The Manchester City (The Citizens) | Special Thread

Klopp mzee wa kufa na tai shingoni.
Kwa namna uchezaji wa trent ulivyo unaonesha directly ana uwezo wa kucheza hiyo role ila klopp yeye anasimamia anachokiamini..saivi naona kaamua kuadapt kulingana na uozo wa middle ya liva.
 
Alikua anaijua vizuri tu potential ya anold kwenye midfield ila ndio hivyo tu huyo mzee ni mgumu kuadmitt mbinu zake zinapofeli.
 
Man city imeandaa mpango wa kupanua uwanja wa etihad na kuongeza uwezo wake wa kuchukua watu kutoka watu 54,500 kwa sasa mpaka watu 60,000.
Mpango huo ambao utagharimu £ 300 million utahusisha pia ujenzi wa sehemu mbalimbali ambazo zitaungana na uwanja kwa ajili ya shughuli za kiburudani, maduka, hoteli, makumbusho pamoja na Fan zone (sehemu ya mashabiki waliokosa nafasi ya kuingia uwanjani) yenye kuchukua watu 3000 ambayo itakuwa imefunikwa ambayo kutakuwa na huduma ya vyakula na vinywaji. Pia kutakua na baa ya juu ya uwanja "sky bar" ambayo watu watakua na uwezo wa kuona kinachoendelea uwanjani "aerial view".

Kwa sasa mpango huo unasubiri kuidhinishwa na baraza la klabu ya Manchester city na phase ya kwanza inategemea kuanza mwezi september mwaka huu na kukamilika mwezi August mwaka 2025 huku maboresho kamili yakitarajiwa kukamilika mwaka 2026.

Etihad inakwenda kuwa moja kati ya viwanja vya kisasa zaidi duniani.
 
BACK IN TRAINING:

Foden amefanya mazoezi na timu leo asubuhi kuelekea maandalizi ya mchezo dhidi ya bayern.

Bado haijajulikana kama atasafiri na timu kwenda ujerumani ama la.
 
Clement Turpin from France has been appointed a referee for BAYERN MUNICH vs MAN CITY
 
Hiii ndio itakuwa view ya uwanja ...
 
Nice
 
Pep on foden's return.

"Definately it's good news for us.
He has trained once but we decided he would come with us and be on the bench"
 
Nawaangalia hapa Napoli ,....


inanikumbusha tu kipind tunastruggle kumfunga Liverpool UEFA ,wakati kwenye league tulikuwa tunajipigia ....


Uzoefu unambeba ac Milan UEFA ...
Huyu napoli kuna watu walikua wanampa kombe!! timu ndio robo fainali yake ya kwanza ya UEFA watu wanaipa kombe kwenye makaratasi.
 
Yaani tunamtaka Madrid msimu huu akione kilicho mnyima kanga manyoya ya shingo.
 
Madrid akikutana na timu yenye firepower pale mbele, atarudishwa la liga mapema sana.
Chelsea hii game wangekuwa clinical & aggressive, madrid angekua na hali ngumu sana.
 
Madrid akikutana na timu yenye firepower pale mbele, atarudishwa la liga mapema sana.
Chelsea hii game wangekuwa clinical & aggressive, madrid angekua na hali ngumu sana.
Madrid wameonesha wanatoboka vizuri tu ila chelsea ndio wamekuwa wavivu kutumia nafasi.

Huyu tunaenda kumuua vizuri sana kwa mpira huo.
 
Sioni Madrid kama anatisha ...

Labda mambo mengine ya kimpira yatokee ...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…