The Only Thing We Have to Fear is Fear itself

The Only Thing We Have to Fear is Fear itself

Mwanasiasa,

I am dead serious. KANU kukaa benchi kumeifaidi sana Kenya, na hata KANU yenyewe. CCM iliyopo upinzani itajikarabati na kujijengea maadili mema tena. Wako wadanganyifu wanaopita huku na huko wakisema wapinzani wakitawala kutakuwa na vurugu. Kufanikiwa kwa serikali ya upinzani Kenya kunatoa ushahidi wa nguvu kwamba si kweli.

Haiwezekani kuleta mfumo mzuri wa utwala wa kisheria na usioendekeza rushwa bila kuiweka CCM benchi kwa kipindi fulani. We need a new beginning, but we cannot have it without consigning CCM to the ranks of the opposition first.

Augustine Moshi
 
Tatizo la Tanzania na nchi nyingi za kiafrika ni kuwa zilikuwa chini ya chama kimoja kilichojichimbia mizizi yote ya madaraka, influence, mali na uwozo. Halafu ghafla baada ya mwisho wa Cold war, wakakurupuka na kusema basi ukitaka kuanzisha chama chako ruksa. Wakafanya hivyo wakati chama kongwe bado kiko madarakani na raslimali zote kilichopata chini ya mfumo wa chama kimoja; mbaya zaidi ni kuwa yote hayo yaliendelea kufanyika chini ya katiba ile ile ya zamani.

Kwa hiyo, pamoja na uwozo wa upinzani, Mwalimu Moshi yuko right kusema kuwa hatuwezi kutengua mfumo mbovu wa utawala ulioletwa na CCM wakati CCM yenyewe bado iko madarakani. Ni lazima kwanza CCM iondolewe madarakani ndipo nchi nzima ianze mfumo mpya ambao hata walioko madarakani watakuwa wanaogopa mfumo wa utawala; hawa wa CCM sasa hivi hawaogopi lolote kwa vile wanachukulia kama nchi hii ni yao na mfumo wa utawala wanaweza kuupindisha kama wapendavyo bila kuwa na wasiwasi wowote. Ndiyo maana mCCM akisaini mkataba bomu anahamishwa idara "kuimarisha utendaji wa serikali," na mCCM akigundulika ana cheti cha elimu cha uwongo anaachwa madarakani bila kuulizwa kwa vile "cheti hicho hakitakiwi kwenye madaraka yake," na mCCM akisema uwongo bungeni "spika anatumia busara zake" kumsevu.

Ni Lazima CCM itolewe madarakani kwanza ndipo tuanze kujenga mfumo mpya. Inawezekana kuwa kutakuwa na matatizo katika kuanza mfumo mpya huo but it will be "a nacessary bitter pill"
 
Kwa hiyo, pamoja na uwozo wa upinzani, Mwalimu Moshi yuko right kusema kuwa hatuwezi kutengua mfumo mbovu wa utawala ulioletwa na CCM wakati CCM yenyewe bado iko madarakani. Ni lazima kwanza CCM iondolewe madarakani ndipo nchi nzima ianze mfumo mpya ambao hata walioko madarakani watakuwa wanaogopa mfumo wa utawala; hawa wa CCM sasa hivi hawaogopi lolote kwa vile wanachukulia kama nchi hii ni yao na mfumo wa utawala wanaweza kuupindisha kama wapendavyo bila kuwa na wasiwasi wowote.
Ni Lazima CCM itolewe madarakani kwanza ndipo tuanze kujenga mfumo mpya. Inawezekana kuwa kutakuwa na matatizo katika kuanza mfumo mpya huo but it will be "a nacessary bitter pill"

Maneno mazito sana haya ndugu yangu Kichuguu. Hata hivyo, nina shida kidogo na "blanket statements" katika submission yako. Je, unaweza kufafanua kidogo hoja yako kuhusu uwozo wa upinzani? We have very been specific about CCM woes; I think we need to do the same when it comes to the opposition parties. Otherwise, I think we are doing injustice to the opposition by making such bold but unsubstantiated statements!
 
Mwanasiasa,

Hali yako mkuu!...
Pamoja na kwamba nimeyakuta maongezi haya katikati lakini naomba nichangie pale palipokuwa na mapungufu katika statement zote mbili hasa zile ambazo zimetolewa na ndugu yetu Freeman.

