The Official Azam FC Thread

The Official Azam FC Thread

inatakiwa ifike mahali mashabiki wa simba na yanga wakubali kwamba kwa sasa azam ni timu kubwa. zile zama za a two horse league kati ya simba na yanga na simba zimeisha
 
Aug 2, 2015
Dar-es-Salaam, Tanzania

CECAFA Kagame Cup 2015 Final Azam FC vs Gor Mahia



CECAFA: Gor Mahia yanyukwa na Azam 2-0 kwa fainali
https://www.youtube.com/watch?v=y8qMfU_lr0s


Mbele ya Mhe. Raila Odinga waziri mkuu wa zamani Kenya, Gavana Joho wa Mombasa pamoja na wabunge kadhaa wa Kenya kama Mh. Juneit na mashabiki wao wenye ngebe nyingi, timu ya Gor Mahia ilishindwa kutengua kitendawili cha kushindwa kunyakua kombe la CECAFA (Challenge Cup) kwa miaka 30 mfululizo ikiwa mara ya mwisho Gor Mahia kuwa bingwa ni mwaka 1985.

Timu changa ya Tanzania, Azam FC iliishinda Gor Mahia kwa bao 2 bila majibu na hivyo Azam FC kubeba ubingwa wa CECAFA Kagame Cup 2015.




Gor yalambishwa
https://www.youtube.com/watch?v=3O98SrDR6NM
 
Aug 4, 2015
Dar-es-Salaam, Tanzania

By ppkahemele

Stewart Hall: Azam FC bado sana, subirini kwenye Kombe Ngao ya Jamii na ligi

Baada ya Azam FC kuchukua ubingwa wa Kombe la Kagame bila kuruhusu goli hata moja kutinga kwenye nyavu zake. Kocha mkuu wa kikosi hicho, Muingereza Stewart John Hall (Mourinho) amesema, safu yake ya ulinzi imekuwa imara kwa sababu ndiko alianza nako na aliamini patampa mafanikio kwa sababu safu hiyo ni sawa na msingi wa nyumba.



Lakini amesisitiza kuwa bado hajapata soka analolitaka, soka la kutiririka na pasi za haraka haraka za vuvutia, hivyo basi anakwenda mafichoni kujipanga upya na atakaporudi timu itakuwa moto wa kuotea mbali.



Sambamba na kuboresha kikosi pia kwenye ushambuliaji anataka wachezaji wawe na makali na atakaporudi kwenye mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga wapenzi wa soka wategemee kitu kingine kipya na wanaodhani ni nguvu ya soda, wakae mkao wa kula.



Stewart alisema: "Timu ilikuwa imara kwenye ulinzi kwa sababu ndiko nilianza nako kutengeneza kama unavyojua, safu ya ulinzi kwenye timu naweza kuifananisha na msingi unapoanza kujenga nyumba, unapokosea kuanzia hapo kila kitu kinaharibika."



"Hivyo baada ya kukamilisha hili, sasa nakwenda kujiandaa na Yanga, huko nitaboresha pia safu nyingine ambazo zina mapungufu tukirudi, kila kitu kitakuwa safi,"alisema Stewart.



Azam FC imechukua Kombe hilo baada ya kushiriki mara mbili kwa nyakati tofauti, lakini imeweka historia tangu ianze mashindano haijaruhusu hata bao moja la kufungwa.



Safu yake ya ulinzi, iliyokuwa chini ya Waziri wa Ulinzi Serge Wawa, Aggrey Morris, Said Morrad, Gardiel Michael, Abdallah Kheri, Shomari Kapombe, Farid Mussa na Erasto Nyoni huku viongo Jean Baptiste Mugiraneza na Himid Mao wakicheza eneo la kiungo cha ulinzi. Stewart Hall anasisitiza, ulinzi huo ulifanywa na wachezaji wote 11 waliokuwa wanacheza kwenye timu.

