The Only Thing We Have to Fear is Fear itself

Siku Bwana Mbowe akifanya hivyo, nahamia CHADEMA! Problem is, hana uwezo huo.

Is this a challenge?
 
Is this a challenge?

Ha ha ha! That's a good one there. No, that was sorta rhetorical. Seriously, I don't believe Mbowe can take up the Kyaruzi challenge to emulate Prof. Lipumba na kuongea mambo ya msingi na kwa kutumia statistics na kuacha mashairi ya kwamba ana uchungu na nchi kana kwamba wengine wote hatuna.
 
Kinyau

I do agree that Politicians use different means in covyeying their messages. But this one of Mbowe I find it to be rather more poetic than serious message to the public.
 


You Know what Mugongo Mugongo?

Najua kinachokuleta hapa sio forum wala kuchangia bali ni kwasababu MBOWE ame-register hapa. Na soon hapo kazini kwako waliopewa arlet kwamba mbowe karegister, wewe ndio ukajisajili UWONGO? na ukapewa kazi ya kudefend MBOWE & CHADEMA.

Najua bosi wako hapo kazini kwako ndio kazi alivyokupa kazi ya kuangalia watu wanasemaje kuhuku kuhusu Chadema na mbowe.

sasa usijifanye kwamba you cant help it. na usitake niseme unafanya unafanya kazi wapi, kwasababu unafanya kazi sehemu nyeti sana kwenye serikali yetu.
 
Habari leo.. kama Mugongo amewekwa hapa kufanya anayo fanya well and good.. wote tukiwa na mawazo yanayofanana pataboa... and NO we are not interested to find out anafanya kazi wapi na bosi wake ni nani... hoja zake tu ndio zinaangaliwa!!
 
Habari leo.. kama Mugongo amewekwa hapa kufanya anayo fanya well and good.. wote tukiwa na mawazo yanayofanana pataboa... and NO we are not interested to find out anafanya kazi wapi na bosi wake ni nani... hoja zake tu ndio zinaangaliwa!!

Habari Leo,

Na Masatu hapo naye katumwa na nani? Look, mambo ya kitoto ya kutishiana peleke huko kwenye forum uchwara. Hapa haangaliwi mtu sura. Zinaangaliwa hoja.

Mzee Mwanakijiji,

Hawa jamaa sasa ubabaishaji wao ndio unaonekana...manake wakizidiwa na hoja wanashindwa kuzijibu wanabakia kwenda kuangalia archives kuona mugongo amekuwa anaandika nini, mara wanatafuta mugongo anafanya kazi wapi, mara wanamuita mugongo tumbili, mara hivi, mara vile. Come on CHADEMA guys...deal na hoja iliyo mbele yenu. You have dominated this place for too long and you can't take it kwamba kuna different view points. I presented a simple challenge: what are Mbowe's alternatives to Kikwete's political program (export push, expansion of secondary and tertiary education, investment promotion, fight against HIV/AIDS, etc), and what are the intellectual, philosophical, ideological and political underpinnings of those alternatives? Mmeshindwa kujibu hilo suala la msingi, mmebakia kutafuta mugongo mugongo ni nani. But I can understand the shock and distress when a paradigm and set of beliefs are put to interrogation.

Bila majibu ya hili suala la msingi, kama alivyosema Masatu, Mbowe ataendelea tu kutuandikia mashairi kwenye tafakuri zake za kila wiki. But, I am sure anapata column kwasababu ni gazeti analolimiliki.
 

Well, I wish your line of argument was this one. But sadly it wasn't. I for one would have respected your contribution if you inclined your contribution towards our political parties' philosophical and ideological stances. But this is not what you are after (at least you have been). Your criticism about Mbowe has always centred on his personality rather than his political partiy's philosophical paradigm, with a clear aim of vilifying him as a politician. The best you have done in this forum is to correct grammatical errors here and there.

We will do a huge service to this forum if we can have a serious discussion around our political parties's ideological and policy directions. I am not sure if this is the right thread, though. Let us open a thread for this important topic.

Talking about our political leaders' intellectual capacity, and going by the power of argument demonstrated in the recent past general elections' race, certainly, Mbowe's intellectual prowess is unquestionable. There is no doubt also that, if communication skills remains to be one of the critical salient features of intellegince, our current president needs an urgent training session to bring him to the level deserving a president.