Kwanza kabisa, mawazo ya Mzee wangu Augustine Moshi ni mazuri sana isipokuwa tu kwamba ngoma hiyo ni nzito sana kwa nchi ambayo - The big four, bado wameshika madaraka makubwa kichama na ndani ya serikalini....
Haliwezekani kabisa mabadiliko ya kiutawala unless yatokee mapinduzi ya Kifikra ndani ya chama tawala kwanza kama ilivyotokea ndani ya nchi nyinginezo (China).
Freeman na wengine wote wapinzani wanafahamu ukweli wa swala hili na isitoshe kinachoshangaza zaidi ni kwamba wanaendelea kupiga ngoma ndogo zisizoweza kusikika chini ya mdundo wa CCM. Freeman anaelewa fika kwamba JK ni rais ambaye amewekwa kwa nguvu ya CCM - Progressive Thing tank ambao wanaamini kabisa kuwa maendeleo ya nchi yetu yatatokana na kuiuza nchi wakati huohuo kila mmoja akijaribu ku- grab mali inayoelea ktk vyumba vya meli inayozama -Tatanic...
Tatizo kubwa linalotukumba wachangiaji wengi ni pale tunaposhindwa kuitambua hali halisi. Ukweli ni kwamba Tanzania hakuna Mwanasiasa! ila wapo wana Mtukula, wafanya biashara ambao siasa ni moja ya mbinu inayotumika ktk kufikia malengo yao ya kiuchumi.
Kibaya kinachojitokeza zaidi ni pale watu kama Freeman wanapoendelea kupeleka salaam kwa JK hali wanafahamu mchezo mzima hauanzi kwa JK.. kwa maana nyingine JK ni kibaraka wa utawala wa MTUKULA - CCM. haiwezekani kabisa Tanzania kuwa na wanasiasa wenye malengo mazuri ikiwa haohao wanasiasa ndio wafanya biashara wakubwa nchini. Haiwezekani viongozi na wabunge nchini kutunga sheria zenye malengo mazuri ikiwa wao ndio wafanya biashara wakubwa nchini!... Hizi sheria kweli zitamsimamia nani ikiwa wao wataanza kuzifikiria nafsi zao zimesimama wapi ndani ya biashara zao.
Kwa hiyo basi hata kama CCM watasimama nje kwa miaka mitano ya mwanzo, kitakacho tokea zaidi ni kubadilisha utajiri na umilikaji wa biashara hizo, yaani vita ya siasa za mtukula.
Baada ya kukaa Tanzania kwa muda wa mwezi mzima nimegundua kwamba nchi yetu ipo for a grab!... Haiwezekani kabisa nchi kutokuwa na sheria pamoja na standard zake baada ya kukubali kuwa na mfumo wa soko huria.
Ikiwa sisi tunawekewa sheria na standard ktk mali zetu tunazosafirisha nje inakuwaje sisi tuwe hatuna sheria ama standard kwa mali zinazoingia nchini?..Inakuwaje leo ukiwa madarakani (CCM) ndio nafasi pekee ya mtu kuruka viunzi vyote vya kisheria ambavyo vinahusiana na biashara za ndani na za kimataifa!...Jamani lini kesi ya ngedele unamkabidhi nyani ukiwa na lengo la kuhifadhi mazao yetu!.
Je, hivi kweli kutakuwepo na mabadiliko yoyote ikiwa CCM watakuwa hali Katiba ya nchi inawapa nguvu zote watawala ktk kutafuta Utajiri!...
tanzania leo hii inasema serikali haifanyi biashara hali viongozi wote wa serikali ndio wafanya biashara wakubwa!.. hapa kimebadilika kitu gani hasa kama sii ku transfer wealth kutoka mikono ya serikali na kuwapa viongozi wenye tamaa. Kabla hata hatujatazama accountability na mengineyo bora kwanza tukubali makosa makubwa yaliyotangulia.
Nitarudia kusema ya kwamba ile dhana yangu kuhusu UHURU wa mwafrika, huo ndio ukweli uliosimama! ukweli ambao wengi wetu tunashindwa kuukubali ama tumeufumbia macho kwa sababu ambazo nashindwa kabisa kuzielewa.
Ni kweli kabisa kuwa:-
1. Kiutawala:- Dhumuni hasa la Uhuru wa mwafrika lilikuwa kumwondoa mtawala mlowezi - ngozi nyeupe na badala yake kumweka mzawa tukitumia falsafa na itikadi zinazofanana na nguvu ya milki ya mkoloni.
2. Kiuchumi:- Tegemeo la viongozi wetu, Uhuru ni mfumo wa kubadilisha mkono wa mtawala wa uchumi toka mlowezi ngozi nyeupe na badala yake kushikwa na mzawa pasipo bila kujali malengo ya kumkomboa mwananchi kiuchumi na wananchi wote tulitegemea kwamba zimwi likujualo halikuli likakwisha!..Kumbe viongozi weusi ni mbwa mwitu aliyevaa ngozi ya kondoo.

