Mwaka 2011 nilikuwa form one ...kiufupi ndio nilikuwa na akili ya kuaanza kufuatilia mpira ,wakati Niko primary sikuwahi kufuatilia mpira zaidi ilikuwa movie tu ,tena za kihind ,enzi hizo koyla ,Krish ,Karan na arjun ,yaan ulikuwa huwezi nambia kitu cha burudani zaidi ya movie ........,Sasa baada ya kuaangalia hio game nilikuwa na mshikaji wangu anaitwa peter ,alikuwa anamkubali Sana ballotel kisa alikuwa mhuni na mkorofi kama yeye ,na alikuwa nigga kipindi hicho ,mpaka saizi peter anamalizia MD pale bugando na nishabikie wa city hatari kila siku status anatupia magoli ,highlight na habari zote za city ,na Mimi nilianza kumpenda ballotel ,teves ,aguero ,mpaka tukiwa tunacheza mpira form one ulikuwa huwezi nambia kitu kwa aguero .....!
Harafu kuna rafiki yangu alikuwa anawapenda psquare ,anadance kawa wao,alikuwa anajiita Scott ,aisee huyu ndio alinipa unyama zaidi kuhusu man city ,na alizidi kunifanya kuifuatilia city kuliko timu yeyote ,sijajua mpaka saizi Yuko wapi Scott [emoji28][emoji28][emoji28]...
Aisee Mimi nimeanza kushabikia mpira city ndio anadomanite league ,na nilizungukwa na jamaa zangu wanaoipenda city ,...Sasa ilikuwa ngumu Sana kuaanza kuipenda sijui united ,Liverpool sijui arsenal ....
Over