Ok, twende mbele turudi nyuma, wewe si ndio huyu huyu uliyesema Mbowe anaandikwa article zake na Ansbert Ngurumo. Leo unasema anaandika mashairi tena. Kwa wale wanaojua maana ya mashairi sidhani kama kuna mtu mwenye akili za elimu anayeweza kubeza mashairi kama njia ya kuwasilisha ujumbe. Tena kuandika mashairi yahitaji ustadi wa hali ya juu wa kuandika. Na sidhani kama Kikwete ana uwezo wa kuandika hata utenzi mmoja wa hayo unayoita mashairi.

Again, I am not impressed that you seem to fall in the same unfounded theory that you have always critisised; that to you every body who critises CCM government in this forum is a member of CHADEMA. Obviuosly, this simplicity is not eexpected of a person who claims to be discussing substance with an intellectual tone.
 

Mwanakijiji,
Ni kweli wote hatuwezi kuwa na mawazo ya aina moja. Ndipo hapo Mugongo mugongo alipotakiwa kujua hilo kabla ya kutaka Mbowe atoe hoja kama alivyotoa Lipumba. Anachooonyesha hapa ni chuki ya wazi dhidi ya Mbowe ambayo chanzo chake anajua yeye.
Kutaka Mbowe aje na alternatives kwa ajili ya HIV/AIDS umeambiwa Mbowe ndiye anayekusanya kodi za Watanzania?. Hata kama atakuja na hizo alternatives ni nani atamsikiliza kama anatoa maoni yake tayari vibaraka kama Mugongo Mgongo tayari wamesharukia na chuki zao?
Tuharibieni tu nchi ila iko siku kama siyo kizazi hiki basi kijacho, lazoma mlipe kwa ufisadi wenu.
 
MUGONGO x2 I wonder whether you are not on a personal mission to undermine Mbowe or as some surgested you are being paid to do so ; by who? well that is pretty obvious.Had Mbowe written this article under a pseudonym like yourself and myself would you have gone to the great lengths that to have to condemn the contents.And remember ,it was not meant to be a literary piece for the intelectuals like yourself to devour.Go easy mate ,appreciate the fact that all is not well at home; and something needs to be done about it. If not by the likes of you who have "faiedid" from this rotten system we call the Goverment,then by those who feel for the havenots. Dont forget Freeman was not brought up as a villager who moved into town and the next day wanted to own it by Hook or by Crook. Try and appreciate that he has given credit where credit is due and it hasnt been all damning.Thank God there arent to many fat Pi... like you who feel threatened by the truth.
 

Mugongo, nimeweka mada mpya ili kama unataka kuhoji mipango ya chadema kwa nchi iwe kule. Nimeweka vipande vya ilani yetu. Sasa wewe vipime na hali halisi ya nchi yetu ya sasa halafu useme kama Mbowe hana hoja.... Karibu kwa mjadala
 
Mugongo, nimeweka mada mpya ili kama unataka kuhoji mipango ya chadema kwa nchi iwe kule. Nimeweka vipande vya ilani yetu. Sasa wewe vipime na hali halisi ya nchi yetu ya sasa halafu useme kama Mbowe hana hoja.... Karibu kwa mjadala


Mipango? Sijui kama atachangia huko; ngoja tuone!
 

Chanzo: http://www.freemedia.co.tz/daima/2007/4/11/makala1.php
 
Waraka wa nne wa Mbowe kwa Rais Kikwete

Freeman Mbowe
MHESHIMIWA rais;

Leo naendelea na wajibu wangu kwako na nchi yangu, nikiwa katika hali ya kuchanganyikiwa. Yananichanganya mengi, lakini niruhusu leo nichepuke kidogo nje ya hotuba yako ya Desemba 30, 2005 nizungumzie japo kwa ufupi mawili yaliyojiri hivi karibuni.

Kama kuna kikwazo kikubwa kwa taifa letu, basi haya mawili ni sehemu muhimu isiyohitaji kufumbiwa macho kwa njia yoyote. Naam, mambo haya ni uhuru na wajibu wa Bunge na hatma ya elimu ya juu nchini mwetu.

Namwomba Mwenyezi Mungu aendelee kuniwezesha kuwa mtii kwa nchi yangu. Anipe ujasiri wa kuheshimu viongozi wanaojali watu wao. Kama sehemu ya utii huu, kila siku nikijadili jambo linalohusu taifa letu, kila inapobidi, sitaacha kukukumbusha ulichokisema. Taifa hili likifanya masihara, likabweteka na kughilibiwa na kauli zako zisizotafsiriwa kwa matendo, hakika litageuka taifa la “kondoo” ambalo nalikataa kwa unyonge wangu wote! Sitazua! Nitajadili ulichosema! Ndiyo msingi na nguzo ya tafakuri zangu.

