The Official Azam FC Thread

[h=1]Azam FC yarejea kileleni VPL, yaiteketeza Ruvu Shooting 3-0[/h] Submitted by ppkahemele on Sun, 2013-11-03 07:25




Ushindi wa 3-0 dhidi ya Ruvu Shooting Stars umeiwezesha Azam FC kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi kuu Tanzania bara ikiwa imesalia na mchezo mmoja kumaliza mzunguko wa kwanza wa msimu huu wa 2013-2014.

Azam FC imepata ushindi huo na kufikisha pointi 26 sawa na Mbeya City ya mkoani Mbeya zikitofautiana kwa idadi ya magoli huku timu zote zikiwa hazijapoteza hata mchezo mmoja, kwa matokeo ya jana timu ya Yanga inashuka hadi nafasi ya tatu.

Mbeya City na Azam FC zitakutana katika mchezo wao wa mwisho wa kukamilisha hatua ya mzunguko wa kwanza, mchezo ambao kila timu itahitaji kushinda ili isiharibu rekodi yake pamoja na kuendelea kuongoza kwenye msimamo wa ligi kuu, mechi hiyo itachezwa Nov 7 kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi na kurushwa moja kwa moja na Azam TV kupitia Chanel 10.

Katika mchezo wa huo uliozikutanisha Azam FC na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Azam Complex, Azam FC waliandika bao la kwanza mapema katika dakika ya kwanza ya mchezo kupitia kwa mshambuliaji Kipre Tchetche aliyeunganisha vizuri mpira wa Joseph Kimwaga.

Azam FC ikiongoza 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting, ilipata goli la pili mwishoni mwa kipindi cha kwanza katika dakika ya 45, goli lililofungwa na mshambuliaji chipukizi Kimwaga kwa kichwa akimalizia mpira wa mwisho uliopigwa na Waziri Salum na kupeleka timu zote mapumziko Azam FC wakiongoza 2 huku Ruvu wakiwa hawajapata kitu.

Kipindi cha pili timu zote ziliingia kwa kasi Azam FC walifanya mabadiliko dakika ya 60 alitoka nahodha Himid Mao nafasi yake ikachukuliwa na Jabir Aziz na dk 68 aliingia Farid Maliki kuchukua nafasi ya Kimwaga mabadiliko hayo yaliisaidia Azam FC kupata goli la tatu katika dakika ya 70 kupitia kwa Khamis Mcha aliyetumia vyema uzembe wa beki ya Ruvu na kumalizia mpira wa Kipre, goli hilo lilimaliza mchezo Azam FC wakiondoka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Ruvu Shooting.

Kipre amefikisha jumla ya magoli saba ya kufunga huku Kimwaga na Mcha wakifikisha magoli mawili kila mmoja.

Ruvu Shooting watajutia nafasi za wazi walizokosa katika nyakati tofauti wachezaji Hassan Dilunga, Cosmas Lewis, Elius Maguli na Said Dilunga walijaribu kupiga mashuti lakini yakaokolewa na kipa Mwadini Ally wa Azam FC na mengine kutoka nje hivyo kumaliza mchezo wakiwa hawajaziona nyavu za Azam FC.

Azam FC: Mwadini Ally, Erasto Nyoni, Waziri Salum, Said Morad, Aggrey Moris, Kipre Bolou, Joseph Kimwaga/Farid Maliki 68', Himid Mao/Jabir Aziz 60', Kipre Tchetche, Humphrey Mieno/Kelvin Friday 83' na Khamis Mcha.

Ruvu Shooting: Abdul Juma, Michael Aidan, Stephano Mwasyika, Mangasini Mbonosi, Shaaban Sunza, Juma Seif Dion, Juma Nade, Hassan Dilunga, Said Dilunga, Elias Maguli na Cosmas Lewis/Raphael Kiara.
 
