The internet is undefeated: A painful lesson

The internet is undefeated: A painful lesson

Mkuu Nyani Ngabu Rais Hana walinzi Bali Ana wasaidizi wake 🙏🙏🙏🙏
Oh yeah....leakers wamo humo humo serikalini.

Hizi ni zama tofauti sana.

Kuficha ficha mambo ambayo yanajumuisha watu wengi ni vigumu sana.

Taarifa zitapenya tu.

Si ajabu ukakuta waliokuwa wanavujisha hizo taarifa ni hao walinzi wa rais....
 
Mnapotetea maisha ya mitandaoni kuwa ndio maisha halisi mnaleta hoja mufu. Serikali ya mitandaoni haina kiongozi, kila mshiriki ni kambare.

Serikali halisi iliyoko madarakani ni ya CCM ambayo ina Ilani yake inayotekelezwa. Kwa msingi huo hakuna mabadiliko chini ya Mama Samia tofauti na jinsi ilivyoongozwa na Marehemu Magufuli. Isitoshe Mama Samia amefanya kazi naye, akafahamu jinsi ya utendaji wake.

Naangalia hapa, kwenye TV, jinsi wananchi wanaojua kuna Serikali walivyoumizwa na huu msiba. Naamini siku ya kuagwa mwili wake itakuwa siku ya majonzi makubwa.

Hivyo basi Nyani Ngabu endelea kuishi katika Serikali yako ya mitandaoni. I also hope this is a teachable moment to you and the like who live in an hypothetical government
 
Majaliwa atuombe msamaha watanzania la sivyo hatufai Kama kiongozi kwa nafasi yeyote Ile

Alikuwa anaudanganya umma kuhusu Hali ya AFYA ya Rais kwa maslahi ya Nani?

Tunataka kujua la sivyo tutamuhisi vibaya.......
 
Mkuu nyani ngabu upo sawa kabisa, achia mbali miezi michache baadaye, hata hivi sasa kambi ya mtandaoni inaposema kwamba huko ndani Kuna mvutano wa nani awe makamu wa Rais, kwamba wapo wanamtaka bashiru etc watu tunaawaamini kwani Kama mwanzo walikuwa sawa why not now
 
Ni wengi sio peke yako ndugu
Ila naamini kweli Mungu yupo na anasikia maombi yetu,hii dunia tunapita tu hakuna atakae ishi milele,pumzi na uhai si mali yetu,tusiishi kama vile sisi ni miungu watu,Hope hili somo limesomeka kwa wengi
"Msidanganyike; Mungu hafanyiwi dhihaka. Alichopanda mtu ndicho atakachovuna"(Wagalatia 6:7)

Kayafa alipanda kifo kwa kukataa kupambana na Corona na kwa kunyanyasa watu.
 
Ni kweli.

Na yeye mgao wake mkubwa tu wa lawama.
kumbe ulishamsoma akipewa mic yeye ni kuwalaumu wasaidizi wake tu.. Pale polisi alimlaumu Simbachawene kuhusu mafao ya wastaafu wa polisi kumbe wizara ilishafanya kila kitu ila hazina (Kwa dotto) ndio wamekalia malipo
 
Mimi sijawahi iamini serikali toka JPM amekuwa raisi. Serikali ya watu waoga JPM aliitengeneza. JK aliugua tezi dume na taifa tulijulishwa na tukamuombea raisi.
 
Mimi sijawahi iamini serikali toka JPM amekuwa raisi. Serikali ya watu waoga JPM aliitengeneza. JK aliugua tezi dume na taifa tulijulishwa na tukamuombea raisi.
Niliwahi kusema kuwa Rais Magufuli hakuwa kiongozi mzuri.

Ila, alikuwa ni msimamizi mzuri wa miradi ya ujenzi.

Mpe mradi wa ujenzi ausimamie. Utampenda!

Kwenye uongozi [leadership] alipwaya sana.
 
Tabia ya ufichaji taarifa ilikubuhu zama hizi yani watu walishindwa kutoa taarifa kuwa anaumwa guess what mtu alikua anajihoji je akipona atakua katika hali gani! So uhuru wa vyombo vya habari haukuwepo na ndio tumevuna matunda yake kwa awamu hii!
 
Hii imefanya kigogo kujiongezea a lot of followers!It really has to change!
Matumaini yetu mama hatatuangusha
 
Ni kweli wenzetu wametuzidi ujuzi. Kwa asilimia kubwa ni kupona. Anyways, mponyaji ni Mungu, na haya yote yaliyotokea ni mipango yake
 
Waachiwe huru wote waliokamatwa kwa kusema kwamba magufuli anaumwa maana walikuwa sahihi.
 
If your going to believe the media on your life then be prepared to live as hell, having one correct news doesnt wash it from all other dirty publications we know
 
Back
Top Bottom