The Official Azam FC Thread

By ndetichia
TRANSFER NEWS:
Player's Name : Ismail Mamadou Conte

From: Stella Abidjan (Ivory Coast)

To: Azam FC (Tanzania)
Position : Striker
source: www.azamfc.co.tz
 
MABORESHO AZAM COMPLEX YAENDELEA, SHIRIKISHO LA SOKA AFRIKA HUENDA IKAPIGWA CHAMAZI

[TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD="align: center"] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Mafundi wakiendelea na zoezi la uwekaji wa viti vya kisasa katika majukwaa ya Uwanja wa Azam Complex, uliopo Chamazi, Dar es Salaam. Klabu ya Azam inataka kuutumia Uwanja huo kwa michuano ya Afrika pia mwakani na inapambana na muda kuhakikisha uboreshaji unakamilika mapema ili mechi zake za Kombe la Shirikisho icheze hapo mwakani.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

[TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD="align: center"] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Siti za kulala[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD="align: center"] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Hiki ni moja ya vyumba vya kubadilishia nguo kwa ajili ya timu, unaweza kujionea ni cha kisasa kabisa[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD="align: center"] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Mafundi wamemaliza kazi ya kupaka rangi na sasa mabinti wanafanya usafi[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD="align: center"] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Chumba cha mikutano, ni cha hadhi ya juu[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

[TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD="align: center"] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Eneo hili ndilo timu zitakuwa zinatokea kuingia uwanjani[/TD]
[/TR]
[/TABLE]



CHANZO: BIN ZUBEIRY BLOG + www.azamfans.blogspots.co.uk

 
well done team mngment kudos sana we make it now..
 
Dah! Mpaka raha yani.
 
MAPINDUZI CUP 2014
03 January2014
Unguja, Zanzibar.

RESULTS: Azam Fc 2 - Spice Stars (Unguja Combine) 0

Azam FC yaanza vema Mapinduzi Cup


Submitted by ppkahemele on Fri, 2014-01-03 16:06




Brian Umony na Himid Mao jana waliifungia Azam FC magoli na kuifanya ianze kwa ushindi wa 2-0 kwenye mashindano ya Mapinduzi Cup yanayorushwa moja kwa moja na Azam TV



Brian Umony aliyeingia dakika ya 59 kuchukua nafasi ya Muamad Ismael Kone, alicheza vizui sana na kusaidia kupatikana kwa ushindi huo.



Himid Mao aliifungia Azam bao la pili dakika ya 86, baada ya kuuwahi mpira uliokuwa unaelekea mikononi mwa kipa Silima kufuatia shuti la Salum Abubakar na kupiga shuti lililotinga nyavuni.



Katika mchezo huo, uliochezeshwa na refa Mfaume Ali, mabadiliko yaliyofanywa na kocha Mcameroon Joseph Marius Omog kipindi cha pili kuwatoa Khamis Mcha ‘Vialli’, Kipre Herman Tchetche na Kone na kuwaingiza Umony, Joseph Kimwaga na Seif Abdallah ndiyo yalileta ushindi huo.

Azam walitawala zaidi mchezo katika dakika 45 za kwanza, lakini wakakosa mbinu za kuivunja ngome ya Spice, inayoundwa na wachezaji mchanganyiko wa Unguja.



Kocha Omog alifanya mabadiliko kwenye kikosi cha kwanza cha Azam leo, akimrejesha Himid Mao kucheza nafasi ya kiungo pamoja na Salum Abubakar ‘Sure Boy’ na Kipre Michael Balou, huku Erasto Nyoni akicheza beki ya kulia na Waziri Salum beki ya kushoto.



Azam ilitawala sehemu ya kiungo na pasi nyingi ziliwafikia washambuliaji Kipre Herman Tchetche na Muamad Ismael Kone, lakini wakashindwa kabisa kufunga kipindi cha kwanza.



Kwa ushindi huo, Azam inaongoza Kundi C kwa pointi zake tatu, na kubaki au kushuka itategemea na matokeo ya mchezo wa pili jioni ya leo Uwanja wa Amaan kati ya Ashanti United ya Dar es Salaam na Tusker FC ya Kenya.


Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Mwadini Ali, Erato Nyoni, Waziri Salum, David Mwantika, Aggrey Morris, Kipre Balou, Himid Mao, Salum Abubakar, Muamad Kone/Brian Umony dk59, Kipre Tchetche/Seif Abdallah dk 70 na Khamis Mcha ‘Vialli/Joseph Kimwaga dk46.

Source: The Official Website of Azam Football Club | Tucheze pamoja kwa furaha
 
leo mapinduzi cup
ft azam fc 1 - 0 tusker fc k tchetche
 
Azam FC leo imeshinda 1-0 dhidi ya Ashanti United, Azam FC imekuwa timu pekee iliyoshinda mechi zote kwenye kombe la Mapinduzi, baada ya kushinda 2-0, 1-0, na 1-0
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…