Tukikubali ukweli huo basi hii ni hatua ya kwanza muhimu sana ktk utunzi wa katiba, sheria na malengo ya taifa jipya la Kibongo.
 
Mkandara: ni hatari sana kuamini katika nchi ile hatuna tena watu wenye nia nzuri na uwezo; hiyo tutakuwa tunakosea na kujikatia tamaa. Watu wazuri siku zote wapo. Tatizo ni pale wapiga kura tunaposhindwa kuwagundua hao watu wazuri na.

Kwa maoni yako, ni kama vile sasa tuwalete wakoloni tena au? Hapana. No. Kuna watu wazuri tu pale. Kinachotakiwa ni kubadilisha system. Madereva wamejaa tele, tatizo ni gari. Tukibadilisha gari safari yetu tutakwenda vizuri.

Wewe naona urudi haraka sana huku ughaibuni maana unavyozidi kukaa huko ndio unazidi kuchanganyikiwa na kukataa tamaa!
 
Well talented mwanasiasa!

I admire your vision mzee. Hebu one day ujitose rasmi basi kwenye ulingo. I believe you can mzee!

Keep it up
 
Mwanasiasa,

Ndugu yangu nimesha rudi na hayo niliyoyasema hapo juu ndio ukweli usiokubalika pamoja na kwamba ni UKWELI mtupu...Truth from facts!
Hii ndiyo hali halisi ya Tanzania pamoja na kwamba madai yako kuwa wapo viongozi wazuri.

Nafikiri unachoshindwa kuelewa ni kuwa sikusema hakuna viongozi ama watu wazuri isipokuwa nilichoisema mimi ni kwamba hakuna Wanasiasa nchini.
Mwanasiasa ni yule ambaye ana nia na malengo mazuri kwa wananchi wake. malengo ambayo yanatanguliwa na sheria, haki na kutambua nini maana ya UHURU. leo hii Freeman na wengine wote ambao wanaweza kuwa viongozi wazuri lakini siasa zao zimejaa propaganda zaidi ya kukubali kwamba Tanzania ina tatizo kubwa la kimsingi nalo ni kuutambua kwanza UHURU wetu.
sasa kitakacho fuatia ni kitu gani ikiwa leo hii kila kiongozi ni mfanya biashara!... sijaona hata mwanmasiasa mmoja aki question mfumo huo ambao ndio chanzo cha utawala mbaya. Freeman akishika madaraka unadhani kweli ataacha kuangalia maslahi yake binafsi?.. hata kama ataweza kuvumbua mbinu za kuwatajirisha wananchi bado yeye ni binadamu mwenye tamaa kama walivyo wengine nan hiyo sheria inamruhusu kujikita ndani ya biashara binafsi. Sidhani kama Free na wenzake wote ni wapumbavu kiasi cha kuongoza nchi bila kujitajirisha wao kwanza. Na hawawezi kufanya hivyo bila kuweka sheria zinazowapa nafasi kujiendeleza wao. Cha ziada watakacho kifanya ni kutuachia kamba sisi wakati wao wakipanda juu lakini haiwezekani kabisa wao kubaki chini hali nchi haina sheria inayowafunga wao. nitakubali tu ikiwa viongozi wote nchini wakaruhusiwa kununua share ktk binashara ambazo zipo ktk soko letu lakini sio wao kuhodhi makampuni binafsi ktk nchi ambayo haina katiba,sheria wala malengo ya kitaifa.
 
Fikiraduni,
Shukrani muungwana ndio habari zenyewe pamoja na kwamba zinauma sanaa...

Nitaongezea tena kuwakumbusheni yale maandishi yangu ya awali kwa lugha ya kigeni maanake mauzauza yamezidi na hawa wanasiasa wetu.

