The Lema Verdict: Did the Court of Appeal encroach on litigation rights of a voter?

[/QUOTE]

George Jinasa Bila ya kutathiminiwa kideo chenye hotuba za lema huwezi kuwatia doa wapinga marejeo. Wao walithibitisha malalamiko yao kwa kuleta kideo sasa kama kideo hakikutathiminiwa mahakama kuu ilibidi mahakama ya rufaa ikitathimini na kwa vile hakikutathiminiwa mahakama ya rufaa ilijitungia uamzui wake kutoka kibindoni kwake.......................yaani inashangaza kweli sijui hawa majaji huwa wanawaokota wapi?
 
Last edited by a moderator:

Mghaka ni vyema ungeliisoma hukumu yenyewe. Mahakama ya Rufaa haikutofautisha hizi nyanja za kukashifiwa na unair election................................ingawaje kesi hii iligusa yote hayo......................hakuna fair election kama lugha chafu zinatumika.....................period.
 
Last edited by a moderator:
Kaka Rutashubanyuma, mimi naona si haki kwa mtu ambaye haki yake haijaathiriwa na kampeni za uchaguzi kwenda kupinga matokeo mahakamani kwani hii inawanyima haki wapiga kura wengi ambao walikuwa na haki ya kumchagua waliyekuwa wanamtaka.

Ozzie Utajuaje kuwa haki zake hazijaathirika wakati hata ushahidi aliokuletea hutaki kuupima? Kama jamii nzima ilitukanwa mahakama bado ingelisema haki za wapigakura hazijaathirika? Mbaya zaidi wao walikwisha kuwafuta kwenye oroddha ya wapigakura wapinga rufani bila hata ya kuwapatia nafasi ya kuzijibu khoja ambazo mahakama ya rufaa ilizitumia kwenye kufikia maamuzi haya. Haki ya asili ya wapinga rufani ilikiukwa na huu uamuzi maana walikuja kufahamu ya kuwa Mahakama ya Rufaa haiwatambuwi kama wapiga kura wakati walipoupata uamuzi. Ni nini kiliizuia mahakama ya rufaa kuwauliza juu ya hizo khoja ukuzingatia sheria ya uchaguzi iko wazi ushahidi ni kwenye maeneo ambayo yanabishaniwa na hilo halikuwa mojawapo?
 
Last edited by a moderator:

gfsonwin usiseme hata kama hatukanwi yeye.....sisi hatujui Lema alisema nini na hata kama alimtukana batilda yawezekana kabisa tafsiri ya hiyo lugha ikawa kutukana jamii...........kwa mfano mtu akiukashifu uchi wa mwanamke.........na washitaki ni wanaumme isije ikasemekana eti mbona wao siyo wanawake..........wakati tuna watoto wa kike, mama zetu na dada zetu wametukanwa?
 
Last edited by a moderator:

MTK Do not say it now a done deal...................this ruling has wide implications beyond the lema fate as an MP............................................my focus has nothing to do with Lema as a person but what bearing this ruling has in the future conduct of electoral litigation................that is all

Am pleased that you have tersely noted my input could have a positive intervention to the case............the problem was how would I have known that the courts are such lousy ones............it was only after the ruling I became aware of this sad fact...........

marekani nimeitolea mfano kwa sababu sheria yao ya ychaguzi kwenye hili eneo inafannanana ya kwetu sasa niwashangaa hawa majaji kwa kutoa tafsiri inayotofautiana na hawa ambao sisi sheria zetu tumewaiga.......................inapokuja kuchakachua sheria tunadai sisi siyo fotokopi......inapokuja kuzinakili na kuziasisha hapo hatuziiti fotokopi................................what a double standard
 

hivyo mtu baki anaweza kushtaki sio?? sasa kwann majaji waseme aliyepaswa kushtak sio jamii ni mtu husika? ama sikuelewa vzr?
 
sina maana hiyo nisamehe na nakuomba unisaidie kujibu swali langu hili.

gfsonwin well nimekujibu lile la ziada maana la awali umesema umeridhika na jibu ulilopewa.......
 
Last edited by a moderator:
hivyo mtu baki anaweza kushtaki sio?? sasa kwann majaji waseme aliyepaswa kushtak sio jamii ni mtu husika? ama sikuelewa vzr?

gfsonwin wao wametoa tafsiri ambayo inakinzana na katiba na sheria ya uchagzui na ndiyo maana tunahoji hivi ni shule zipi wenzetu walisoma maana wanaonekana ni wababaishaji tu?
 
