Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
We gonna miss you Stewart Hall and we wish you all the best
majibu ya leoo hii..LICHA ya kuyaaga mashindano ya uhai Cup katika ngazi ya nusu fainali baada ya kufungwa 1-0 na Coastal Union, wanafainali wa Uhai Cup mwaka jana ambapo kombe lilichukuliwa na Azam Academy, bado Azam Academy imekuwa timu ya mfano na kujivunia baada ya kutoa wachezaji wanne kwenye kikosi cha timu ya taifa Kilimanjaro Stars inayoshiriki mashindano ya GoTV CECAFA Challenge Cup
Huenda kutolewa kwa Azam Academy kumechangiwa na kukosekana kwa nyota hao ambao haiyumkini uwepo wao ungeisaidia sana Azam Academy, lakini uongozi wa Azam FC bado unajivunia kikosi chake cha timu ya vijana.
Uongozi wa Azam FC haumlaumu kocha kim Poulsen kwa kuchukua wachezaji wake bali unajisikia faraja kuona vijana wake wakipata nafasi ya kuwakilisha nchi kwani hilo ndilo lengo kuu la Azam FC (Mapinduzi ya Soka la Tanzania)
Aishi Salum Manula, mmoja wa magolikipa bora nchini na mlinda mlango namba mbili wa kikosi cha kwanza cha Azam FC anatoka kwenye academy hii na hii ni faida zaidi ya kutwaa Uhai Cup.
Lakini si Aishi pekee, Farid Mussa Malik na mchezaji bora wa vijana wa Gazeti la Mwanaspoti Joseph Kimwaga ambaye goli lake la dakika ya 90 lilitosha kuipa ushindi Azam FC dhidi ya Yanga wamo kwenye kikosi cha timu ya taifa na hili linaifanya Academy ya Azam FC iwe na maaana zaidi ya academy nyingize zilizopo nchini.
Katika kikosi kilichopo Nairobi, kocha Kim Paulsen amemjumuisha Ismail Adam Gambo kikosini na kufanya wachezaji kutoka Azam Academy kufika wanne.
Lakini utasema nini kuhusu Braison Raphael? Huyu ni zaidi ya lulu kwenye soka la Tanzania, moyo wake wa kupambana, ushujaa wa kujitolea na safari zake kwenye dimba la soka kunamfanya awe mchezaji wa kipekee¡- ni dhahiri Braison Raphale atapaa kwenda kikosi cha kwanza hivi karibuni kama ilivyo kwa Gardian Michale ambae kama ilivyo kwa Braison, wameonesha kiwango kikubwa sana.
Wachezaji wengine walioonesha kiwango kikubwa kwenye mashindano haya ni, beki wa kati Yaruk Dizana na winga teleza mwenye uwezo mkubwa na kuuchezea mpira Erick Haule¡-.
Wawili hawa watapata mafanikio makubwa sana kama watapata nafasi ya kujiendeleza.
Azam Academy pia inajivunia uwepo wa Mudathir Yahya kwenye kikosi cha kwanza ambaye ameungana na Samih Haji Nuhu na Himid Mao Mkamy ambao walipandishwa miaka mitatu iliyopita.
Kutokana na hayo licha ya Azam FC kusononeka kutokana na kutolewa kwenye hatua ya nusu fainali za Uhai Cup, lakini mafanikio haya ya kuzalisha vipaji ambayo vimeweza kupevuka na kuwa na manufaa ndani ya muda mfupi unatoa faraja na kuonesha dira ya mafanikio.
wellcome josee at chamazi stadio..[h=1]Joseph Marius Omog Kocha Mpya Azam Football Club[/h]
Submitted by ppkahemele on Sat, 2013-11-30 12:36
![]()
Klabu ya Azam inapenda kuufahamisha umma hususan wapenzi wa mpira wa miguu kuwa imeingia mkataba na kocha Joseph Marius Omograia wa Cameroon kwa kipindi cha miakamiwili (2) kuanzia leo.
