Lunyungu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2006
- 8,873
- 1,906
CHADEMA: Tunasisitiza CCM ilitumia rushwa
Edward Ibabila, MUC na Magreth Kinabo
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeendelea kushikilia msimamo wake kuwa, matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa 2005, hayakuwakilisha matakwa ya wapiga kura na kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kilitumia rushwa kwenye uchaguzi huo.
Msimamo huo upo kwenye taarifa ya chama hicho iliyotolewa jana kwenye vyombo vya habari na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa chama hicho, Erasto Tumbo.
Taarifa hiyo inasema, CHADEMA inashangazwa na kauli iliyotolewa na Katibu Mwenezi wa CCM, hivi karibuni, ya kupinga ukweli huo uliowekwa hadharani na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, baada ya kumaliza awamu ya kwanza ya ziara yake ya kuwashukuru wananchi.
Ni kweli kwamba CCM ilitoa rushwa katika uchaguzi na hili hata wakati wa kampeni CHADEMA tulilipinga, rushwa hii ilikuwa ni bidhaa mbalimbali kama khanga, sukari na maeneo mengine hata fedha taslimu. CCM ilijitetea wakati huo na kuiita ni takrima, mara baada ya uchaguzi Mahakama Kuu imethibitisha takrima ni rushwa, imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.
Inaeleza kuwa, hivi karibuni kwenye Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM, uliofanyika mjini Dodoma, Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete, aliwahimiza wanachama wa chama hicho kutojaribu kutumia rushwa kwenye uchaguzi wa chama hicho mwaka huu kwa sababu anawajua.
Tumekuwa mstari wa mbele kuweka wazi masuala ambayo yana mazingira ya rushwa ikiwemo mikataba yenye utata, hususan kwenye sekta ya nishati na madini. Tulimsaidia rais kwa kuweka kama agenda yetu ya msingi kuwa mikataba ipitiwe upya, lakini kinachoendelea ni tofauti.
Hata rais aliposema kwamba anawafahamu wala rushwa na anawapa muda wa kujirekebisha, tulimsaidia kwa kumueleza wazi kwamba rushwa ni kosa la jinai hivyo kama wapo hawapaswi kwa namna yoyote kupewa muda wa kujirekebisha, inaeleza taarifa hiyo.
Tunaendelea kuitikia mwito wa kushirikiana na chama tawala kukabiliana na rushwa, tunaitaka CCM na serikali yake ianzie kwa kuweka wazi kwa umma wamiliki wa Richmond ni hasara kiasi gani tumepata kama taifa na iundwe tume ya kuchunguza suala zima, ilisema.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa, Watanzania hawapaswi kuaminishwa kwamba suala la Richmond ni kitu kidogo, huu ni mkataba wa zaidi ya bilioni 260/-, fedha hizi zingeweza kugawiwa kwenye mikoa kama zile bilioni moja zilizotolewa na serikali kwa kila mkoa na kuendeleza wananchi.
Taarifa hiyo pia ilipinga taarifa zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa CHADEMA, ilianzishwa wakati wa ukoloni kwa malengo ya kuendeleza Wachagga (Chagga Development Manifesto CHADEMA).
Inaeleza taarifa hiyo kuwa chama hicho kilianzishwa na kusajiliwa mara baada ya Tanzania kuingia katika mfumo wa vyama vingi vya siasa na jina la chama hicho lilibuniwa na Simon Madete, ambaye ni Msukuma.
Awali CHADEMA tulipuuza uzushi huu, lakini kutokana na kauli hizi kurudiwarudiwa, tunaamini kuwa uongo na upotoshaji huu unaweza kugeuzwa na umma wa Watanzania ukaaminishwa kuwa ndio ukweli.
Safu za juu za uongozi wa kitaifa za CHADEMA zina viongozi sita, wenyeviti na makatatibu kati yao Mchagga ni mmoja tu ambaye ni Mwenyekiti wa chama Taifa, Mbowe, wengine ni Muiraq, Myao, Mpemba na Muunguja, ilisema taarifa hiyo.