Source: Stewart Hall; Azam FC bado sana, subirini kwenye ligi | The Official Website of Azam Football Club
 
Aug 8, 2015
Dar-es-Salaam, Tanzania

HOMA MECHI YA NGAO YA JAMII AZAM FC NA SIMBA SC ZAJICHIMBIA KAMBINI

WAKATI Yanga SC wanatarajiwa kuondoka kesho kwenda Mbeya kuweka kambi ya kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii, wapinzani wao, Azam FC nao watakwenda visiwani Zanzibar.
Azam FC ambao Jumapili iliyopita walitwaa ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame wametua Zanzibar leo kwa kambi ya wiki mbili.

Mechi ya Ngao ya Jamii itachezwa Agosti 22, 2015 ikiashiria kuwa Ligi kuu Vodacom ya Tanzania bara ipo mbioni kuanza katikati ya mwezi Septemba 2015.................. soma zaidi kwa kubofya linki hapo chini.

Source: HOMA YA MECHI YA NGAO, YANGA HAOOOO MBEYA, AZAM FC WAFUATA ‘KARAFUU' ZENJI | BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE
 
Aug 10, 2015
Dar-es-Salaam, Tanzania

TP MAZEMBE KUWEKA KAMBI CHAMAZI COMPLEX, KUJIANDAA NA MCHEZO WA KLABU BINGWA AFRIKA


TP%2BMazembe.jpg

Photo: team TP MAZEMBE Congo DRC

MABINGWA mara nne Afrika, Tout Puissant Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wanatarajiwa kuja kuweka kambi fupi Dar es Salaam kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Timu hiyo yenye Watanzania wawili, Mbwana Ally Samatta na Thomas Emmanuel Ulimwengu itakuwa na mchezo mgumu wa ugenini dhidi ya Al Hilal nchini Sudan Jumapili ya Agosti 23, mwaka huu na kuelekea mechi hiyo itakuja kuweka kambi Dar es Salaam.

Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE leo kwamba Mazembe wameomba kutumia Uwanja wa Azam FC kwa mazoezi.

“Wanataka kuja kutumia vifaa vyetu kwa maandalizi kwa maana ya Uwanja wa mazoezi na vitu vingine ikiwemo gym. Kimsingi tumewakubalia na kuna uwezekano pia tukacheza nao mchezo wa kirafiki,”amesema Kawemba.

Haijajulikana kama Mazembe itakuwa tayari kucheza mechi zaidi za kujipima na vigogo wa hapa Simba na Yanga ambao nao wangependa changamoto hiyo.

Ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Smouha ya Misri jana mjini Lubumbashi umeipandisha kileleni mwa Kundi A Mazembe Ligi ya Mabingwa Afrika.

Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Mazembe, bao pekee la TPM lilifungwa na Roger Assale dakika ya 53 na sasa mabingwa hao mara nne Afrika wanatimiza pointi nane baada ya kushinda mechi mbili na sare mbili.

Al Hilal inabaki na pointi zake tano baada ya juzi kufungwa 1-0 nyumbani na Moghreb Tetouan ya Morocco ambayo sasa nayo imefikisha pointi tano. Smouha ya Misri ina pointi tatu.

Source: TP MAZEMBE YAJA DAR KUCHEZA NA AZAM FC, SIMBA NA YANGA WAKITAKA… | BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE
 
Hongera sana chama langu kwa kunitoa kimasomaso jana dhidi ya mahasimu wetu mbeya city..
 
Hawa ndo wakimataifa siyo timu hata suti hazina wala viwanja hakuna zinajiita wakimataifa..sema timu tunayocheza nayo timu yetu ifanye kazi ya ziada
 
Bidvest Wits vs Azam FC
Bidvest Wits take on Azam FC in the first leg of the 1/16 round of the CAF Confederation Cup, on Saturday 12 March 2016. The Clever Boys will play host to the Tanzanian side Azam FC at the Bidvest Stadium. Kickoff is set for 18h00.
Source:
Bidvest Wits vs Azam FC
 
By ppkahemele on March 12, 2016

Azam FC ‘kazi kazi’ v Bidvest Wits

KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, ipo kamili kabisa kuingia vitani na kusaka matokeo bora katika mchezo huo muhimu wa kwanza wa raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Bidvest Wits utakaofanyika saa 1.00 usiku katika Uwanja wa Bidvest.

