The last days of Prof. Kighoma Ali Malima, July/August 1995

Halafu eti watu wanataka kusema eti ooh Nyerere sijui alikua na chuki na Waislamu sijui mara nini, nimemfahamu vizuri prefesa Malima akiwa mipango pale; nijuavyo huyu bwana kila sehemu aliko pita aliharibu (hi ya kua mwalimu UD nilikua siijui, nafahamu tu kwamba amewahi kua principal IFM). Hata alipoachana na uwaziri (nafikiri alijiuzuru baada ya kelele kua nyingi) akaanzisha chama chake cha NRA/NAREA; alikua akitoa kanda/tapes Enzi hizo, hakua anaongea kama mchumi kabisa, maada zake nyingi kwenye hicho chama ilikua ni mambo ya dini tu, eti ooh nilichukiwa kwasababu ni mwislam. Rais wa nchi by that time alikua rafikiye kipenzi na wa mkoa mmoja nae yaani Ali HAssani Mwinyi.
Kama Yeriko ambaye nimechangia uzi wake hapo juu na hata mzee Mohamed Said naye nitakua nachukua muda kuzitafakari hoja zake, wengi humu wamekua wanaandika habari za siku za nyuma kwasabau wengi hatukwepo and then tunajikuta tunaamini tu, kumbe uongo mkubwa.
 
Malima hakuwahi kuwa principal wa IFM; zamani hizo IFM ilikuwa inamilikiwa na NBC. Malima alihamishwa kutoka Wizara ya Mipango na kupelekwa UDSM baada ya kukataliwa na Abdulrahamani Babu ambaye alikuwa waziri wa Uchumi na Mipango nadhani ama mwaka 1970 au 1971 kabla Babu hajakumbwa na ile kashfa ya kifo cha Karume mwaka 1972. Katika baraza jipya la mwaka 1972 baada ya kifo cha Karume, bado Malima hakurudishwa serikalini hata baada ya Babu kuwa ametolewa. Malima alikaa UDSM kwa karibu miaka 10 hadi mwanzoni mwa 1980 baada ya vita ndipo aliporudishwa tena serikalini na Nyerere na kupewa Wizara hiyo hiyo ya Uchumi na Mipango. Nyerere alikuwa akimbeba sana kwa vile alikuwa msomi, unajua Nyerere alikuwa "mwalimu" kwa hiyo alikuwa na upendo wa tofauti sana kwa wasomi wanaokubaliana naye. malima alikuwa anakubaliana na Nyerere kwa kila kitu hadi pale Nyerere alipotoka madarakani.
 
Thanks brother kwa ufafanuzi zaidi; jukwaa hili kwasasa linatakiwa watu wazima kuigia na kupitia pitia ili kuweka mambo sawa, tukiwaacha hawa kina mzee Mohamend Said kueleza mambo ya zamani wanadanganya sana tu; unakuta mtu anaijua vizuri historia ya Profesa Kighoma Ali Malima lakini huyo huyo haijui historia ya Harace Kolimba!? Kolimba kafa mwanzo mwa Mkapa na Malima kafa mwishoni mwa utawala wa Mwinyi, sasa mtu huyu kama sio mdini ni kitu gani? How comes uijue historia ya mtu wa nyuma halafu huyu wa juzi kati usiijue!? Naanza kuhisi wengi humu hua wanachangia mambo yanayo hutubiwa kwenye nyumba za IBADA. Kuna siku nilikua Riverside pale kwa ndugu yangu mmoja hivi ambaye kwa maana ya dini huyu ndugu yangu ni Muislamu (ni ndugu yangu hasa, sio kidogo; akaja mtu mwingine ambaye kupitia yale mazungumzo alisema kwanza alikua Mkristo na sasa yeye ni Muislamu (hilo halikunisumbua cause watu wanabadiri DINI kila siku) kilicho nishangaza kwa yule mtu ni hiki; kwamba eti mji wa ROMA mwanzoni ulikua ni mji wa Kiislamu na Wakristo waliuteka NYARA tu, nilishangaa sana. Mtu kama huyu akipewa kipaaza sauti ahubiri msikitini atayasema hayo na watu watatoka na kuja humu jamvini na kuyaandika and then wenye akili kidogo wataamini na baada ya hapo kitakacho fuata ni chuki dhidi ya Wakristo na waislam cause itatafsirika kua Wakristo hunyang'anya mali za waislamu, Mungu atusaidie tu.
 
Mzee Mohammed Said, umepotelea wapi
 
tuambie nani kaleta maana tusidanganywe pasi sababu
 
Mzee Mohammed Said, umepotelea wapi
 
Swali la msingi
Hizi historia kila siku ni Nyerere tu na uislamu ,sawa alifanya makosa ,ila Mwinyi alipochukua kiti kama Rais alifanya nini kuondoa Makosa ya Nyerere na uislamu ??
 
👆👆Hii picha ya tarehe 22 Oktoba 1987 katika mkutano mkuu wa CCM uliofanyika KIZOTA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…