There are no hard distinctions between what is real and what is unreal, nor between what is true and what is false. A thing is not necessarily either true or false; it can be both true and false.'
Most African brothers (leaders) thought Independence should furnish us with noble ends rather than means to an end! As to say independence to us is being handed over power and instruments of exploitation to indigenous so that they can forever trample over them.
I believe that these assertions still make sense and do still apply to the exploration of reality through my writings. So as a writer I stand by them but as a citizen I cannot. As a citizen I must ask myself: What is real and what is unreal?
After 40+ years of independence,
Africa has become worse than ever! Poverty has spread across the board like virus, Africa has produced a generation of selfish, close-minded, unscientific, illogical generation consumed with immoral.
At this point, I can't stop wondering whether we needed to be independent at all! 'cause - The most dangerous criminal may be the man gifted with reason, but with no morals. This is how we always define African leaders.

To my knowledge our struggle has been a drama and truth in drama is forever elusive. You never quite find it but the search for it is compulsive. The search is clearly what drives the endeavour. The search is your task. More often than not you stumble upon the truth in the dark, colliding with it or just glimpsing an image or a shape which seems to correspond to the truth, often without realizing that you have done so. But the real truth is that there never is any such thing as one truth to be found in dramatic event. There are many and in different faces. These truths challenge each other, recoil from each other, reflect each other, ignore each other, tease each other, and are blind to each other. Sometimes you feel you have the truth of a moment in your hand, and then it slips through your fingers and is lost.
Do I blame anyone? No!....No because most of us have a misconception of
Independence. We are prone to let our mental life become invaded by legions of half truths and propaganda instead of sift and weigh evidence, discern the true from false, real from unreal, and the facts from fiction…all this before we take correct measures.

A Special message from Mkandara... Quote my word!

 
Mkandara ni sawa kabisa kwamba wanasiasa kujihusisha na biashara ni tatizo. Lakini kinachonishangaza mimi ni kwa nini hasa utumie kigezo hiki pekee kufika hitimisho ulilofikia. Matatizo ya bongo ni mengi sana, hili ni mojawapo tu. Kuna yanayosemwa hadharani mengine yanasemwa lakini hayasikiki. Sasa kwa wanasiasa wa upinzani kutokusikika kuhusu hili haimanisha kwamba wanapendezwa au ndio kusema hawasemi pale mambo yanapoharibika. Wanasema sana, sema matatizo yetu ni lukuki mno. Sisemi kwamba we are perfect, lakini nakataa kauli za kuonesha kwamba sisi wote hamnazo.

Hebu rejea kwa mfano, nyaraka za Mbowe kwa Rais amesema mambo mengi. Wasikiliza Lipumba na Mbatia wamesema sana. Jana tu hawa wapinzani wamesema sana kuhusu mfumo wetu wa elimu ya juu na kufuzwa kwa vijana pale mlimani na hata wameamua kwenda mahakamani. Ndio tushambulie, lakini tutiane moyo pia pale panapofanyika kitu. Naogopa kama wote tutajikatia tamaa ile nchi itakuwa ndio bado. Matumaini ni japo la msingi sana katika kwenda mbele na kukataa tamaa ni mwanzo wa kushindwa vibaya. Tusifike huko.
 
Mwanasiasa,
nakubaliana na wewe kimsingi tu kwamba madai mengi yametokea. lakini huwezi kuweka madai ktk serikali ambayo nyote mnaikubali ktk mfumo wa kiutawala ikiwa ni pamoja na hili swala la Biashara. Mambo yote haya na lawama zote zimekuja jitokeza wakati huu wa mfumo huu wa Soko huria. Hiki ndicho chanzo cha maafa yote! - kutokubali hivyo ni kujidanganya!