Nitakusaidia kwa kukumbusha kila kauli uliyoitoa, bila kuchoka hadi hapo utakapoamua kunifunga mdomo; ama kwa mamlaka yako ama kwa kutekeleza kauli zako kwa vitendo.

Mheshimiwa rais;

Wakati unafungua jengo jipya la Bunge kule Dodoma, Juni 12, 2006, kama kawaida yako ulitoa hotuba yenye sura mbili. Sura ya kwanza, ilikuwa ni hotuba iliyoonekana kujaa nia njema na kutoa matumaini kuwa serikali yako itaheshimu uhuru na nafasi ya Bunge katika kujenga taifa letu.

Sura ya pili, inayojengeka kutokana na ushahidi wa kimazingira, inahoji ni nini kinasababisha kauli zako zisishabihiane na nia unayojaribu kuijenga kwetu wananchi wako.

Hapa chini nanukuu sentensi chache kwenye hotuba yako.

“Mheshimiwa Spika; Ukumbi huu utawawezesha waheshimiwa wabunge wetu kupata huduma bora na hivyo kufanya shughuli za uwakilishi kwa ufanisi wa kiwango cha juu. Ni ukumbi wenye hadhi ya kimataifa unaowapa wabunge vionjo vya Bunge katika karne ya 21.

“… Sina shaka akilini mwangu kuwa, kwa hakika jengo hili litabadilisha namna tunavyofanya kazi ikiwa ni pamoja na mienendo na mitazamo yetu kuhusu vikao na maamuzi ya Bunge.

“… Bila ya shaka kwa kuutumia kwa ukamilifu ukumbi huu wa Bunge… sauti za Watanzania zitasikika bila mikwaruzo. Aidha, matakwa na matarajio yao yatawasilishwa, kujadiliwa, kufanyiwa kazi na kupatiwa majibu kwa ufanisi zaidi sasa.

“Mheshimiwa Spika; Serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa Bunge, kama mhimili huru wa utawala wa nchi yetu. …Nawaahidi ushirikiano wangu binafsi na wa wenzangu wote serikalini.”

Mheshimiwa rais;

Hilo ni wakati huo. Lipo hili la majuzi. Wakati ukiwahutubia wanafunzi kutoka vyuo vikuu mbalimbali siku ya Februari 3 katika ukumbi wa Diamond Jubilee. Ulisema maneno yafuatayo:

“Tupeni muda suala hili tunalishughulikia haraka na kwa muda mfupi mtapewa majibu, lengo ni wale wote waliofaulu waweze kujiunga na masomo na si kuacha kwa vile wazazi wao hawana uwezo wa kuwalipia ada.” Mwisho wa kunukuu.

Mheshimiwa rais;

Si siri, serikali yako inadharau Bunge. Serikali yako inadhalilisha Bunge. Serikali yako, inatumia kila mbinu kulificha Bunge ukweli wa ufisadi ndani ya serikali yako na zile zilizokutangulia. Wasaidizi wako - nina hakika kwa baraka zako - wanawafunga wabunge midomo. Wanazuia mijadala.

Kama mnaamini Watanzania watasahau, mnajidanganya. Tunazidi kukusanya takwimu na muda unavyokwenda bila majibu, ndivyo mshindo utakavyokuwa mkuu. Kwa mema yote mnayoyafanya tunawapongeza, lakini hayatatufunga midomo kusema na kuhoji mpaka kieleweke!

Ahadi yako kuwa jengo jipya litabadilisha utendaji wa Bunge ni dhahiri kuwa haikuwa ahadi ya kweli. Kwa kuzingatia mengi mnayowazuia wabunge kujadili, ni dhahiri ahadi yako kuwa, utawasaidia wabunge kutekeleza wajibu wao kwa kulifanya Bunge kuwa huru, haikuwa ya kweli.

Mheshimiwa rais;

Kero kubwa za wananchi bado zinaendelea kuwa siri ndani ya serikali yako. Waziri mkuu wako anaendelea kwa kasi kulidhibiti Bunge na kukingia kifua ubadhirifu ndani ya serikali yako. Unayaona, unayajua, unakaa kimya, unayabariki. Ni wewe unayemtuma? Kwa nini tusiamini wewe ni sehemu ya ufisadi huu?