Last edited by a moderator:
gfsonwin wao wametoa tafsiri ambayo inakinzana na katiba na sheria ya uchagzui na ndiyo maana tunahoji hivi ni shule zipi wenzetu walisoma maana wanaonekana ni wababaishaji tu?

najijua mie ni kishoka/kilaza wa sheria ila ni mtu ambaye napenda sana kuuliza kwa wanaojua hata kama nauliza kwao litakuwa ni jambo dogo sana.

sasa basi kwa mantiki hiyo tafsiri ambayo imetumika ni tofauti na sheria za uchaguzi je ni sahihi kusema kwamba hukumu ni ya haki??

na je kwann wenye akili dogo kama zangu tusiseme tu kwamba iliamriwa iwe hivyo ili waridhishwe ila ukweli utabaki kuwa ukweli?? nasema hivyo manake sijui na narudia tena SIJUI vifungu vya sheria kiundani ila tu najitahd kuelewa concepts zinazotolewa na wanaojua.
 
ruttashubanyuma with due diligence i dare to say something is not known to us. the good people to say it are the judges who ruled the case as why such double standards?? and what will be the fate for future electoral litigation
 
Last edited by a moderator:
ruttashubanyuma with due diligence i dare to say something is not known to us. the good people to say it are the judges who ruled the case as why such double standards?? and what will be the fate for future electoral litigation

gfsonwin labda katiba hii ifafanue zaidi lakini majaji wakorofi watajitahidi kuja na tafsiri zao.......................lakini kwa wapigakura ambao hawaridhiki na mwenendo wa matokeo ya uchaguzi bado ni haki yao kwenda mbele na kusikia majaji wanasemaje pamoja na hii hukumu sasa kuwa kikwazo katika ufunguaji wa masuala ya namna hii.....................labda waleta marejeo warudi tena Mahakama ya Rufaa a kuomba marejeo kwa kutumia khoja kama hizi au na nyinginezo walizonazo....................tatizo la masuala ya namna hii yanahitaji fedha na nasikia hawana hela ya kuendelea kudai haki yao...............haki hapa kwetu ni ya mwenye vijisenti......................lol
 
Last edited by a moderator:

gfsonwin katiba Ibara ya 26 (2) na sheria ya uchaguzi kifungu cha 111 (1) (a) vimeweka wazi kuwa mpigakura anayo haki ya kuhoji uhalalai wa matokeo ya kura aliyoshiriki majaji hawa sasa wameandika sheria yao mpya na kufuta ile ya zamani kwa kudai wao wameitafisiri vizuri..................inachanganya kwa wengi hilo...
 
Last edited by a moderator:
kumbe basi tuko wengi ambao tumebaki na maswali ya kutoelewa na nikaishia kusema mie kishoka wa sheria sijui lolote.
kwani Rutashubanyuma kuna tafsiri tofauti za sheria?? hadi huyu asema tumeitafsiri vzr zaid??
 
Last edited by a moderator:
kumbe basi tuko wengi ambao tumebaki na maswali ya kutoelewa na nikaishia kusema mie kishoka wa sheria sijui lolote.
kwani Rutashubanyuma kuna tafsiri tofauti za sheria?? hadi huyu asema tumeitafsiri vzr zaid??

gfsonwin tafsiri za sheria kama zilivyo za mambo mengineyo huwa nyingi kulingana na mtu mwenyewe anavyoona........na huyo anayesema wametafsiri vizuri ni kuwa kauufarahia uamuzi leo ingawaje kesho utakapokuja kuwa shubiri kwake atasema walikosea.............siyo kuwa hatuelewi tunaelewa walichokifanya ila sikubaliani nao......naona ni wavivu wa kuyachambua mambo wametafuta njia ya mkato kuimaliza kesi......na ndiyo maana hata hukumu yao ni kurasa moja tu........wavivu wakusoma na kuandika..........
 
Last edited by a moderator:
Rutashubanyuma, Nimesoma maoni yako but what I say is this:

Mahakama ya Rufaa haikujadili hoja yoyote ya rufaa on merit. Ilijadili preliminary objection-The petitioners have go no LOCUS STANDI. Warufaa walibase rufani yao kwenye Mgonja case ambayo kimsingi ilitumia kifungu cha 26(2) kuwa hata kama their rights have not been infringed, they have the right to bring the action against Lema. Lakini ukisoma kifungu hicho kwa makini, between lines, utaona kuwa kina-impose conditionalities:

26(2) Kila mtu ana haki, kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria, kuchukua hatua za kisheria kuhakikisha hifadhi ya Katiba na sheria za nchi.

Kwenye red hapo, pamoja na kuwa na haki ya kufungua shauri, lakini lazima utimize masharti ya sheria zingine. Mojawapo ya sheria hizo ni common Law on the doctrine of LOCUS STANDI. Majaji walikuwa sahihi kabisa. Sheria zetu zinatokana na Common Law almost by over 99%!. To my knowledge, doctrine of LOCUS STANDI has never undergone any change. Unless you deny the doctrine of JURISDICTION, then ........

Katika taratibu za mahakama, lazima uwe na LOCUS STAND kabla ya kusikiliza hoja zako. Lazima uwe na uhalali wa kufungua kesi. Kama huna uhalali wa kufungua kesi, mahakama haiwezi kusikiliza hoja zako. Ndicho kilichotokea kwa rufaa ya Lema. Warufani hawakuwa na uhalali wa kufungua kesi, hivyo hoja za rufani haziwezi kusikilizwa maana High court haikusikiliza hoja ya Preliminary objection rightly!

