The Manchester City (The Citizens) | Special Thread

The Manchester City (The Citizens) | Special Thread

Ubingwa ulikuwa wewe ukipoteza game mm nakuwa bingwa. wewe umepoteza leo na mm nimekuwa bingwa. Ila ni bora kwa njia hii kuliko ile ya mwanzo.Halafu kumbe wewe ni Man U, ndo maana unakataa ubingwa wa liver kwenye ucl.
Na ndio maana ni Real Madrid. Alihama na Ronaldo
 
Champs
IMG-20180415-WA0011.jpg
 
JOSE Mourinho ameipongeza Manchester City kwa kubeba ubingwa wa Ligi Kuu England na kukiri kikosi hicho cha Pep Guardiola kilikuwa bora zaidi kwa muda wote msimu huu.

Wakati wachambuzi wakimtolea macho Mourinho na Man United yake imeshindwa kupambana na Man City kwenye mbio za ubingwa wa msimu huu, kocha huyo Mreno alisema kazi hiyo haikuwa ya kwanza tu, bali klabu zote kubwa kwenye ile Top Six zilipaswa kupambana, kuanzia Arsenal, Liverpool, Chelsea na Tottenham.

Lakini, ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu, unaambiwa hivi ni ngumu ya pesa. Mourinho na Guardiola walimwaga pesa za kutosha, lakini aliyechana pochi lake kwa kiasi kikubwa zaidi, ndiye aliyeibuka kidedea. Katika msimu wa 2016/17, Man United ilitumia Pauni 99.22 milioni, wakati Man City ilitumia Pauni 145.15 milioni. Msimu huu, Man United imetumia Pauni 138.3 milioni na Man City, Pauni 142.05 milioni.

Hata katika matumizi ya jumla kabla ya kufanya makato yoyote, Man City imetumia Pauni 365.85 milioni na Man United Pauni 291.3 milioni. Soka la kisasa, kutamba unahitaji kumwaga pesa za kutosha na ndiyo maana kwa timu hizo ndizo zenyewe zilizoonekana kupeana upinzani kwenye ligi, licha ya Man United ilizembea katika baadhi ya mechi zake. Katika msimu wake wa kwanza Mourinho, alitumia Pauni 145.3 milionbi, akiwanasa Eric Bailly (Pauni 30 milioni), Henrikh Mkhitaryan (Pauni 26.3 milioni) na Paul Pogba (Pauni 89 milioni).

Kwa msimu huo, pesa alizoingiza kwa kuuza wachezaji ni Pauni 46.08 milioni. Msimu huu, Mourinho alitumia Pauni 138.3 milioni, akiwanasa Victor Lindelof (Pauni 31 milioni), Romale Lukaku (Pauni 75 milioni) na Nemanja Matic (Pauni 40 milioni). Wachezaji waliouzwa waliingiza Man United, Pauni 7.7 milioni.

Man City, Guardiola alitumia Pauni 167.15 milioni, akibeba orodha ndefu ya wachezaji Ilkay Gundogan (Pauni 20 milioni), Nolito (Pauni 13.8 milioni), Oleksandr Zinchenko (Pauni 1.7 milioni), Leroy Sane (Pauni 37 milioni), Marlos Moreno (Pauni 4.75 milioni), John Stones (Pauni 47.5 milioni), Claudio Bravo (Pauni 15.4 milioni), Gabriel Jesus (Pauni 27 milioni). Pesa alizoingiza kwa kuuza wachezaji ni Pauni 22 milioni. Kwa msimu huu, Man City imetumia Pauni 198.7 milioni, kunasa wachezaji, Bernardo Silva (Pauni 43 milioni), Ederson (Pauni 34.9 milioni).

Kyle Walker (Pauni 45 milioni), Danilo (Pauni 26.5 milioni) na Benjamin Mendy (Pauni 49.3 milioni).

Kiwango alichoingiza kwa kuuza wachezaji ni Pauni 56.65 milioni. Katika tofauti hiyo ya matumizi ya pesa, inaonyesha wazi namna Guardiola alivyowashinda wenzake katika mbio za kulitaka taji hilo la Ligi Kuu England.

Gharama hizo hazikuhusu usajili wa Januari, ambapo Guardiola alimnasa Aymeric aporte kwa Pauni 57 milioni, wakati Mourinho alimnasa Alexis Sanchez kwa kubadilishana na Mkhitaryan.
 
Pep Guardiola anatarajiwa kutia saini mkataba mpya na klabu ya Manchester City.

Guardiola anatarajiwa kupata bonasi ya Pauni10 milioni baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England.

Kocha huyo mwenye miaka 47, anatarajiwa kubaki Man City hadi mwaka 2020 baada ya kupata mafanikio katika msimu wake wa pili.

Guardiola amewavutia wamiliki wa klabu hiyo kutoka Abu Dhabi, baada ya kuipa Man City ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu ikiwa na mechi mkononi.

Kocha huyo anatarajiwa kuvuna Pauni15 milioni kwa mwaka atakapotia saini mkataba huo.

Mbali na Guardiola, Man City inatarajiwa kuwabakiza baadhi ya nyota wake waliotamba msimu huu akiwemo kiungo mshambuliaji Kevin De Bruyne
 
Kiwango cha hali ya juu kabida leo kimeonekana yani mpira mwingiiiii
20180422_234515.jpg
20180422_234553.jpg
20180422_234641.jpg
 
Back
Top Bottom