Demi
JF-Expert Member
- Nov 22, 2016
- 40,466
- 88,695
Kila kitu hapa duniani hupangwa na Mungu.Hata Hitler, Amin, Firauni nk, walitoka kwa Mungu??!!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kila kitu hapa duniani hupangwa na Mungu.Hata Hitler, Amin, Firauni nk, walitoka kwa Mungu??!!
Kila kitu hapa duniani hupangwa na Mungu.
Mungu anajua mipango yote ya mwanadamu tangu anazaliwa, yaani anaijua fika future yangu. So mpangaji ni yeye.Kila kitu duniani kimepangwa na Mungu???, je uzinzi, wizi, ujambazi, nk, vyote vimepangwa na Mungu???
Mungu anajua mipango yote ya mwanadamu tangu anazaliwa, yaani anaijua fika future yangu. So mpangaji ni yeye.
Usijifananishe na Mungu.Kujua jambo na kupanga jambo ni sawasawa???, mfano mimi nikijua kwamba mtu fulani ataiba na kweli akaiba je mimi ndiye nitakuwa nimepanga au nimemfanya aibe???
Mkuu kashasema "fyatueni tu" ameona mbali sana! Hayo kwa wakolea ni mazao ya uzazi wa mpango!Katika pitapita yangu mitandaoni, nikakutana na taarifa hii kwenye gazeti maarufu la THE GUARDIAN yenye kichwa cha habari: South Korea's population falls for first time in its history | South Korea | The Guardian ambayo inaongelea kuhusu kushuka kwa idadi ya watu nchini Korea ya Kusini kwa mara ya kwanza katika historia.
Taarifa hii inasema mpaka kufikia mwaka 2067, asilimia 46 ya wakorea watakuwa watu wa umri wa zaidi ya miaka 64 na idadi ya watu kushuka kutoka 51 milioni mpaka 39 milioni endapo hali ya sasa inachagiza kushuka kwa idadi yao itaendelea kuwa hivyo. Na kwa wakati huo huo idadi ya watu kwa bara Africa kuongezeka na umri wa wastani kuwa ni miaka 25 (sikumbuki chanzo cha taarifa hii nilikiona wapi maana sikitilia maanani mpaka nilipoona taarifa ya SK). Sasa tatizo hili sio kwa taifa hilo tu bali ni kwa mataifa mengi ya Ulaya kama Ufaransa.
Sasa mimi kama kijana mtanzania, nikaona hiyo ni fursa kwetu na kwa kizazi chetu katika mitizamo miwili.
1. Mataifa mengi ya Ulaya na Asia yanazidi kupoteza nguvukazi na hivyo kuwa tegemezi kwa Africa katika masuala mengi hasa mazao ya chakula.
USHAURI:
Naiomba serikali na mashirika binafsi itoe mafunzo kwa vijana na watoto wetu tangu elimu ya awali mbinu mpya na za kisasa za kilimo ili uzalishaji wa mazao mbalimbali kuongezeka kwa matumizi ya ndani na nje ya nchi hasa katika mazao ya kimkakati.
Kuwe na mashamba ya serikali/watu binafsi watakaowezeshwa na serikali au taasisi binafsi ambayo yaweza kutoa internship kwa vijana kwenda kujifunza kilimo kwa vitendo na baada ya hapo vijana kuunganisha kimakundi na kuanzisha miradi yao binafsi kwa maslahi ya Taifa. Mkazo ukiwa zaidi katika kushikilia mnyororo mzima wa kuongeza thamani ili bidhaa iende kwa mlaji moja kwa moja.
2. Nguvukazi. Vijana wengi wa mataifa ya Africa wanatoka katika nchi zao na kwenda kufanya kazi kwenye mataifa ya Ulaya, Asia na Marekani kisha fedha wanazopata hutuma nyumbani. Fursa hii bado haijachangamkiwa sana na watanzania wengi labda ni kutoka na Taifa kutokuwa na mipango thabiti ya kutafuta fedha za kigeni kupitia diaspora au ipo lakini watendaji bado wamelala mpaka baba aseme kama kawaida yao ya kupenda kusukumwa au labda mimi sina uelewa sana juu ya kinachoendelea.
