By ppkahemele on March 12, 2016
Azam FC ‘kazi kazi’ v Bidvest Wits
KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, ipo kamili kabisa kuingia vitani na kusaka matokeo bora katika mchezo huo muhimu wa kwanza wa raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Bidvest Wits utakaofanyika saa 1.00 usiku katika Uwanja wa Bidvest.
Huo ni mchezo wa kwanza kwa Azam FC kwenye michuano ya kimataifa iliyosimamiwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) mwaka huu, mara baada ya mechi hiyo watarudiana na timu hiyo wiki moja ijayo (Machi 20) kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam kuanzia saa 1.00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Kuelekea mchezo huo yafuatayo ni mambo muhimu kuhusu timu zote mbili na namna Azam FC ilivyojipanga vema kusaka ushindi wa ugenini dhidi ya Bidvest Wits inayojiita jina la utani la Clever Boys.
Hali ya hewa?
Azam FC tokea iwasili jijini Johannesburg imekutana na hali ya hewa ya baridi kiasi na mvua zinazonyesha, hivyo kikosi hicho kimejipanga vilivyo kukabiliana na hali ya hewa hiyo na kupata matokeo.
Kama hiyo haitoshi timu hiyo imenunua viatu maalumu vya kukabiliana na Uwanja wa Bidvest pamoja na mvua kama itanyesha, yote hayo yamefanyika ili kuwaweka wachezaji katika mazingira mazuri ya kupata matokeo mazuri
Allan Wanga: Nitawafunga Bidvest Wits | The Official Website of Azam Football Club .
Jambo kubwa na la kupendeza hali ya hewa ya hapa inafanana sana na ile waliyokutana nayo nchini Zambia walipokwenda kushiriki michuano maalumu ya timu nne (Zesco United, Zanaco FC na Chicken Inn)
Ziara ya Zambia yaanza kuzaa matunda Azam FC | The Official Website of Azam Football Club na kutwaa ubingwa wa michuano hiyo, hivyo kambi hiyo ya jijini Ndola imeanza kuipa faida Azam FC.
AZAM FC TV - Ziara ya Azam FC Zambia Source: Azam Football Club youtube
“Tumejiandaa kupambana na hali ya hewa ya hapa kwa sababu ni tofauti sana, pia nyasi za uwanja tutakaotumia zimenyooka na ni za kijani na unaruhusu soka kuchezwa kwa haraka sana, vilevile hali ya hewa ni mvua, na katika kujipanga na mazingira yote hayo kila mchezaji anacho kiatu cha kukabiliana na hayo,” alisema Hall.
Rekodi ya Kocha Stewart Hall?
Hii itakuwa ni mara ya pili kwa Kocha Mkuu Stewart Hall, kuiongoza Azam FC kwenye michuano hiyo, kwa mara ya kwanza aliweza kuifikisha katika hatua ya 16 bora rekodi ambayo imeshindwa kufikiwa na kocha aliyekuja nyuma yake kwa miaka miwili iliyopita.
Hall hadi anafika hatua hiyo alifanikiwa kuitoa timu ya El Nasir ya Juba kwa jumla ya mabao 8-1 raundi ya awali, ikaitupa tena nje Barrack Young Controllers II ya Liberia kwa ushindi wa 2-1 kabla ya kutolewa na FAR Rabat ya Morocco (2-1).
Katika mchezo huo dhidi ya Wamorocco, Azam FC ingeweza kusonga mbele kama nahodha wake John Bocco ‘Adebayor’ angefunga penalti waliyoipata dakika za mwisho ambayo ingefanya matokeo kuwa 2-2 na kuvuka kwa faida ya mabao ya ugenini lakini aliikosa.
Hall amesema amepanga kuikifikisha mbele zaidi Azam FC kuizidi rekodi hiyo aliyoiacha na ana malengo makubwa aliyowekewa na Bodi ya Wakurugenzi ya timu hiyo ni kufika hatua ya makundi (robo fainali) ya michuano hiyo mwaka huu.
Source:
Azam FC ‘kazi kazi’ v Bidvest Wits kesho | The Official Website of Azam Football Club