The Official Azam FC Thread

The Official Azam FC Thread

FT Polisi Moro 0 - 1 Azam FC Kipre Tchetche (KC 10)
 
in mbeya city
400904_474665162573845_1087781763_n.jpg

66177_474665239240504_601486867_n.jpg
 
hongereni kwa kipindi cha Azam tv, sasfi sana na mapinduzi yenu yatakuwa chachu kwetu kubadilika na mpira wa Tanzania kupaa

Bravo sana!!
 
[h=5]Azam FC inashuka kwenye uwanja wa Sokoine-Mbeya kukwaana na banyambala Tanzania Prisons kikosi kinachoanza ni
GK Mwadini Ally
FB Erasto Nyoni & Ibrahim Shikanda
CB Aggrey Morris & Said Moradi
MD Himid Mao, Jabir Aziz, Abdi Kassim & Salum Abubakar
ST John Bocco & Kipre Tchetche

Usiache kufuatilia matangazo ya mchezo huu kupitia Kiss FM
[/h]
 
hongereni kwa kipindi cha Azam tv, sasfi sana na mapinduzi yenu yatakuwa chachu kwetu kubadilika na mpira wa Tanzania kupaa

Bravo sana!!

mdogo mdogo tu tutafikia level za kina tp mazembe..
 
FT T Prisons 0 - 0 Azam FC

well done boys maana bado tuna akiba ya gemu moja safi sana...
 
Uamuzi mbovu wa mwamuzi wa kati na mshika kibendera leo umeipokonya ushindi Azam FC dhidi ya Tanzania Prisons baada ya mwamuzi kukataa magoli mawili ya Abdi Kassim Baby na penati ya wazi baada ya mchezaji Salum Abubakar kuangushwa ndani ya eneo la hatari

Goli la kwanza mwamuzi kulikataa ulikuwa ni mkwaju wa mbali wa Abdi Kassim ambao ulitinga nyavuni kabla ya kurudi uwanjani na mwamuli licha ya kuona kuwa lilikuwa ni goli bado akaamua kukataa

Baadaye Salum Abubakar Sureboy alifanyiwa madhambi ndani ya eneo la 18 na kwa mshangao wa wengi wakiwemo viongozi na wachezaji wa Prisons ambao walishashika vichwa, mwamuzi akapeta na mpira kuendelea

Zikiwa zimesalia dakika chache kabla ya mpira kumalizika, Azam FC ilipata adhabu ndogo na Abdi Kassim aliupiga mpira ule na kutinga ndani ya nyavu lakini kwa mara nyingine tena mwamuzi akakataa kwa madai kuwa kabla ya kufunga Abdi Kassim alikwa ameotea wakati Abdi alifunga kutokana na mpira wa adhabu ndogo.

Kutokana na hali hii mpambano kati ya Azam FC na Tanzania Prisons ulimalizika kwa sare ya 0-0

sosi:
Refarii aipoka Azam FC ushindi dhidi ya Tanzania Prisons | The Official Website of Azam Football Club
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading, width: 100%"]Rushwa yashika hatamu Ligi Kuu [/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Friday, 19 October 2012 10:42 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]

*Simba, Yanga, Azam zadaiwa kupanga matokeo
Mwandishi Wetu
KASHFA nyingine imezikumba klabu za Simba na Yanga zikidaiwa kuanzisha kampeni ya kutoa fedha kuhakikisha Azam haipati ubingwa msimu huu ambayo inaitwa 'kampeni didimiza Azam'.

Azam inaonekana kuwa tishio katika harakati za Simba na Yanga kuendelea kutawala soka ya Tanzania kwenye miaka ya karibuni.

Habari ambazo Mwananchi ilizipata zinadai kuwa viongozi wa Simba na Yanga walifanya kikao mwezi uliopita kwenye Hoteli ya Kempinski na kukubalina kwamba watahakikisha Azam haichukui ubingwa msimu huu.

Chanzo hicho kilidai kuwa viongozi hao walikubaliana kutumia mbinu zote kuhakikisha Azam haipati ubingwa, pia waliafikiana kutofanya michezo michafu katika michezo yao.