Sasa tazama swala la shule zetu pamoja na ahadi zote walizotoa hapo awali utakuta wenye mashule ya private ni baadhi ya viongozi wetu wafanya biashara. Chuo kikuu kutoa masomo bure ni barden kwao kibiashara na wala sii ushindani mzuri! Sasa kitazamike kipi kwanza elimu kama biashara ama elimu kama huduma, hapo tutakesha kwa lugha zote.
Point yangu kubwa ni chanzo cha yote haya. Vigumu kwetu kutambua nini habari ya kweli ama neno la Mungu ikiwa kila mtume atazungumza kutoa makosa ya mwenzake ktk mfumo wa imani wenye makosa.
Nitarudia kusema kwamba ikiwa nchi yetu haitaweza kuwa na mfumo ambao unawabana viongozi kujihusisha na biashara na kuhodhi makampuni itakuwa vigumu sana kuweza kuona mapungufu ya kiongozi yeyote yule. They are businessmen!
Na ukweli wa haya hauwezi kuwa ukweli ikiwa tutachukua ahadi za mtu kuwa kigezo cha uongozi bora. Hata hao mitume wetu wa dini zetu walifungwa na sheria ama aya ambazo zinawaka wao kuwa mitume bora kwa mifano kwanza kabla ya mafundisho yao. Leo hii tunachoona ni mitume wanaofundisha dini wakisema fuata ninayoyasema sii yale nayoyafanya. Hapa mzee wangu kuna utata wa kufahamu tamu ni ipi toka ktk chachu na wala tusiwalaumu zaidi viongozi wetu kwani sheria haiwafungi. Ikiwa biblia haikukataza kula nguruwe utasema vipi kula nguruwe ni haramu?... na nani atakaye kusikiliza wewe kama sio choice yako mwenyewe.
Huu ndio uongozi wa kiafrika mzee wangu tatizo kubwa ni Umaskini wa akili na mali. pale penye penyo za kujitajirisha sioni kabisa kuwa kutakuja kuwepo na kiongozi zaidi ya watawala. Hizi longalonga zote hazina mwanzo mzuri na hata kama wewe utakuja shika madaraka huwezi kabisa kuongoza nchi ikiwa mikono, macho yako na fikra zako hazikufungwa na sheria. Kwa sababu hakuna definition iliyopo ktk biashara inayosema kiongozi mzuri ni yule asiyetaka faida zaidi, utajiri zaidi na kutoka mshindi ktk mashindano ya biashara. Mwekeshaji yeyote ktk biashara yako huyo ni adui wako ktk biashara na mbinu zinazotumika ni kuhakikisha unamshinda mwenzako kibishara. Akifunga biashara yake hii ndio furaha yako!...
Huu ndio uongozi wa kiafrika na ndio maana tunapata taabu sana kusimamisha vyama vya upinzani!
 
Mkandara,
Wamarekani ni mabepari waliokubuhu. Lakini kuna wakati ilifika wakaamua kuwa huwezi kuhudumia mabwana wawili. Yaani kiongozi wa ngazi ya juu serikalini huwezi kuendelea na biashara zako. Hawa hawakuwa wajinga. Sasa sisi bongo leo tunatumia nafasi za uongozi wa serikali kuimarisha na kupanua biashara zetu. Katika hali hii maslahi ya wananchi ndiyo yatakayopunjika.
 
Mkandara,
Wamarekani ni mabepari waliokubuhu. Lakini kuna wakati ilifika wakaamua kuwa huwezi kuhudumia mabwana wawili. Yaani kiongozi wa ngazi ya juu serikalini huwezi kuendelea na biashara zako. Hawa hawakuwa wajinga. Sasa sisi bongo leo tunatumia nafasi za uongozi wa serikali kuimarisha na kupanua biashara zetu. Katika hali hii maslahi ya wananchi ndiyo yatakayopunjika.
Hivi ni viini macho hata Marekani hao viongozi wanpeeana tender!Lakini wenzetu angalau wanawajibika!
 
KNKCU
That is an important point. Wanawajibika. Sisi hata kuwajibika hakuna kabisa. Karamagi atavutia kwenye manufaa ya biashara zake. Lowassa atavutia Vodacom na Richmond hata kama maslahi ya nchi yanadhurika.
 
Kiongozi anapokaa na kufanya biashara za kitapeli kuwaibia walipa kodi ni fedheha. Chagueni moja kufanya biashara kihalali na kulipa kodi au kuongoza?
 
I told my colleagues kuanzia mwanzo kwamba hawa wanafunzi wa elimu ya juu wangeenda kuomba ufafanuzi wa madai yao mahakamani..well in advance wakiwa bado chuo kabla ya mgomo! Maana ni kweli hii sheria ya mikopo ilikiukwa! SASA ANGALIA Wanasiasa ndo wanataka kujitosa kwenda mahakamani kwa niaba yao! Again I say wengi wetu hatusomi alama za nyakati na kujifunza kutatua matatizo yetu wakati hayajawa makubwa! Its a shame kuona swala kama hili wanafunzi wanashindwa kujimobilize na kulishughulikia kisheria! I tell you, Mi bado nina imani na hii mahakama yetu ya TZ..Mtikila has shown the way!
 
