Mazindu Msambule
JF-Expert Member
- Feb 22, 2012
- 7,510
- 6,877
Halafu eti watu wanataka kusema eti ooh Nyerere sijui alikua na chuki na Waislamu sijui mara nini, nimemfahamu vizuri prefesa Malima akiwa mipango pale; nijuavyo huyu bwana kila sehemu aliko pita aliharibu (hi ya kua mwalimu UD nilikua siijui, nafahamu tu kwamba amewahi kua principal IFM). Hata alipoachana na uwaziri (nafikiri alijiuzuru baada ya kelele kua nyingi) akaanzisha chama chake cha NRA/NAREA; alikua akitoa kanda/tapes Enzi hizo, hakua anaongea kama mchumi kabisa, maada zake nyingi kwenye hicho chama ilikua ni mambo ya dini tu, eti ooh nilichukiwa kwasababu ni mwislam. Rais wa nchi by that time alikua rafikiye kipenzi na wa mkoa mmoja nae yaani Ali HAssani Mwinyi.Hata kwenye Taaluma Malima hakufanya vizuri; inawezekana aliingizwa kwenye taaluma ya kufundisha bila kupenda kwa vile ndiyo iliyokuwa njia pekee kwake wakati huo. Malima alianza kazi chuo Kikuu cha Dar akiwa professor kamili kutokana na kuwa alihamishwa kutoka kuwa katibu mkuu wa Wizara ya mipango chini ya Waziri Abdulrahman Babu baada ya kushindwa kazi. Uprofesa alipewa kutokana na mshahara alioingia nao UDSM wa Katibu Mkuu wa Wizara akiwa anabebwa na Nyerere. Ilimchukua miaka mingi sana kutoa Professorial Inaugural Lecture kabla hajakaamka na pumba za "Political Economy of devaluation in Developing Countries" alizotoa akiwa Waziri katika serikali ya Mwinyi. Mwulizeni mwenzie Profesa Shivji kuhusu pumba alizotema jamaa huyo wakati huo.
Kama Yeriko ambaye nimechangia uzi wake hapo juu na hata mzee Mohamed Said naye nitakua nachukua muda kuzitafakari hoja zake, wengi humu wamekua wanaandika habari za siku za nyuma kwasabau wengi hatukwepo and then tunajikuta tunaamini tu, kumbe uongo mkubwa.