Mwanamke huwa kama pasi huchelewa kupata joto na hutunza joto kwa muda zaidi hata baada ya kumaliza kupiga pasi. Kwa wengi wetu huwa inatokea either kusahau au kujifikiria wao wenyewe. Utakuta baba akirudi toka kazini na kumkuta mkewe nyumbani humsalimia na kwenda zake chumbani kubadilisha nguo za kazini.
After that anapata chakula cha usiku (Dinner) then anaanza kutazama TV au kupitia magazeti yake na kuyasoma.
Muda wa kulala umefika anaenda kuoga na kuvaa pajama zake; mke naye anaenda kuoga na kufanya sawa na mume. Wanapanda kitandani, mume anampapasa mke, mke naya anajua mzee anataka maana ndiyo sex code yake akinigusa kwa mtindo huu maana yake anataka tuwe mwili mmoja na anajisikia kama kusumbuliwa maana alikuwa hajui kama mzee atataka kutokana na
kutowasiliana hata hivyo anamkubalia.
Baada ya dakika chache wamemaliza, wapo kimya na mzee anapiga usingizi.
Mke anajiona kama
ametumiwa tu kwani hakukuwa na raha yoyote ni kuumizwa tu kwani
mwili haukuwa connected hisia.
Mwanaume ni rahisi kusisimka kimapenzi wakati
mwanamke huhitaji kusisimuliwa. Mwanaume husisimuliwa na moja ya mlango wake wa fahamu kupitia kuona (sight) wakati mwanamke husisimuliwa kupitia milango yote mitano ya fahamu Kuguswa, kusikia, kuona, kuonja, kunusa na wororo (tenderness) wa mwanaume. Mwanaume ni mfano wa bulb ya umeme uki-switch tu mara moja inawaka wakati mwanamke ni mfano wa pasi ya umeme ambayo huchukua muda hadi ipate joto na hutumia muda zaidi to cool off.
Hii ni muhimu sana ukitaka kuwa mpenzi mzuri na mpenzi mzuri hujua na kuzingatia jinsi ya kumridhisha mwenzake.
Mwanamke anaongozwa na highway ya emotions, atajisikia vizuri sana kama alikuwa na idea kwamba kutakuwa na kuwasha pasi yake ya umeme mapema.
Itakuwaje kama wakati wa kuondoka asubuhi mume akampa mke busu la uhakika na kumnongoneza mkewe kwamba vipi unaonaje leo usiku ukawasha pasi mapema kwani nina hamu sana kupiga pasi nguo kwani naona bulbu yangu ina mwanga wa uhakika leo".
Nahisi mke atashinda anaweza jinsi ya kuhakikisha pasi yake inawaka chapchap usiku na ikitokea na mchana akaambiwa neon linguine mwororo inaweza kuwa jioni yenye mwako wa mahaba.
Lakini kwa wengi wetu huwa ni kinyume na hayo na ndio maana wakati mwingine ukipapasa usiku unaambiwa baba nanii leo kichwa kinaniuma sana au nimechoka sana au unapata zero participation na kuambiwa maliza haraka au pasi inakuwa kavu kabisa matokeo yake ni pasi inagoma kuwaka na kuanza kuumizana.
Jifunze kuwa mwanaume mwororo (tenderness) wasiliana na mke, tafuta muda wa kumsikiliza, cheka naye, cheza naye, ongea naye, mpe mgusu (touch), mkumbatie na kumbusu hata kama si wakati wa sex ni wako na ni wewe uliamua kuishi naye.
Mwanaume humtengeneza mwanamake!
Source:
The Hill Of Wealth