Mikuki, kuna wakati ambao inabidi wananchi wenyewe wachukue sheria mkononi kwa sababu mahakama zetu zimeundwa kutokana na chama tawala na aslimia 90 ya mahakimu wetu ni wanachama wa chama tawala. Haya ndio mazao ya Ujamaa na kama nilivyosema toka awali kuwa Tanzania leo hii kila kitu ni Biashara!.. Hata mahakama yetu inatazama kwanza biashara ipo?... kisha sheria inafuata.
It was wrong kwa serikali kuwafungia wanafunzi na huyo Prof. Mukandala ni kibaraka wa baadhi ya watu ktk kundi la CCM, anatumiwa. Viijana wa chuo kikuu wameweza kwenda kumuona Lowassa ambaye aliwaahidi kuwaona na kufanya suluhisho kati yao na chuo. Lakini unajua kwamba taarifa hii alipopewa Mukandala aliwajibu wanafunzi anataka official letter toka kwa Lowassa, ili mradi tu kuonyesha ubavu wake.
 
Namuunga mkono Mukandala maana isije ikawa viongozi wakuu (JK, EL, Msolla) wanamchanganya kwa kumpa maagizo na kutoa kauli zinazokinzana kila wakati. Bora ashikilie hapo hapo ili ijulikane nani alichemka.
 
Mkandara I fully agree unayoyasema hapa! We all know the sytem is corrupt and devoid of good will kusaidia wanafunzi...lakini unafikiri hata kama Lowassa akitoa memo jamaa wakarudi shuleni unadhani watakuwa wamesolve tatizo? Harafu ujue Prof. Mkandala is a governemnt employee! solely accountable to the governemnt! Kwa hiyo yeye anatekeleza alichoambiwa! My point is, lets try..ile sheria iwe challenged... Hakuna sehemu inayosema kwamba anayepewa funding ni wa division one au two! Ni statement za wanasiasa! Tukikaa kimya...ndo hivyo tumehalalisha huo usemi na wote tunajua madhara yake..after all tumeshaanza kuyaona....!

Its sad but, mahakama ndo nyenzo tuliyokubaliana kwamba itatumika kutatua migogoro yetu! However its imperfections! Kama ile sheria ikiwa overhauled, basi jamaa watakuwa na ground ya kudeal na serikali WITH justifications But kwa sasa wanaahirisha matatizo..I tell you..Hicho chuo cha Dodoma kikifunguliwa wanafunzi watakaohitaji funding watakuwa wengi..sasa usishangae serikali ikajitoa kulipia wanafunzi tena bila notice na jamaa wataambiwa anayetaka kusoma aje chuo asiyetaka..aende home apumzike. Please lets not try to solve problems kwa sortcut..Hapa I smell fish, Tunaahirisha tatizo. Ukisema huna imani na hii mahakama, well hapo sina comment.....sasa sijui tutaenda wapi! Ila wanafunzi especially wa UD wajue siku hizi vyuo ni vingi.......WAJIZATITI KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA UTANDAWAZI...and they can only win when and only when they are smart.
 
Mikuki,
Nchi yetu inakwenda pabaya sana hasa pale fedha inaposhika nafasi kubwa ya maendeleo ya aina yeyote, hakuna wa kumsimamia mnyonge na tatizo kubwa ni kwamba hata hizo mahakama hupokea simu toka juu kuwaelekeza nini kifanyike. Mkuu fulani anaweza ahirisha kesi na mahakama isiwe na uwezo wa ku-question. Mara nyingi hukumu huwa zimepangwa nje ya korti.
Katika mtazamo wangu kila mara hujaribu kutafuta chanzo cha tatizo na nadhani, Tatizo kubwa la Vyuo vyetu ni pale serikali ilipoamua kuchanganya wanafunzi wa kulipia na wale walalahoi!..
Hii inashindwa kutafsirika vizuri kama elimu inayotolewa ni part ya biashara ama huduma! na ukisikia maelezo ya pande zote mbili hasa za wanafunzi utagundua kuwa wale wanaolipa wanaona maamuzi ya chuo ni sawa. Hakuna mtu anayependa kulipa hata kama wao hawakufanya vizuri huko nyuma.
 
Back
Top Bottom