Kocha Omog ni bingwa kwani anakuja kuifundisha Azam akiwa ametoka kuiongoza klabu ya A.C Leopards ya Jamhuri ya Kongo (Brazaville) kutwaa ubingwa wa ligi ya nchi hiyo kwa misimu miwili mfululizo (2012 na 2013). Timu hii ilikuwa haijatwaa ubingwa wa ligi kwa zaidi ya miaka 30. Kwa mwaka huu wametwaa ubingwa wakiwaacha wapinzani wao, Diables Noirs kwa pengo la pointi kumi (10) wakikusanya pointi 87 katika ligi yenye timu 18.
Pia ni mwaka jana tu (2012) aliiwezesha A.C Leopards kunyakua ubingwa wa Kombe la Shirikisho la Afrika kwa kuzipiga kumbo timu ngumu na zenye uzoefu mkubwa kama vile Mas de Fes ya Morocco, Heartlands ya Nigeria na Sfaxien ya Tunisia.
Mafanikio hayo ya kutwaa ubingwa wa Afrika yalifikiwa baada ya miaka 38 tangu klabu ya Jamhuri yas Kongo ifanye hivyo, na kumfanya kocha Omog kuwa moja ya makocha wa kupigiwa mfano barani Afrika.
Kadhalika mwaka huu 2013, A.C Leopards chini ya ukufunzi wa Omog ilitinga hatua ya makundi ya Ligi ya mabnigwa Afrika na kupangwa katika kundi moja na timu mbili zilizocheza fainali; Al Ahly ya Misiri (bingwa) na Orlando Pirates ya Afrika Kusini.
Yote hayo ameyafanya akitumia asilimia kubwa ya wachezaji wa ndani ya Kongo huku akiwainua kutoka katika hali ya kuonekana wachezaji wa wastani hadi kuwa tishio na kuhofiwa kote barani Afrika.
Azam Football Club inamuona kocha Omog kuwa anakidhi vigezo vya kuendana na dira ya klabu ambayo ni kukuza na kuwaendeleza wachezaji na kushindana kwa kiwango cha juu kwa lengo la kuwa mabingwa katika mashindano mabalimbali ambayo timu inashiriki.
Uongozi wa Azam FC utampatia ushirikiano wa kutosha ili kufanikisha malengo na mipango thabiti ya klabu.
Maelezo Binafsi
Kocha Omog ni mchezaji wa zamani wa timu ya Dragon Yaounde Cameroon. Alipata mafunzo ya ualimu wa michezo na elimu ya viungo (Sports and physical education) kutoka chuo cha vijana na michezo (Higher Institute of Youth and Sports, INJS Yaounde).
Baadaye alipata fursa ya kujiendeleza nchini Ujerumani ambako mwaka 1987 alitunukiwa stashahada ya ukufunzi wa mpira wa miguu na leseni B ya ukocha kwa viwango vya Shirikisho la mpira wa miguu barani Ulaya, UEFA.
Aliporejea nyumbani kwao Cameroon Joseph Marius Omog, alifundisha kabumbu katika klabu mbalimbali, zikiwemo; Fovu of Baham na Aigle of Menoua na kufanikiwa kufuzu kwa fainali za kombe la Cameroon. Mwaka 2001 aliteuliwa kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Cameroon, Indomitable Lions chini ya kocha raia wa Ujerumani Winfried Schafer.
Omog amewahi pia kufundisha timu ya taifa ya Cameroon iliyoundwa na wachezaji wa ndani ijulikanayo kama Intermediate Lions hadi mwaka 2010 na baada ya hapo akelekea Kongo kuionoa A.C Leopards kwa mafanikio makubwa na hasa kutwaa ubingwa wa kombe la Shirikisho wakiifunga Djoliba ya Mali kwa ushindi wa jumla wa magoli 4-3 katika michezo miwili ya fainali.
Uongozi,
Azam Football Club,
Source: Joseph Marius Omog
Novemba 30, 2013
Alafu jamaa anakipaji cha ajabu.TRANSFER NEWS:
Player's Name : Ismail Mamadou Conte
From: Stella Abidjan (Ivory Coast)
To: Azam FC (Tanzania)
Position : Strike