Mwananchi ilipomtafuta Katibu wa Simba, Evodius Mtawala kujibu tuhuma hizo alisema hana taarifa za kikao hicho cha pamoja na kwamba ndiyo kwanza anazisikia habari hizo.

"Sijawahi kusikia kikao kama hicho ndiyo kwanza nasikia kutoka kwako, sijui lolote," alisema Mtawala.

Naye Katibu wa Yanga, Lawrence Mwalusako alisema, "Sielewi taarifa hizo kwani ni siasa ambazo nimekuwa nikizisikia kila wakati hivyo sishangazwi nazo zaidi ya kuangalia majukumu yangu ya kazi yanayonikabili."

"Hivi hizo habari mnazipata wapi? Kikao kama hicho ndiyo nakisikia kwako, hakuna taarifa hizo na wala sijasikia tuhuma kama hizo ambazo mimi naziita ni siasa za soka, acha timu zicheze, ni mapema sana kuanza kuzungumza mambo kama hayo ambayo mimi binafsi siyapi nafasi," alisema Mwalusako.

Hata hivyo chanzo chetu cha habari kilidai kuwa,"Kampeni hiyo imeingia dosari hivi karibuni baada ya viongozi wa Simba kudaiwa kutoa fedha kwa Kagera Sugar walipokuwa wanacheza na Yanga ili wawafunge."

"Tumebaini baada ya hapo viongozi wa Yanga nao wameapa kulipiza kisasa kwa Simba kwa kuhakikisha wanapitisha mikono yao kwa kila mechi watakayocheza ili wasiweze kutetea ubingwa wao," alisema kiongozi huyo aliyedai kuwa alishiriki katika kikao hicho ambaye ndiyo chanzo chetu cha habari hii.

Katika hatua nyingine chanzo hicho kilidai kuwa Azam katika kujihami imeingia katika mchezo mchafu wa kutoa fedha ili watwae ubingwa wa ligi baada ya msimu uliopita kuishia katika nafasi ya pili.

Yanga wanadaiwa walitoa ahadi ya Sh10 milioni kwa wachezaji wa Kagera Sugar kama wangeifunga Simba juzi, lakini kwa sare hiyo vijana wa Kagera walikabidhiwa Sh5 milioni huku Azam wakishutumiwa kutoa Sh7milioni kwa waamuzi wa mchezo huo ili kuwakandamiza Simba.

Akizungumzia tuhuma hizo, mratibu wa timu ya Azam, Patrick Kahemela alisema hawajawahi kutumia fedha ili kuharibu mechi ya Simba.

"Hatuna taarifa zozote juu ya kufanyiwa fitina hizo zaidi ya kuangalia malengo yetu ya kutwaa ubingwa kwa kucheza soka la uwanjani," alisema Kahemela.

Hivi karibuni Kocha wa Kagera Sugar, Abdallah Kibaden aliilamikia TFF kwa kushindwa kuchukua hatua ya kupambana na rushwa michezoni.

"Kutokana na baadhi ya waamuzi kuhongwa fedha na kupindisha sheria za soka, siku zote matokeo huwa mabaya na yasiyotarajiwa," alisema Kibaden.

sosi mwananchi
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
155168_470650229642005_1497072679_n.jpg




Azam FC leo inajitupa kwenye dimba lake la Chamazi kukwaana na moja ya timu bora kabisa VLP ya Ruvu Shooting Stars.
Mchezo wa leo ni muhimu sana kwa Azam FC kwani utaihakikishia uongozi wa ligi kuu huku ikiwa na mechi moja mkononi.
Kocha Mkuu wa Azam FC, Boris Bunjak amesema amekiandaa vema kikosi chake kwa ajili ya mchezo huo na anatarajia matokeo mazuri.
Kiungo Abdulhalim Humud ambaye aliumia kwenye mazoezi na kukosa mchezo uliopita anatarajia kurejea dimbani leo kusaidiana na wenzake.
Webmaster anaiombea dua Azam FC, "Mungu Ibariki Azam FC"
 
Back
Top Bottom