[h=1]PRESS RELEASE[/h]
Submitted by ppkahemele on Thu, 2013-11-07 18:54




Azam FC and Coach Stewart John Hall have decided by mutual agreement to terminate the existing contract with immediate effect. The partnership has been mutually rewarding to both parties and has been the continual and consistent growth of Azam FC into one of the most progressive and visionary football clubs in Africa. The timing of the decision is critical and coming at the end of round 1 and will allow the coach the opportunity to take up a new challenge and the club to replace him in an appropriate manner.
The club would like to place on record its gratitude to the coach for his hard work and professionalism. He has proved himself over his two spells to be a coach of outstanding technical and tactical acumen. He will continue to be a friend and supporter of Azam FC and will always be most welcome at the football club. SOURCE: PRESS RELEASE | The Official Website of Azam Football Club
We gonna miss you Stewart Hall and we wish you all the best
 
By Emmanuel Muga BBC News, Dar es Salaam England-born coach Stuart John Hall has parted company with Azam FC and alleged the Tanzanian league is rigged in favour of the country's two top teams.
"The Tanzanian football is organized in favour of two teams, Simba and Yanga," Hall told BBC Sport.
"Fixtures, refereeing, administration are all rigged to favour them, that's why Azam has failed to topple them."
The Tanzania Football Federation (TFF) officials were not readily available to comment on Hall's allegations. BBC Sport - Hall leaves Azam and alleges Tanzanian league is fixed
 
November 9, 2013, Dar-es-Salaam, Tanzania. Kipre Tchetche jana alitwaa tuzo mbili za Mwanaspoti kutokana na kiwango alichokionesha msimu uliopita.Kipre Tchetche alishinda tuzo ya ufungaji bora wa ligi kuu Vodacom akiwa na magoli 17 kabla ya baadaye kushinda tena tuzo ya kuwemo kwenye kikosi cha wachezaji 11 bora wa VPL.
Kikosi hicho kinaundwa na Juma Kaseja, Mbuyu Twite, Shomary Kapombe, Kevin Yondan, David Mwantika, Amri Kiemba, Thomas Ulimwengu, Haruna Niyonzima, Themi Felix, Mbwana Samatta na Kipre Tchetche.
Mchezaji mwingine wa Azam FC aliyeshinda tuzo ni David Mwantika ambaye kwa bahati mbaya hakuwepo ukumbini na zawadi yake kuchukuliwa na mwakilishi wake. David alishinda tuzo ya kuwa Sentahafu Bora wa msimu uliopita.
Joseph Kimwaga jana alishinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi kwa mara nyingine tena akiwaangusha Ramadhani Singano wa Simba na Juma Luizio wa Mtibwa
Kimwaga ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya vijana na ambaye majuzi kocha mkuu wa timu ya taifa Kim Paulsen amemjumuisha kwenye kikosi chake cha wakubwa alikuwepo kwenye hafla hiyo akisindikizwa na nahodha wake Mgaya Abdul na kupokea tuzo yake yeye mwenyewe kama anavyoonekana pichani. Source: David Mwantika, Kipre Tchetche watisha tuzo za Mwanaspoti | The Official Website of Azam Football Club
 
Uhai Cup 2013 (U20)

Azam academy 1 - 2 Coastal Union
 
Uhai Cup U20 2013

azam academy 1 - 0 JKT Ruvu

leo
azam academy 2 - 0 yanga
 
NUSU FAINALI UHAI CUP

Kesho (alhamisi): AZAM ACADEMY Vs COASTAL UNION U20

Ijumaa: YANGA U20 Vs MTIBWA SUGAR U20
 
uhai cup robo fainali result:
azam 2-1 t.prison

coastal union 1-0 jkt oljoro

yanga 2-1 ashant united

simba sc 2-3 mtibwa sugar
 
LICHA ya kuyaaga mashindano ya uhai Cup katika ngazi ya nusu fainali baada ya kufungwa 1-0 na Coastal Union, wanafainali wa Uhai Cup mwaka jana ambapo kombe lilichukuliwa na Azam Academy, bado Azam Academy imekuwa timu ya mfano na kujivunia baada ya kutoa wachezaji wanne kwenye kikosi cha timu ya taifa Kilimanjaro Stars inayoshiriki mashindano ya GoTV CECAFA Challenge Cup

Huenda kutolewa kwa Azam Academy kumechangiwa na kukosekana kwa nyota hao ambao haiyumkini uwepo wao ungeisaidia sana Azam Academy, lakini uongozi wa Azam FC bado unajivunia kikosi chake cha timu ya vijana.

