntakuuliza swali ukijibu basi ntaelewa kuwa wewe ni mwelewa wa mambo au unabisha tu.

Swali: Unaamini Mungu wako unayemuamini anaijua leo na kesho yako? Je haimaanishi ya kuwa tayari anafahamu mwezi ujao utaenda kuiba?

Swali mbona ni dogo tu lisilohitaji maneno mengi!!, je kujua na kutenda ni sawasawa??---
 
Labda ngoja nikuambia kwanini idadi ya watu ni kitu muhimu sana. Kwa mfano ushawahi kujua kwanini mapato ya nchi hukusanywa zaidi dar es salaam kuliko mikoa mingine, vipi kuhusu population yao... na ndo sehemu inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watu... ni coincidence ama. Siku zote soko lazima liendane na idadi ya watu (supply and demand), kama unazalisha huna pa kuuza then what...? Soko la Afrika mashariki na SADC huoni watu huungana kwa sababu ya kuincrease number...
When we come into demand and supply idadi ya watu sio issue mkuu. Unaweza ukawa na watu wachache lakini wakawa na demand kubwa kuliko idadi kubwa ya watu. What if watu ni wengi but they don't afford the commodities' prices due to small number of people who are earning high income comparing to large number of people in the country.?
Kwahiyo population increment is not an important issue in this era of technology advancement.
Kama ingetokea miaka 200 au 100 nyuma kwasasa ingefaa sana
 
Ok, if that is the case then, Kujua jambo kwa Mungu hukuhusiani na utendaji wake kwa hilo jambo.
Labda nikurahisishie kazi ndugu yangu. Ni hivi Mungu ndiye muweza wa yote, Mungu ndiye mpangaji wa yote, Mungu ndiye hujua kesho yetu, Mungu kila kitu... na hata shetani alishaongeaga na Mungu aende kumjaribu Ayubu na akaruhusiwa ingawa kwa masharti.

Sasa mimi nawewe tuna haja gani ya kuzozana. Hebu kwa mfano ukija kiimani hata serikali iliyo madarakani sass unadhani Mungu hakujua yenyewe ndo itakuwepo, je asingeweza kuzuia isiwepo, kwanini kaacha iwepo, ana makusudi yake na ndo hapo mimi naww hatupaswi kuhoji... Mipango ya Mungu hatuwezi kupingana nayo...
 
Katika pitapita yangu mitandaoni, nikakutana na taarifa hii kwenye gazeti maarufu la THE GUARDIAN yenye kichwa cha habari: South Korea's population falls for first time in its history | South Korea | The Guardian ambayo inaongelea kuhusu kushuka kwa idadi ya watu nchini Korea ya Kusini kwa mara ya kwanza katika historia.

Taarifa hii inasema mpaka kufikia mwaka 2067, asilimia 46 ya wakorea watakuwa watu wa umri wa zaidi ya miaka 64 na idadi ya watu kushuka kutoka 51 milioni mpaka 39 milioni endapo hali ya sasa inachagiza kushuka kwa idadi yao itaendelea kuwa hivyo. Na kwa wakati huo huo idadi ya watu kwa bara Africa kuongezeka na umri wa wastani kuwa ni miaka 25 (sikumbuki chanzo cha taarifa hii nilikiona wapi maana sikitilia maanani mpaka nilipoona taarifa ya SK). Sasa tatizo hili sio kwa taifa hilo tu bali ni kwa mataifa mengi ya Ulaya kama Ufaransa.

Sasa mimi kama kijana mtanzania, nikaona hiyo ni fursa kwetu na kwa kizazi chetu katika mitizamo miwili.
1. Mataifa mengi ya Ulaya na Asia yanazidi kupoteza nguvukazi na hivyo kuwa tegemezi kwa Africa katika masuala mengi hasa mazao ya chakula.

USHAURI:

Naiomba serikali na mashirika binafsi itoe mafunzo kwa vijana na watoto wetu tangu elimu ya awali mbinu mpya na za kisasa za kilimo ili uzalishaji wa mazao mbalimbali kuongezeka kwa matumizi ya ndani na nje ya nchi hasa katika mazao ya kimkakati.

Kuwe na mashamba ya serikali/watu binafsi watakaowezeshwa na serikali au taasisi binafsi ambayo yaweza kutoa internship kwa vijana kwenda kujifunza kilimo kwa vitendo na baada ya hapo vijana kuunganisha kimakundi na kuanzisha miradi yao binafsi kwa maslahi ya Taifa. Mkazo ukiwa zaidi katika kushikilia mnyororo mzima wa kuongeza thamani ili bidhaa iende kwa mlaji moja kwa moja.

2. Nguvukazi. Vijana wengi wa mataifa ya Africa wanatoka katika nchi zao na kwenda kufanya kazi kwenye mataifa ya Ulaya, Asia na Marekani kisha fedha wanazopata hutuma nyumbani. Fursa hii bado haijachangamkiwa sana na watanzania wengi labda ni kutoka na Taifa kutokuwa na mipango thabiti ya kutafuta fedha za kigeni kupitia diaspora au ipo lakini watendaji bado wamelala mpaka baba aseme kama kawaida yao ya kupenda kusukumwa au labda mimi sina uelewa sana juu ya kinachoendelea.

Yote kwa yote, ninaishauri serikali yetu iweke mipango ya muda mfupi na muda mrefu katika kutengeneza nguvukazi itakayoenda kuvuna fedha hizi za kigeni katika mataifa ambayo nguvu kazi yao inapungua kwa kasi. Ni muhimu vijana wakafuzwa maadili mema ya nchi yetu na uzalendo kwa taifa letu ili watakapokuwa huko waendelee kuwa watiifu kwa taifa letu na kwa uamini wao na uchapaji kazi basi Taifa lipate sifa. Lugha za kimataifa zitiliwe mkazo mashuleni kwetu ili iwe rahisi kuingia katika soko la ajira la nchi hizo.

Kwa leo naomba niishie hapo.

Disclaimer: Mimi sio shabiki wa chama chochote cha siasa ila ni muumini wa serikali iliyo madarakani kwa sababu ya imani yangu kunifundisha kuheshimu mamlaka zilipo, kwa kuwa zote zatoka kwa Mungu. Kwa ambao nimewakwaza kwa maoni yangu, waniwie radhi.

Ahsanteni

Mwisho
Mamlaka ya kuteka na kuua wakina azory gwanda, na ben saanane, mamlaka ya kuiba kura, mamlaka ya kujenga uwanja wa ndege vijijini kwao ilhali hamna wateja na watoto wanakaa chini shuleni zote hizo. Zimetoka kwa mungu?
 
Kama utaamini hivo, itakuwa vyema zaidi. Ila sidhani kama hiyo ndo mada hapo juu. Tafadhali rejea katika mada na utoe mchango wako kama hutojali. Kuhusu hayo mengine natumai kuna nyuzi ama waweza anzisha nyuzi yako kuongelea jambo hilo. Na hakika utapata wachangiaji wengi ikiwamo mimi mwenyewe. Ahsante
 
Back
Top Bottom