The Manchester City (The Citizens) | Special Thread

The Manchester City (The Citizens) | Special Thread

pengine nusu fainali yaweza kua hivi

REAL MADRID Vs Bayern Munich

Liverpool Vs Barca
Na ndo Madrid mnachoomba [emoji23][emoji23]

Japo bado Liverpool hana ubavu wa kuiondoa Barca UCL
 
Kitu pekee ambacho Guardiola anatakiwa awe anamshukuru Mungu. Katika maisha yake ya ukocha. Nikupata bahati ya kumfundisha Messi. Enzi alipokuwa kwenye kilele cha kiburi, jeuri, na ubabe. Huku akifanya ukatili wa kuitetemesha mikono ya wazee kama Ferguson.

Ni sababu alikuwa akiishi kwenye safina. Iliyokuwa ikiendeshwa na miujiza inayoishi kwenye viatu vya Lionel Messi.

Tangu ilipovunjika ndoa ya Messi na pep. Simulizi ya Guardiola usiku wa Ulaya imejaa simanzi na huzuni kila anakopita. Mbinu zake zinapopata utasa nakushindwa kuzalisha magoal.

Pep anakosa mtu mwenye uwezo wa kuibeba timu kwa uwezo binafsi. Kitu pekee ambacho Guardiola anawashinda mameneja wengine kwasasa usiku wa Ulaya. Nikumiliki suruali nyingi zilizo ktk mtindo wa model.
 
Labda wapigwe kadi nyekundu liverpool kumbuka pep toka kaja england kamfunga liverpool mech moja tu ktk 4
Tena isiwe kadi moja, ziwe kadi kama 3 hivi, hata mechi ya kwanza EPL City walipata advantage kwa Liver kupewa redcard
 
Tena isiwe kadi moja, ziwe kadi kama 3 hivi, hata mechi ya kwanza EPL City walipata advantage kwa Liver kupewa redcard
Fact mkuu hata mm hua naamini hivyo klopp anamuonea sana pep huyu klopp anashambulia sana halina woga
 
Madrid anachukua kombe kwa mara ya tatu mechi wangeanza nyumban kwa city liverpool angekufa historia inawahukumu city nyumban kwa liverpool kibaya zaid karuhusu magoli mengi hata kama city atashinda mech ijayo ila liverpool lazima watapata goli nilipoona mech inaanzia nyumban kwa liverpool nilijua city yupo hatarin sana labda itokee miujiza tu pia klopp ndo kocha anaemsumbua sana pep mech ijayo natabiri sale liverpool kishapita.
Man u bado roho inawauma tu[emoji13] [emoji13] tatzo sio makosa yetu ila nia salah na rob wanataka sifa!!
 
Kipi kisichowezekana labda
Kumbuka Liverpool akili zao kwasasa ni kuhakikisha hawaruhusu goli, inshort hawaendi Etihad kutafuta magoli, yaani ni mwendo wa kuhakikisha hawawaruhusu City kuona lango lao,
 
Michuano ya klabu bingwa barani Ulayani, hatua ya robo fainali inaendelea usiku wa kuamkia leo. Michezo miwili imepigwa ambapo Barcelona wakiwa nyumbani dhidi ya As Roma wamepata ushindi wa mabao 4-1.
Mabao ya Barcelona katika mchezo huo, yamefungwa na wachezaji De Rossi ,Kostas Manolas ambao walijifunga wenyewe.Goli la tatu limefungwa na Gelard Pique huku bao la nne likipachikwa na Luis Suarez, bao la kufutia machozi la As Roma likifungwa na Edin Dzeko.
Katika mchezo mwingine Liverpool wao wamewachapa bila huruma vinara wa ligi kuu ya England Manchester city bao 3-0, Magoli ya Liverpool yamefungwa na Mohamed Salah, Oxlade Chamberlin pamoja na Sadio Mane.
Robo fainali nyingine ya pili itafanyika tarehe 10 mwezi April kwa michezo miwili,As Roma itacheza dhidi ya Barcelona na Manchester City itachuana na Liverpool, na Aprili 11 Bayen Munich itacheza na Sevilla huku Real Madrid ikicheza na Juventus.
 
Liva walicheza fresh jana....hongera kwao....
Ila kati ya timu nisizoziamini mojawapo ni mitomingi hawa....
Unaweza shangaa next match wanapigwa pampu nyingi za maana...,
subira muhimu....
All in all city mpigwe2....mtoke kwa aibu ya kupigwa kamba nyingi...
 
Hii page ilichangamka sana juzi hadi nilikimbia kwatulichofanywa
 
Back
Top Bottom