The Most 5 skilled RAPPER in Bongo Hip Hop Of All Time.

The Most 5 skilled RAPPER in Bongo Hip Hop Of All Time.

Moe
Jcb
Hashimu Dogo
Afande Sele
FA
In no particular order
Huyu Hashim dogo ni jinga tu hamna kitu humo, kuna jamaa alikuwa akimsifia nikaja kutafuta collection ya nyimbo zake pumba tupu ni matusi nikaitupilia mbali!
 
One incredible na nikki mbishi are the most skilled rappers if we talk about skills, meaning utunzi, wordplays, rhymes and flows.
Nikki mbishi anakuwa bora zaidi b'cz anajua kufreestyle sana tofauti na wasanii wengi wakubwa wa hip hop. Fid is also skilled and he's good with rhymes, flow na utunzi ( bila kusahau misemo ) but when it comes to wordplays he can't stand the comparison with nikki au one.
True that 100% nikk ni another case kwa wordplays na hapa ndio anawakalisha rapper wengi kama kina God Zilla, Pia ana vitu vingi vya ziada vilivyofanya kumuweka namba tano badala ya One the Incredible japo one na nikk hawapishani mbali sana. Laiti kama list ingekuwa top 10 basi bila shaka angekuwemo katika list hiyo.
 
Mahaba niuwe.kumbe...???..hivi unamuachaje mtu kama joo makin au afnd sele kwenye hizo countdown zako...???
 
Mahaba niuwe.kumbe...???..hivi unamuachaje mtu kama joo makin au afnd sele kwenye hizo countdown zako...???

Johmakini sio skilled rapper ni commercial rapper soma kichwa cha uzi vizuri, Pia kuhusu Afande ni kweli anastahili kuwa kwenye hiyo list japo afande kwa muda mrefu ni kama amaweka mbali shughuli za mziki na kujikita na siasa.

Pia hii ni list binafsi unaweza kukosoa na kuja na list yako pia, thus why nilisha sema toka hapo mwanzoni NENO LANGU SIO SHERIA.
 
Huyu Hashim dogo ni jinga tu hamna kitu humo, kuna jamaa alikuwa akimsifia nikaja kutafuta collection ya nyimbo zake pumba tupu ni matusi nikaitupilia mbali!
Dogo ni the most gifted emcee we've ever had...
 
Nimeikumbuka hii mistari,

Hivi vitu viko wazi, kama vazi la kahaba,
Nasambaza maradhi, halafu nakupa Siku 7,
Machozi ni haba, Uokozi ni Njozi baba,
Ulimwengu wa Saba, Jehanam ya aina yake,

Kipe kitu kikupe, kikutupe kupe akikunyonya damu kwa hamu,
Kama hujafaham, DOGO mwanaharam,
Kalam inamwaga damu,

Nakuacha mweupe ka' mkorogo,
Chata ka' wagogo,
Wabongo acheni nyodo,
Wote mnakula hongo,

Hivi hii ni Serikali,
Au Sera Kali kwa mbali,
Au sera za mali,

Ni ipi, tafakari, nakufa kiume,
Tunapokwenda pana Zali,
Vichaa wangu walume wananyaka hiyo hali,

Tujitume, Pesa tuchume, kwa mwezi tudake,
Utake usitake, kila mjuba sasa kivyake mifuko itune,
Kama hujipendi njoo nichune, wabongo roho ziume,

Kama hufiki, usijikune,
Hivi inatiki,
Kila siku ya wiki,
Ikipata karatasi, wino hutoka kwa kasi,
Basi nina wasiwasi, kwa haya nawahasi,


Kiu ya Jicho, ulicho nacho ndicho ulicho,
Bongo ni Kama ficho, ya huwezi huchezi na anga,
Tokea '78 wabongo wamefunga mkanda!!
 
kwanini Joh makin hayupo katika list hii?
Hit single za Jcb ni ngapi hadi kuingizwa katika list tena nafasi za juu kabisa?
mara ya mwisho Jcb alitoa hit tanfu lini
Si bora ungeuliza Ngwair kwa nn hayupo? Joh mistari miwili ya bata nyimbo imeisha
 
Back
Top Bottom