The Manchester City (The Citizens) | Special Thread

Manchester City wameanza mazungumzo upya ya kujaribu kumnasa winga wa Leicester City, Riyad Mahrez ambaye huenda akaondoka ndani ya klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.

Pia Manchester United wako tayari kumwachia Anthony Martial kwenda Borussia Dortmund kama chambo ya kumnasa Christian Pulisic.

Hata hivyo winga huyo anayetajwa kuwa na thamani ya £40m anatolewa macho pia na vigogo wengine kama Liverpool, Chelsea na Arsenal.
 
Yaya Toure anaweza kujiunga na timu nyingine ya Premier League mwisho wa msimu endapo atafungashiwa virago vyake Manchester City, Everton, Burnley na waliopanda daraja Wolves wamekuwa wakivutiwa na kiungo huyo mwenye miaka 34.

City imenyakua ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu ikijikatia mapema tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Upande mwingine Uongozi wa Everton imefichua kuwa, bosi wa FC Porto, Sergio Conceicao (43) anaweza akachukua mikoba ya Sam Allardyce, kama Meneja huyo ataondoka Goodison Park.
 
Will be missing him (Toure Yaya)
 
Klabu ya Manchester City imemuaga kwa heshima ya aina yake mchezaji nguli, Yaya Toure kwenye Uwanja wa Etihad.

Nahodha huyo wa zamani wa Ivory Coast, jana alicheza mchezo wa mwisho kwenye uwanja huo baada ya kudumu kwa miaka minane.

Katika mchezo wa jana usiku, Yaya alikuwa nahodha na aliingoza Man City kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Brighton.

Nguli huyo mwenye miaka 34, ametangaza kuondoka Man City baada ya mkataba wake kumalizika majira ya kiangazi mwishoni mwa msimu.

Wachezaji wa Man City na Brighton walipanga mstari na Yaya kumuaga na muda mfupi baadaye nahodha Vincent Kompany alimtaja nguli huyo ni shujaa wa Man City.

“Unastahili kuagwa kwa heshima kubwa kama hii, wewe ni gwiji wa Man City na utabaki kuwa shujaa wa Man City,”alisema Kompany.

Yaya alikabidhiwa picha huku kaka yake Kolo Toure aliyewahi kucheza Man City akishuhudia pembeni.

Uwanja wa Etihad ilipambwa na mabango yenye picha za kiungo huyo na baadhi ya mashabiki wakiwemo watoto walimpamba kwa majina tofauti.

Hata baada ya kutoka wachezaji wenzake walimkumbatia huku Sadio Sane akionyesha hisia kwa nguli huyo walipokuwa wamekumbatiana. Yaya alitoka dakika tano kabla ya mpira kumalizika na alikwenda moja kwa moja kumkumbatia kocha Pep Guardiola.

Mchezaji huyo alijiunga na Man City mwaka 2007 kutoka Barcelona na ameitumikia Man City katika michezo 230 na amefunga mabao 62.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…