Mokaze
JF-Expert Member
- Aug 3, 2018
- 14,370
- 14,929
Labda nikurahisishie kazi ndugu yangu. Ni hivi Mungu ndiye muweza wa yote, Mungu ndiye mpangaji wa yote, Mungu ndiye hujua kesho yetu, Mungu kila kitu... na hata shetani alishaongeaga na Mungu aende kumjaribu Ayubu na akaruhusiwa ingawa kwa masharti.
Sasa mimi nawewe tuna haja gani ya kuzozana. Hebu kwa mfano ukija kiimani hata serikali iliyo madarakani sass unadhani Mungu hakujua yenyewe ndo itakuwepo, je asingeweza kuzuia isiwepo, kwanini kaacha iwepo, ana makusudi yake na ndo hapo mimi naww hatupaswi kuhoji... Mipango ya Mungu hatuwezi kupingana nayo...
Na mimi ngoja nikurahishie kazi rafiki yangu.
Unasema:- Mungu ndiye muweza wa yote, Sio kweli kwamba Mungu ni muweza wa yote, kama Mungu ni muweza wa yote, je Mungu anaweza kusema uongo??, Mungu anaweza kuiba??, Mungu anaweza kuua watu hovyo???, Mungu anaweza kufa??, Mungu anaweza kuumba Mungu mwingine kama yeye???, Mungu anaweza kukugeuza wewe ukawa Yesu??nk,
Hivyo sasa utaona kwamba kuna baadhi ya vitu Mungu hawezi kufanya ili kulinda heshima na utukufu wake, hivyo sio kila kitu Mungu anaweza kufanya.
Unasema:- Mungu ndiye mpangaji wa yote, Sio kweli kwamba Mungu ndio mpangaji wa Yote, Mungu hawezi kupanga uhalifu na mambo yote ya kishetani, mfano kuzini, kuiba KURA, kula rushwa, kuua nk, hivyo sio kila kitu hupangwa na Mungu, Mungu hupanga mambo mema tu kwasababu yumwema.
Unasema:- Hujua kesho yetu, ndiyo hujua jana yetu, leo yetu na kesho yetu, na kujua kwake jana, leo na kesho yetu hakuhusiani na matendo yetu ya jana, leo na kesho yetu, matendo yetu husukumwa na nia na dhamira za nafsi zetu na ndio maana tunaamini ipo siku ya hukumu ambapo kila mtu ataulizwa juu ya matendo yake aliyofanya pindi alipokuwa duniani na hatimaye kulipwa malipo yanayompasa, kama kujua kwa Mungu kungalihusiana na matendo yetu basi wala kusingalikuwepo na malipo siku ya mwisho kwani kujua kwa Mungu na u husiano na matendo yetu ingalikuwa ni kikwazo cha watu kuadhibiwa au kulipwa malipo.mema, hiyo ndio falsafa ya malipo ya mema na maovu kwa mtu katika siku ya malipo.
Unasema Mungu aliongea na Shetani, Ndiyo, shetani mwenyewe ni Ibilisi au Lucifer, Shetani ni Generic name (jina la ujumla), lakini Mungu hajaumba Shetani kwani Mungu huwa haumbi vitu viovu na vibaya, Shetani ni kiumbe chochote kiovu na ushetani ni uovu na Mungu alimruhusu shetani awepo miongoni mwetu ili awe ni mtihani au ngazi yetu kwa ajili ya kupanda kuelekea juu kwenye wema, utajuaje kwamba jambo fulani ni jema kama hakuna ubaya wake???, utajuaje wizi ni mbaya kama hakuna wizi au hujaibiwa??, au utajuaje kupigwa ni kubaya kama hujapigwa??, Mungu alipaswa amuache shetani miongoni mwetu na ndiyo maana pia akawaleta mitume, manabii na malaika kupambana na shetani na watu tujifunze mema ya manabii na tuache mabaya ya shetani na hapo ndipo tutakapo panda madaraja ya kiroho duniani na akhera.