Uongozi wa Azam FC haumlaumu kocha kim Poulsen kwa kuchukua wachezaji wake bali unajisikia faraja kuona vijana wake wakipata nafasi ya kuwakilisha nchi kwani hilo ndilo lengo kuu la Azam FC (Mapinduzi ya Soka la Tanzania)

Aishi Salum Manula, mmoja wa magolikipa bora nchini na mlinda mlango namba mbili wa kikosi cha kwanza cha Azam FC anatoka kwenye academy hii na hii ni faida zaidi ya kutwaa Uhai Cup.

Lakini si Aishi pekee, Farid Mussa Malik na mchezaji bora wa vijana wa Gazeti la Mwanaspoti Joseph Kimwaga ambaye goli lake la dakika ya 90 lilitosha kuipa ushindi Azam FC dhidi ya Yanga wamo kwenye kikosi cha timu ya taifa na hili linaifanya Academy ya Azam FC iwe na maaana zaidi ya academy nyingize zilizopo nchini.

Katika kikosi kilichopo Nairobi, kocha Kim Paulsen amemjumuisha Ismail Adam Gambo kikosini na kufanya wachezaji kutoka Azam Academy kufika wanne.



Lakini utasema nini kuhusu Braison Raphael? Huyu ni zaidi ya lulu kwenye soka la Tanzania, moyo wake wa kupambana, ushujaa wa kujitolea na safari zake kwenye dimba la soka kunamfanya awe mchezaji wa kipekee… ni dhahiri Braison Raphale atapaa kwenda kikosi cha kwanza hivi karibuni kama ilivyo kwa Gardian Michale ambae kama ilivyo kwa Braison, wameonesha kiwango kikubwa sana.

Wachezaji wengine walioonesha kiwango kikubwa kwenye mashindano haya ni, beki wa kati Yaruk Dizana na winga teleza mwenye uwezo mkubwa na kuuchezea mpira Erick Haule….

Wawili hawa watapata mafanikio makubwa sana kama watapata nafasi ya kujiendeleza.

Azam Academy pia inajivunia uwepo wa Mudathir Yahya kwenye kikosi cha kwanza ambaye ameungana na Samih Haji Nuhu na Himid Mao Mkamy ambao walipandishwa miaka mitatu iliyopita.

Kutokana na hayo licha ya Azam FC kusononeka kutokana na kutolewa kwenye hatua ya nusu fainali za Uhai Cup, lakini mafanikio haya ya kuzalisha vipaji ambayo vimeweza kupevuka na kuwa na manufaa ndani ya muda mfupi unatoa faraja na kuonesha dira ya mafanikio.
 
majibu ya leoo hii..
 

Attachments

  • wp_ss_20131130_0001.png
    29.8 KB · Views: 47
[h=1]Joseph Marius Omog – Kocha Mpya Azam Football Club[/h]
Submitted by ppkahemele on Sat, 2013-11-30 12:36




