The Network: Abdul kiungo muhimu kati ya Rostam Aziz na Mukhsin Patel upande mmoja na Sameer Karim Alibhai na W. Salum upande mwingine

The Network: Abdul kiungo muhimu kati ya Rostam Aziz na Mukhsin Patel upande mmoja na Sameer Karim Alibhai na W. Salum upande mwingine

Mkuu, Magufuli alikuwa hamkubali Samia kiutendaji hata kidogo. Ila kwa vile alikuwa ni mtu mpenda kunyenyekewa na kusifiwa, na Samia alijua kufanya hivyo, basi akaamua kuendelea naye kwani hakujua kuwa anaweza kufariki mapema hivyo. Alidhani atamaliza muda wake wa urais na kumweka mtu atakayemtaka yeye. Kwa kifupi alijisemea kuwa ''huyu mwache tu, madhali nguvu zote ziko kwa rais na ananitii, hakuna shida. Kuna habari kuwa Magufuli alizidiwa ghafla hivyo akashindwa kufanya maamuiz yoyote, lakini angekuwa ameugua ugonjwa usioua ghafla, basi kungekuwa na mabadiliko kabla hajafa.
Naheshimu mtizamo wako.
 
Kuna mambo mengi yatafunuka ndani ya siku chache zijazo kuhusiana na huu mtandao.

Kwanini tunarudishwa kwenye ujinga uleule?

Rostam, you can do better than this! Enzi za JK hukujifunza mzee?

Elewa kuwa kila hatua, kila kinachofanyika - viko well documented. Ni suala la muda tu.
Si mliona jinsi Rostam azizi alivyosimama majukwaani kwa hoja za ovyo kutetea kuporwa bandari zetu zote na dubai? Eti msipozalisha kitu hamli kitu kwa hivyo tuwape waarabu bandari zetu. Yaani tusomeshe watoto wetu umeneja na ufundi waletwe mameneja na mafundi wafilipino nchini. Yaani tuwe watazamaji tu hatuwezi hata kujua muwekezaji anaingiza faida kiasi gani kwa hivyo tudai kulipwa ngapi. Ule mkataba Adam Malima alisema hata haufai kwa kulumangia ugali ndio rostam aziz alitoka huko anajificha kuja kutetea. Asante sana Adam Malima kwa uzalendo wako. Yule mama supika yeye akatuita wenye kupinga huo mkataba wapumbavu. Wananchi wataamua hatima yake.
 
Naiona regime kama ya Bukinabe ikijongea, itasafisha miungu watu wanaoogelea katika damu za wanyonge wakimuacha mama Tanzania, akiendelea kutembeza bakuli huku akimiminia katika midoyo yao wazi. Eee Mungu tuepushe na hali hiyo weka macho ndani ya mioyo yao waone.
 
Ila huyu Abdul anapata wapi hizi nguvu?
Je ni Mama anampa support?
Je Usalama wanaona haya?
Muda ni mwalimu mzuri sana!
Ila hawa akina Rostam wamesahau haraka sana, watakuja kujutia haya!
 
Nani alipaswa kuwa raisi kwa mujibu wa katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania?
Mama sa100 ana haki kikatiba na anaupiga mwingi nchi imetulia inapiga hatua kimaendeleo kila mtu anaona japo napenda sana akope matrilioni amalize kwanza kujenga SGR Dar-Mwanza/Kigoma pesa yote itarudi aache kwanza miradi mingine atakuwa bonge la Rais wa mfano Afrika maana tutapiga pesa nyingi mno kusafirisha haraka mizigo ya nchi jirani na kuwa super power East Africa. Kenya walijenga SGR yao ili kuua bandari zetu na uchumi wetu bahati nzuri reli ikaishia njiani sijui Naivasha kwa ufisadi wa kutisha , otherwise mda huu tungekuwa tunawaamkia shikamoo jogoo.

Shida iko kwenye akili zetu za chuo zinazofundisha kuandika katiba, Rais anapokufa madarakani inapaswa katiba iseme ufanyike uchaguzi ndani ya miezi mitatu ila katiba ya Nyereri yenye falsafa ya ukoo wa panya na wasomi wa sheria wapo eti haisemi hivyo na hapo ndo utadharau sana wanasheria wetu. Sijui wana shida gani. Angalia Iran Rais Ebrahim amekufa juzikati wanarudi kwenye sanduku la kura, kule hakuna kupeana urais bila kutembea juani vijijini kuomba kura na kutoa ahadi na kunadi sera zikapimwa wanaosema siyo waseme siyoo, wanaosema ndiyo waseme ndiyoooooo! Yule dingi amekufa ila bado tunaogopa hadi kivuli chake na hii ni sumu kubwa ya maendeleo.
 
Tangu Nchi ipate Uhuru watu ni wale wale na watoto wao na wote ni wa kutoka mule mule 😳

Lakini watu humu jf wanajaribu kujiaminisha kwamba awamu hii ndio imeharibu zaidi kuliko nyingine zilizopita !
Hakuna kitu kama hicho 🙄
Midundo ni ile ile tangu Enzi na Enzi 😳
Na hata ikija awamu nyingine midundo ni ile ile kwa sababu watu watakuwa ni wale wale 🙄

Labda kitakacho badilika ni sura za watu na staili ya miondoko lakini watu watakuwa ni wale wale 😳😷🤠🫵
 
Back
Top Bottom