Chuo kikuu leo kimefungwa. Ahadi zako hazijatekelezwa. Hakuna maelezo yeyote ya mtu mwingine yeyote yataeleweka. Tunasubiri kauli yako. Pengine fikra zako umeelekeza kwenye chuo kipya Dodoma! Cha nini kama kilichopo tumeshindwa kukiendesha?

Wanafunzi leo wamefukuzwa chuoni! Nani kasema kufukuza kila kukicha ndiyo ufumbuzi wa elimu ya juu nchini? Haya ni majibu ya sera mbovu za elimu ya juu. Ninyi mtumbue, mfuje matrilioni halafu mfukuze maelfu ya watoto masikini. Nikisema rais alidanganya watoto masikini na wazazi wao nitakosea?

Bado mnacheza na elimu ya juu. Serikali yako ni serikali ya anasa. Naam, ni serikali ombaomba. Mnaomba, mkipata mnatumia bila kuheshimu bajeti. Kila siku makusanyo ya kodi yanavyoongezeka, ndivyo matumizi ya uendeshaji serikali yanavyoongezeka.

Taifa linakusubiri utoe kauli inayoeleweka kuhusu shilingi trilioni moja (bilioni 978) ambazo serikali yako imezifuja nje ya bajeti bila maelezo ya kutosha na bila yeyote kuchukuliwa hatua.

Mheshimiwa rais;

Kwani nani kawaambia wewe na mtandao wako mmemilikishwa nchi hii muichezee, muitumie na muiongoze mnavyojisikia? Nini maana ya wabunge kushinda miezi kadhaa bungeni wakitumia mabilioni ya fedha kujadili na kupitisha bajeti, kisha ninyi mtumie bila kujali?

Sawa sheria ya rushwa imepitishwa. Ofisi yako (Ikulu) imeng’ang’ania usimamizi wake. Pamoja na kilio na hofu ya wadau, yaani wananchi, kwamba Ikulu ni kinara wa rushwa, hivyo asisimamie TAKURU, mmegoma. Nina hakika mmejadili na kuweka msimamo. Nia njema iko wapi? Unaogopa nini wewe na wenzio kama mko safi?

Wewe kama rais, umetoa kauli nyingi tangu uchukue dhamana ya kuliongoza taifa letu. Kauli zako hizi, ulizozitoa maeneo mbalimbali na katika mazingira mbalimbali, kwetu wananchi wako zinawakilisha ahadi yako kwetu.

Ni wajibu wetu kuzihuisha na hotuba yako ya kufungua Bunge. Ya ufunguzi ilikuwa dira yako kwa taifa na zinazofuatia zote, tunazitegemea si zitoe ahadi na dira tena, bali zijikite kwenye utekelezaji wa dira yako ya Dodoma ambayo kwetu ni ahadi.

Mheshimiwa rais;

Woga wangu ni kuwa, taifa hili linaanza kuamini kauli za rais ni usanii. Ni uzushi. Ni danganya toto. Ni funika kombe mwanaharamu apite. Ni ubabaishaji. Rais anazungumza asichoelewa, asichokijua, asichoamini!

Kama sivyo, basi ni kuwa rais wetu ni dhaifu; na wasaidizi wake wanamwona hivyo. Na wao ni dhaifu, pengine zaidi. Ni kwamba rais ana ubia na watu katika utawala wake, na hana kauli ya mwisho.

Sifa zote hizi si sifa nzuri. Sisi watiifu kwa nchi yetu na kwako tunakueleza, kwani tunajua hao unaojaribu kuwakingia kifua ndio hao hao wanaotumia fursa hiyo kuonyesha udhaifu wako. Nchi hii haijapata kupata kiongozi wa sifa mbaya kama hizi.

Kiongozi mwongo, asiyeaminika hakika ni sifa mbaya isiyo na kifani. Ukimya wako si ushindi, ni uthibitisho wa hofu hiyo. Kataa sifa hiyo. Mtandao wako hauwezi kukusaidia kwenye hili. Onyesha kwa vitendo kuwa kweli huna ubia na wanamtandao, bali una ubia na wananchi wako.

Mheshimiwa rais;

Yako mengi yanafukuta. Kumbuka hakuna siri ya watu wawili. Punde yatawekwa hadharani. Watanzania wanajua Richmond tu! Mbona Richmond ni cha mtoto! Yako mengi, mazito! Kama huyajui, tutakusaidia kuyajua.

Kupenda sana kusema maneno ya kufurahisha watu wako hata kama hukusudii kuyatekeleza, kutakuponza na kukuvunjia heshima. Kutaliangamiza taifa letu.