Mahakama ilibidi ijiridhishe kwanza kama warufani wana uhalali wa kufungua kesi. Ni issue ya jurisdiction, mfano mahakama ya wilaya/hakimu mkazi/ya mwanzo haziwezi kusikiliza kesi ya mauaji. Ukifungua kesi ya mauaji district court, haiwezi kusikilizwa kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za namna hiyo- huu ni mfano kati ya mingi ambao unaeleweka kirahisi, ndio maana ya jurisdiction!
 
Last edited by a moderator:
@Rutashubanyuma,

Swala la ushahidi wa video ni swala ambalo lilipaswa kuwa determined na High Court. Ikiwa ushahidi huo ulipelekwa mahakamani na ukawa admitted kisha jaji akapuuza kuuzingatia, hilo ni kosa la jaji wa mahakama kuu.
Swala linapokwenda court of appeal si kazi ya court of appeal kusikiliza kesi (trying the case) bali kuamua rufaa. Ikiwa kuna upande wowote uliona kuna tatizo kwenye admission ya huo ushahidi, ulipaswa kuiomba court of appeal iagize kesi kusikilizwa upya na jaji mwigine (retrial). Hii inatokea kukiwa na irregularities zilizopelekea kupoteza haki ya mtu! Sasa kama huo ushahidi haukupelekwa High Court tusetegemee court of appeal waanza kuchunguza kitua ambacho hakikuwepo in the first place.Pili, kuna mambo mengine katika kesi yakiamuliwa yanaathiri mwenendo mzima wa shauri na hiyo mahakama haina haja ya kuendelea na hoja zingine. Kwa mfano kama case imepita mda wake wa kusikilizwa (time barred) au mahakama haina mamlaka ya kuisikiliza (jurisdiction), itaitupilia mbali kesi hiyo wala haitaangalia maswala ya msingi ya kesi hiyo (the substance of the case). Sasa katika swala la Lema, kujua kwamba wajibu rufaa walikuwa na haki ya kufungua kesi hiyo ni swala la msingi. Mahakama imeona hawakuwa na haki ya kufungua kesi hiyo (ama hawakuwa na locus stand). Sasa kama hawakuwa na locus stand hakuna haja ya kuendelea na hoja nyingine however good they might be!
 
Reactions: EMT

ivi wajua kwann naipenda zaid sayansi ni kwasababu huwa iko straightforwad. leo hii ukitaja newton's laws of motion ni zile zile ingawa zina mulitple applications ila sheria siipend kwasababu kila siku ina definition tofauti and it gives me some problems when writing my contracts, like there are no common definition of some contractual terms. every term shld be defined according to the meant purpose.
 
mwanagu Ronn M merry x-mass.

haya nieleweshe hapa hivi wataka kuniambia kwamba wajbu rufaa ndio mahakama kuu ama mahakama ya rufaa??
na je wataka kuniambia kwamba rufaa imepita sawa majaji wa mahakama kuu hawawez kupinga hukumu hii ya rufaa??
 
Last edited by a moderator:
Ronn M Huwezi kufikia mahitimisho haya wakati ushahidi wa kideo si mahakama kuu au Mahakama ya Rufaa ambayo ilichunguza hilo............................you are only being prejudicial in making such vacuous assertions.......

Sasa ndugu mahakama si inaamua basing on the evidence presented? Remember we are using adversarial system. Court has no duty to make inquiry kama ilivyo kwenye inquisitorial system. Sasa kama ushahidi huo haukuletwa then hauwezi kuchunguzwa! You ve to make your case strong in court sir, usitegemee mahakama ifanye on your behalf. Copy ya High court judgement nimeiacha Dar, so sikumbuki sana kama ushahidi wa CD uliletwa mahakamani, ila kama haukuletwa si High Court wala Court of Appeal ilipaswa kuuchunguza.
 
mwanagu Ronn M merry x-mass.

haya nieleweshe hapa hivi wataka kuniambia kwamba wajbu rufaa ndio mahakama kuu ama mahakama ya rufaa??
na je wataka kuniambia kwamba rufaa imepita sawa majaji wa mahakama kuu hawawez kupinga hukumu hii ya rufaa??


Merry Christmas sweetheart, love u ma!

Wajibu rufaa ni wale ambao walikuwa wanamshtaki Lema katika mahakama kuu. Pale huitwa Plaintiffs na anayeshtakiwa anaitwa Defendant. Sasa inapokwenda kwenye ngazi ya rufaa, yule anayekat rufani anaitwa appellant (mrufani) ambaye ni Lema na wanolalamikiwa katika rufani hiyo wanaitwa wajibu rufani yaani respondents ambao ndio wale wa CCM.

Kuhusu majaji wa mahakama kuu kupinga hilo haliwezekani mama yangu gfsonwin. Mahakama ya rufaa ipo juu ya mahakama kuu na uamuzi wa mahakama ya rufaa ndio huchukuliwa kuwa ni uamuzi halali wa mahakama. Mahakama zote za chini zinapaswa kufuata jinsi mahakama ilivyoamua mpaka hapo itakapoamua vinginevyo au bunge litakapotunga sheria mpya
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…