Yote kwa yote, ninaishauri serikali yetu iweke mipango ya muda mfupi na muda mrefu katika kutengeneza nguvukazi itakayoenda kuvuna fedha hizi za kigeni katika mataifa ambayo nguvu kazi yao inapungua kwa kasi. Ni muhimu vijana wakafuzwa maadili mema ya nchi yetu na uzalendo kwa taifa letu ili watakapokuwa huko waendelee kuwa watiifu kwa taifa letu na kwa uamini wao na uchapaji kazi basi Taifa lipate sifa. Lugha za kimataifa zitiliwe mkazo mashuleni kwetu ili iwe rahisi kuingia katika soko la ajira la nchi hizo.
Kwa leo naomba niishie hapo...
Disclaimer: Mimi sio shabiki wa chama chochote cha siasa ila ni muumini wa serikali iliyo madarakani kwa sababu ya imani yangu kunifundisha kuheshimu mamlaka zilipo, kwa kuwa zote zatoka kwa Mungu. Kwa ambao nimewakwaza kwa maoni yangu, waniwie radhi.
Ahsanteni
Mwisho
Ongera sana mkuu ubarikiwe sana .ulayaHuu ushauri ni Mzuri sana ila hauendani na nyakati
Ingefaa utolewe karne ya 18 au 19 hivi
Huwa sielewi dhana ya kusema Idadi ya sisi, wa-Afrika ni tishio kwa Ulaya na Amerika
Kwanini?
Katika karne ya 21, bado Kuna Watu wanaamini wingi ni Hoja?
China ina Watu wangapi? Kwanini walibadili Sera yao ya kuzaliana?
Unahisi huko Ulaya na Amerika wanashindwa kuzaliana?
Ukiweza kujibu maswali hayo utaondoa dhana potofu iliyopo kwako
Ngoja tu nikuibie siri kidogo
Dunia ya sasa inategemea zaidi innovation and Technology,
Tupo katika Zama za Artificial Intelligence, AI na ulimwengu wa 5G bado kidogo tu tuufikie
Duniani huko Watu wanahangaika katika hayo maswala
Sasa anatokea mtu anasema eti Afrika tuna nguvu kazi. Huu ni upuuzi
Hio nguvu kazi mnayojivunia tayari ishaanza kubadiliwa na Roboti
Muangalie Elon Musk na Jeff Bozos, chukua jumla ya utajiri wao pamoja na potential growth ya makampuni yao katika miaka 10 tu ijayo
Unahisi Hawa Watu wawili watakuwa wamezidi GDP ya nchi ngapi za huku Afrika? Hao ni Watu wawili
Unless kama mnataka tuzaliane ili Hao watoto zetu waje kuwa wafanyakazi (watumwa) wa hao wazungu
Serikali ishauriwe juu ya Sera nzuri za kuinua Elimu yenye tija ya kutatua matatizo yetu pia inayoendana na kasi ya mabadiliko ya technology
Next time, Tujikite katika kujadili vitu vya maana sio huu ujinga ambapo kila mmoja ni shahidi kwamba kati ya familia yenye watoto 3 na 12 ni ipi yenye maisha mazuri
Wameanza kufanya tafiti za kupanda mboga huko anga za mbali
Mkuu mimi sibishi kwamba suala la Population yao ni tatizo. HAPANA
Nakataa hoja zinazodai African Population is a threat kwa Europe & America
Pia siungi mkono Hoja yako ya kusema tuongeze idadi yetu afu tukawe nguvu kazi huko kwa wazungu.
Sijui kama naeleweka vizuri, naomba usome mchango wangu hapo ju
Nakataa hoja zinazodai African Population is a threat kwa
Hamna tatizo kiongozi. Tuko pamoja maana lengo letu ni kuelimishana.Mkuu samahani kwa Lugha niliyotumia hapo awali, ila Lengo ni Moja tu...