Huo ni mchezo wa kwanza kwa Azam FC kwenye michuano ya kimataifa iliyosimamiwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) mwaka huu, mara baada ya mechi hiyo watarudiana na timu hiyo wiki moja ijayo (Machi 20) kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam kuanzia saa 1.00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Kuelekea mchezo huo yafuatayo ni mambo muhimu kuhusu timu zote mbili na namna Azam FC ilivyojipanga vema kusaka ushindi wa ugenini dhidi ya Bidvest Wits inayojiita jina la utani la Clever Boys.

Hali ya hewa?

Azam FC tokea iwasili jijini Johannesburg imekutana na hali ya hewa ya baridi kiasi na mvua zinazonyesha, hivyo kikosi hicho kimejipanga vilivyo kukabiliana na hali ya hewa hiyo na kupata matokeo.

IMG_3917.JPG


Kama hiyo haitoshi timu hiyo imenunua viatu maalumu vya kukabiliana na Uwanja wa Bidvest pamoja na mvua kama itanyesha, yote hayo yamefanyika ili kuwaweka wachezaji katika mazingira mazuri ya kupata matokeo mazuri Allan Wanga: Nitawafunga Bidvest Wits | The Official Website of Azam Football Club .

Jambo kubwa na la kupendeza hali ya hewa ya hapa inafanana sana na ile waliyokutana nayo nchini Zambia walipokwenda kushiriki michuano maalumu ya timu nne (Zesco United, Zanaco FC na Chicken Inn) Ziara ya Zambia yaanza kuzaa matunda Azam FC | The Official Website of Azam Football Club na kutwaa ubingwa wa michuano hiyo, hivyo kambi hiyo ya jijini Ndola imeanza kuipa faida Azam FC.

AZAM FC TV - Ziara ya Azam FC Zambia Source: Azam Football Club youtube

“Tumejiandaa kupambana na hali ya hewa ya hapa kwa sababu ni tofauti sana, pia nyasi za uwanja tutakaotumia zimenyooka na ni za kijani na unaruhusu soka kuchezwa kwa haraka sana, vilevile hali ya hewa ni mvua, na katika kujipanga na mazingira yote hayo kila mchezaji anacho kiatu cha kukabiliana na hayo,” alisema Hall.



Rekodi ya Kocha Stewart Hall?

Hii itakuwa ni mara ya pili kwa Kocha Mkuu Stewart Hall, kuiongoza Azam FC kwenye michuano hiyo, kwa mara ya kwanza aliweza kuifikisha katika hatua ya 16 bora rekodi ambayo imeshindwa kufikiwa na kocha aliyekuja nyuma yake kwa miaka miwili iliyopita.

Hall hadi anafika hatua hiyo alifanikiwa kuitoa timu ya El Nasir ya Juba kwa jumla ya mabao 8-1 raundi ya awali, ikaitupa tena nje Barrack Young Controllers II ya Liberia kwa ushindi wa 2-1 kabla ya kutolewa na FAR Rabat ya Morocco (2-1).

Katika mchezo huo dhidi ya Wamorocco, Azam FC ingeweza kusonga mbele kama nahodha wake John Bocco ‘Adebayor’ angefunga penalti waliyoipata dakika za mwisho ambayo ingefanya matokeo kuwa 2-2 na kuvuka kwa faida ya mabao ya ugenini lakini aliikosa.

Hall amesema amepanga kuikifikisha mbele zaidi Azam FC kuizidi rekodi hiyo aliyoiacha na ana malengo makubwa aliyowekewa na Bodi ya Wakurugenzi ya timu hiyo ni kufika hatua ya makundi (robo fainali) ya michuano hiyo mwaka huu.

Source: Azam FC ‘kazi kazi’ v Bidvest Wits kesho | The Official Website of Azam Football Club
 
Back
Top Bottom