The Network: Abdul kiungo muhimu kati ya Rostam Aziz na Mukhsin Patel upande mmoja na Sameer Karim Alibhai na W. Salum upande mwingine

The Network: Abdul kiungo muhimu kati ya Rostam Aziz na Mukhsin Patel upande mmoja na Sameer Karim Alibhai na W. Salum upande mwingine

Kwani vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vinafanya kazi gani? Sielewi .!

Kama wao wanabariki hayo, basi wamejiridhisha nchi iko salama.
 
Sheria zetu ni mbovu hawa wahuni ilibidi wawajibishwe kama China wanavyofanya kwa mafisadi
Tatizo siyo sheria. Tatizo ni kulindana au niseme ngazi ya juu wote ni mafisadi. Wangekuwa wanafungwa hata mwaka mmoja au kupigwa faini tu na kurudi mitaani kufanya tena makosa hapo ndiyo ungesema tatizo ni sheria.

Shida ni kuwa hawakamatwi kabisa na wanaachiwa kufanya walitakalo. Hii ina maana hata ukiweka sheria ya kunyonga wataonyongwa watawakuwa watu wadogo kabisa na wao hawatakamatwa.
 
Sana tena walianza Mama Abdul akiwa Vice P. Kwa nchi inayojitambua, Mama hakuwa na sifa za kuwa Raisi. Naona muendelezo, watakomba kila kitu. Watanzania sijui tulikosea wapi!!!
Mlaumu mkuu wa majeshi. Japo timu Mgufuli nayo haikuwa safi na ilitaka kuweka mtu wake kwa sababu ya maslahi binafsi tu, lakini sidhani kama wangeuza Tanganyika kama inavyofanywa sasa.
 
Tatizo siyo sheria. Tatizo ni kulindana au niseme ngazi ya juu wote ni mafisadi. Wangekuwa wanafungwa hata mwaka mmoja au kupigwa faini tu na kurudi mitaani kufanya tena makosa hapo ndiyo ungesema tatizo ni sheria.

Shida ni kuwa hawakamatwi kabisa na wanaachiwa kufanya walitakalo. Hii ina maana hata ukiweka sheria ya kunyonga wataonyongwa watawakuwa watu wadogo kabisa na wao hawatakamatwa.
Uko sahihi mkuu
 
Moja ya project zetu za hovyo za kufanya experiment za uongozi. This project has failed miserably. Na waliofanya hii project sijui wanajisikiaje
Sasshivi ndo naelewa akina dhamira ya akina Bashiru na TISS aliyekuwepo kupinga Samia kupewa Urais,,ila ndo katiba ikabidi Generally asimamie katiba hata kama limtu lenyenwe ni viviu hatintunaibiwa kwa kutumia mkono wake
 
Huyo alikua msaidizi wa magu
… meaning kama ni lawama apewe magu

You want to glorify one person by you don’t want to associate him with his most important choice he ever made

Magufuli ndiye aliyetupa zawadi ya Samia…. Kuna kitu aliona

Naamini kipo
CCM walimlazimisha,hatayeye aliwahi kusema kuwa alipensa Hussein Mwinyi awe makamu wake lakin akina kikwete na kinana wakalazinisha
 
Na ili Tanzania ikae sawa, lazima waje watu wapya wenye fikra tofauti na hawa wanaotuona hatuna akili. Sijui watatoka wapi ila watakuja. Tena wanaweza kuja wakisindikizwa na radi na mafuriko.
Yangu macho....
Kuna scenario moja ambayo watanzania wengi hawaielewi. Ukitaka kuwa na viongozi wanaowajibika unatakiwa kuwa kufanya jambo moja tu: Kiongozi aliye madarakani anatakiwa awe na hofu na kuwe na uwezekano wa kuondolewa kwenye madaraka katika uchaguzi utakaofuata kama hatawajibika na kama alifanya makosa, kuwe na uwezo wa kumshtaki. Hili ni muhimu sana na litawezekana tu kwa kuwa na mfumo wa haki wa uchaguzi.
Nguvu ya kuwa donor country hakuwa nayo. Ni maneno ya kupumbaza watu.
Kukataa mgombea mwenza kulihitaji nguvu gani?
 
Sheria Mama ni Katiba ndio pekee inayoweza kurekebisha hayo mapungufu !
Ila walioshika mpini hawataki kusikia habari hiyo 🙄

Wanaendelea kupiga danadana Ufukweni kwanza 🙄
 
Nguvu ya kuwa donor country hakuwa nayo. Ni maneno ya kupumbaza watu.
Kukataa mgombea mwenza kulihitaji nguvu gani?
Mkuu, Magufuli alikuwa hamkubali Samia kiutendaji hata kidogo. Ila kwa vile alikuwa ni mtu mpenda kunyenyekewa na kusifiwa, na Samia alijua kufanya hivyo, basi akaamua kuendelea naye kwani hakujua kuwa anaweza kufariki mapema hivyo. Alidhani atamaliza muda wake wa urais na kumweka mtu atakayemtaka yeye. Kwa kifupi alijisemea kuwa ''huyu mwache tu, madhali nguvu zote ziko kwa rais na ananitii, hakuna shida. Kuna habari kuwa Magufuli alizidiwa ghafla hivyo akashindwa kufanya maamuiz yoyote, lakini angekuwa ameugua ugonjwa usioua ghafla, basi kungekuwa na mabadiliko kabla hajafa.
 
Back
Top Bottom