... Kuonesha msisitizo juu ya ninachokiamini
Kuhusu hoja hii ni kwamba nianze kwa kukuuliza swali ila sitokusaidia kulijibu kama wewe ulivyofanya.Ila kushauri Afrika iongeze nguvu kazi ambao unashauri wakavune hela ulaya, Asia na America ni mtazamo mbaya sana
Kwani South Korea kwa level ya Uchumi waliofikia walienda kuchumia wapi? What about Singapore na hao China uliowayaja
Did they leave their country/continent to chase wealthy outside their boundaries?
Nope, they didn't!
Now we are talking. Ila tafadhali hoja ya kuhusu propaganda ya TRA sio vyema kuiweka hapa. Napenda sana kuongea kwa facts, otherwise kama utakuja na hoja yenye mashiko kuhusu jambo hilo. Ahsante.Tufanye vitu kwa hatua, tuwekeze katika elimu, tutatue matatizo yetu, tujenge Uchumi imara (achana na hizi propaganda za 2 Trillion za TRA)
Baada ya Hapo ndipo zije Sera za kuongeza idadi ya watu
Kidole kimoja hakifunji chawa. Ni elimu ya shule ya msingi hii. Uonevu wanaofanyiwa wageni katika nchi mbalimbali lazima serikali iwe na mkono wake ili kuzuia mambo kama hayo. Damu ni nzito kuliko maji. Huwezi mwambie kijana wako anayetafuta maisha ukitaka nikusaidia basi kaa hapa nyumbani fanya shughuli hapa ila ukienda mbali na nyumbani hilo ni juu yako.If we're aiming for individually development, America & Europe are good for us ila kama our aim is about Tanzania/Africa in general basi hio strategy yako si sahihi
Nimekukubali 100% upo sawa tena TECHNOLOGY ndio muhimu sasa duniani ukiwa na hiyo kila kitu unafanya na kuunda .India leo imekuwa best ktk IT duniani chuo chao toka 1950 walikufungua leo result yake wahindi wanaotka india ktk chuo hicho ni kipusa America wanatakiwa kila upande na kazi zinawasubiri.Huu ushauri ni Mzuri sana ila hauendani na nyakati
Ingefaa utolewe karne ya 18 au 19 hivi
Huwa sielewi dhana ya kusema Idadi ya sisi, wa-Afrika ni tishio kwa Ulaya na Amerika
Kwanini?
Katika karne ya 21, bado Kuna Watu wanaamini wingi ni Hoja?
China ina Watu wangapi? Kwanini walibadili Sera yao ya kuzaliana?
Unahisi huko Ulaya na Amerika wanashindwa kuzaliana?
Ukiweza kujibu maswali hayo utaondoa dhana potofu iliyopo kwako
Ngoja tu nikuibie siri kidogo
Dunia ya sasa inategemea zaidi innovation and Technology,
Tupo katika Zama za Artificial Intelligence, AI na ulimwengu wa 5G bado kidogo tu tuufikie
Duniani huko Watu wanahangaika katika hayo maswala
Sasa anatokea mtu anasema eti Afrika tuna nguvu kazi. Huu ni upuuzi
Hio nguvu kazi mnayojivunia tayari ishaanza kubadiliwa na Roboti
Muangalie Elon Musk na Jeff Bozos, chukua jumla ya utajiri wao pamoja na potential growth ya makampuni yao katika miaka 10 tu ijayo
Unahisi Hawa Watu wawili watakuwa wamezidi GDP ya nchi ngapi za huku Afrika? Hao ni Watu wawili
Unless kama mnataka tuzaliane ili Hao watoto zetu waje kuwa wafanyakazi (watumwa) wa hao wazungu
Serikali ishauriwe juu ya Sera nzuri za kuinua Elimu yenye tija ya kutatua matatizo yetu pia inayoendana na kasi ya mabadiliko ya technology
Next time, Tujikite katika kujadili vitu vya maana sio huu ujinga ambapo kila mmoja ni shahidi kwamba kati ya familia yenye watoto 3 na 12 ni ipi yenye maisha mazuri
Naelewa sana kuwa kuna mambo kama hayo yanayohusu teknolojia yanayoendelea katika nchi za wenzetu.Ongera sana mkuu ubarikiwe sana .ulaya
Wameanza kufanya tafiti za kupanda mboga huko anga za mbali sisi tuna waza kufyatua😂
Robot zina piga kazi kuliko mtu
Hata mimi hapa naunga mkono hoja. Elimu ni muhimu sana. Na tuiboreshe sambamba na sera zetu.Nimekukubali 100% upo sawa tena TECHNOLOGY ndio muhimu sasa duniani ukiwa na hiyo kila kitu unafanya na kuunda .India leo imekuwa best ktk IT duniani chuo chao toka 1950 walikufungua leo result yake wahindi wanaotka india ktk chuo hicho ni kipusa America wanatakiwa kila upande na kazi zinawasubiri.