Nakushukuru kwa kunisoma. Wiki ijayo nitaendeleza utii huu kwa kurejea hotuba yako ya dira yako kwa taifa!

Mheshimiwa rais;

Naomba kutoa hoja

freeman@chadema.net
 
Kuna wanaolitakia mema taifa letu, na wanaotaka kuendeleza hali iliyopo ya kutapanya mali ya taifa na kutawala kwa ulaghai. Mabadiliko ya kweli itabidi yaondoe mfumo uliojijenga siku nyingi, ndani ya CCM, wa kulindana.

Ili taifa letu lisizidi kudidimia, itabidi CCM ikae benchi (upinzani) kwa kipindi fulani. Hakuna uwezekano wa kukarabati serikali a CCM ikawa nzuri. It is unserviceable. Angalia jinsi ndugu zetu wa Kenya walivyoweza kuanzisha vita vya ya kweli dhidi ya rushwa baada ya kuiweka KANU benchi.

Kura huru na haki haiwezekani chini ya mfumo uliopo sasa. Ni mfumo wa CCM ambao unairuhusu kuiba kura. Kila mwenye ufahamu anajua CCM inaiba kura. Wakenya waliweza kuizui KANU kuiba kura kwenye uchaguzi uliopita. Inawezekana hata kwetu kufanya hivyo.

Kama Mheshimiwa Mbowe na wapinzani wenzake wanataka kweli kuisaidia Tanzania, basi waelekeze nguvu zao kwenye kuleta mfumo wa uchaguzi usioruhusu wizi wa kura. Kumwambia JK ajisahihishe ni vema, lakini hatajisahihisha. Hawezi kuacha kudanganya. He is a compulsive liar.

Ndugu Mbowe, jiulize iliwezekanaje ukapata kura chache hivyo baada ya kampeni nzuri vile. Ziliibiwa kura zako. Kazania kubadilisha mfumo wa uchaguzi Tanzania.

Augustine Moshi
 
Moshi Lamwai na CCM yao wameanza kuwashitaki ama kutishia wanao sema tofauti na magazeti waliyo yanunua . Na wewe ni Mchaga unaweza kuondolewa haki ya Utanzania wakasema wewe ni Mkikuyu wa Kenya kaa unasema haya . Mbowe kasema kaambiwa anamkukana Rais lakini yeye anarudia speeches za Rais . Magazeti sasa hatima yao haijulikani . Utawala wa aliyesema yuko tayari kukosolewa na kwamba tofauti ya mawazo ni ruksa sasa kaja na sheria ya kuivibana vyombo vya habari na mtandao kununua magazeti yote kasoro machache yaliyo bakia yenye akili timamu .
 
nimeipitia hii makala ya mh mbowe sijaona tusi...labda kama ni kweli rais hakuahidi kutatua tatizo la wanafunzi kwa muda mfupi,NA PIA AKAAHIDI USHIRIKIANO NA BUNGE[hasa kuwapa uhuru wa mijadala]..sasa kama hakutatua AITWEJE? tusaidiane kutafuta msamiati au tuseme HAKUSEMA...au tuseme muda mfupi ni MIAKA MITANO
 
Augustine Moshi heshima yako mzee.

My friend if NARC ousting KANU is the best model of war against corruption then , I am sorry we have a long way to go. We would rather stick with what we have. From experience I have had some time in the opposition parties in Tanzania. It is a sad story, it is merely a haven of dissappointed former CCMs with axes to grind. The most unfortunate thing ni kuwa CCM na hawa viongozi wa Upinzani ni watu wale wale wanafahiana in and out. Wengi wa viongozi wa Upinzani walikuwa kwenye parastatal organizations wakaziua. Leo wanijidai ni reinvented thinkers wa jamii yetu. MMMH!!! Kazi ipo.
 
Hali ikiendelea hivi tusikubali 2010 kuwarudisha Madarakani watu wa aina hii.Jipangeni wenye nia njema ili mueleweke nini mnataka kufanya kisichokuwa kile kinachofanywa na viongozi wa aina tuliyonayo sasa.
 

Ndugu yangu usikatishe watu tamaa bwana. Tuache ku-make blanket statements. Unaweza kutueleza kidogo ni kwa vipi viongozi wa CCM na upinzani "wanafahamiana in and out"? Vilevile, unaweza kututajia ni viongozi gani hao wa upinzani walioua parastatal organisations?
 

Moshi: you may have said these words with a light touch, but I tell you, your message is stronger than it may appear here. I wish many people in our country could acqure this way of looking at things!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…