Klabu ya Azam inapenda kuufahamisha umma hususan wapenzi wa mpira wa miguu kuwa imeingia mkataba na kocha Joseph Marius Omograia wa Cameroon kwa kipindi cha miakamiwili (2) kuanzia leo.
Kocha Omog ni bingwa kwani anakuja kuifundisha Azam akiwa ametoka kuiongoza klabu ya A.C Leopards ya Jamhuri ya Kongo (Brazaville) kutwaa ubingwa wa ligi ya nchi hiyo kwa misimu miwili mfululizo (2012 na 2013). Timu hii ilikuwa haijatwaa ubingwa wa ligi kwa zaidi ya miaka 30. Kwa mwaka huu wametwaa ubingwa wakiwaacha wapinzani wao, Diables Noirs kwa pengo la pointi kumi (10) wakikusanya pointi 87 katika ligi yenye timu 18.
Pia ni mwaka jana tu (2012) aliiwezesha A.C Leopards kunyakua ubingwa wa Kombe la Shirikisho la Afrika kwa kuzipiga kumbo timu ngumu na zenye uzoefu mkubwa kama vile Mas de Fes ya Morocco, Heartlands ya Nigeria na Sfaxien ya Tunisia.
Mafanikio hayo ya kutwaa ubingwa wa Afrika yalifikiwa baada ya miaka 38 tangu klabu ya Jamhuri yas Kongo ifanye hivyo, na kumfanya kocha Omog kuwa moja ya makocha wa kupigiwa mfano barani Afrika.
Kadhalika mwaka huu 2013, A.C Leopards chini ya ukufunzi wa Omog ilitinga hatua ya makundi ya Ligi ya mabnigwa Afrika na kupangwa katika kundi moja na timu mbili zilizocheza fainali; Al Ahly ya Misiri (bingwa) na Orlando Pirates ya Afrika Kusini.
Yote hayo ameyafanya akitumia asilimia kubwa ya wachezaji wa ndani ya Kongo huku akiwainua kutoka katika hali ya kuonekana wachezaji wa wastani hadi kuwa tishio na kuhofiwa kote barani Afrika.
Azam Football Club inamuona kocha Omog kuwa anakidhi vigezo vya kuendana na dira ya klabu ambayo ni kukuza na kuwaendeleza wachezaji na kushindana kwa kiwango cha juu kwa lengo la kuwa mabingwa katika mashindano mabalimbali ambayo timu inashiriki.
Uongozi wa Azam FC utampatia ushirikiano wa kutosha ili kufanikisha malengo na mipango thabiti ya klabu.

Maelezo Binafsi
Kocha Omog ni mchezaji wa zamani wa timu ya Dragon Yaounde Cameroon. Alipata mafunzo ya ualimu wa michezo na elimu ya viungo (Sports and physical education) kutoka chuo cha vijana na michezo (Higher Institute of Youth and Sports, INJS Yaounde).
Baadaye alipata fursa ya kujiendeleza nchini Ujerumani ambako mwaka 1987 alitunukiwa stashahada ya ukufunzi wa mpira wa miguu na leseni B ya ukocha kwa viwango vya Shirikisho la mpira wa miguu barani Ulaya, UEFA.
Aliporejea nyumbani kwao Cameroon Joseph Marius Omog, alifundisha kabumbu katika klabu mbalimbali, zikiwemo; Fovu of Baham na Aigle of Menoua na kufanikiwa kufuzu kwa fainali za kombe la Cameroon. Mwaka 2001 aliteuliwa kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Cameroon, Indomitable Lions chini ya kocha raia wa Ujerumani Winfried Schafer.
Omog amewahi pia kufundisha timu ya taifa ya Cameroon iliyoundwa na wachezaji wa ndani ijulikanayo kama Intermediate Lions hadi mwaka 2010 na baada ya hapo akelekea Kongo kuionoa A.C Leopards kwa mafanikio makubwa na hasa kutwaa ubingwa wa kombe la Shirikisho wakiifunga Djoliba ya Mali kwa ushindi wa jumla wa magoli 4-3 katika michezo miwili ya fainali.
Uongozi,
Azam Football Club,
Source: Joseph Marius Omog

Novemba 30, 2013
 
wellcome josee at chamazi stadio..
 
TRANSFER NEWS:
Player's Name : Ismail Mamadou Conte

From: Stella Abidjan (Ivory Coast)

To: Azam FC (Tanzania)
Position : Strike
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…