Kama ungeweza kufafanua kidogo ndugu hoja yako. Hata hivyo kuwa Muafrika sio dhambi, jikubali na jivunie kile kilicho chako maana kama huwezi kupigana nae ungana nae. Kuwa na amani na furaha wakati wote ni jambo la msingi sana kwa afya yako na Taifa.ngoja wenyewe waje miafrika ndio tulivyo kushuka kwao kwa idadi ya watu hakuna kwa njia yoyote ile na uwezekano wa sisi kufaidika nako trust me
Sisemi vitu bila ya kuwa na reference ndugu yangu. Nasoma anagalau kwa kiasi chake ili niweze kusema vitu vya uhakika. Ingawa hii haikuwa kwenye mada ya leo ila nikujibu tu kidogo... soma The Guardian kwa link hii China to overtake US as world's biggest economy by 2028, report predictsHuo Uchumi unaoongelewa kwamba China itakuwa Super Power ni hadithi tu, unakuwaje superpower huku wananchi wakiwa masikini?
USA ni tofauti, angalia Uchumi wa mtu mmoja mmoja kisha linganisha na huko China
Je China Wanakadiriwa kuja kuwa na GDP ipi hio 2029? Kwa population ipi? 1.4 Billion People
Vipi kuhusu USA, unaweza kufanya uoinganishi hapo (achana na hisia za mtazamo wako wa siasa)
Wamebadilishana siti. Kutoka kwa wanaobeba vitabu kwapani mpaka kwenda wanaokaa nyuma ya computer. Kinachoangaliwa hapa sasa je ni nini impact yake katika uchumi... mapato ya serikali yataongezekana hivyo huduma za jamii kuendelea kuboreshwa ikiwemo elimu maana mianya ya kukwepa kodi itapungua. How do you see that?Miafrika bana, hivi mnajua teknolojia zinazidi kubuniwa ili kupunguza tegemezi kwa nguvu kazi za kibinadamu, kwamba mashini inaingizwa sehemu na kufanya kazi ya watu 1,000 kwa mpigo mmoja bila kukosea, sasa mnaagizana kuzaliana ili muwapeleke wapi watu wenu.
Kwa mfano hapo Tanzania kwenu LATRA wametangaza mfumo wa online kununua tiketi za mabasi ya kwenda mikoani, hamna tena tegemezi kwa wale maelfu ya waandika tiketi ambao hubeba vitabu kwapani, endeleeni kuzaliana na kufyatua watoto.....
Yeah wewe ndo umemfanya aibe ikiwa unataka kufikiria hivyo.... ila kama unataka tuelimishane niruhusu.Kujua jambo na kupanga jambo ni sawasawa???, mfano mimi nikijua kwamba mtu fulani ataiba na kweli akaiba je mimi ndiye nitakuwa nimepanga au nimemfanya aibe???
Wamebadilishana siti. Kutoka kwa wanaobeba vitabu kwapani mpaka kwenda wanaokaa nyuma ya computer. Kinachoangaliwa hapa sasa je ni nini impact yake katika uchumi... mapato ya serikali yataongezekana hivyo huduma za jamii kuendelea kuboreshwa ikiwemo elimu maana mianya ya kukwepa kodi itapungua. How do you see that?
Kila jambo na nyakati zake