ICRC alarmed by situation in Libya, says fears worse
Five months into a conflict that has embroiled NATO ..........
Health care and food supplies are deteriorating in Libya, but the Gaddafi government has managed to keep paying wages and food subsidies in areas under its control, the International Committee of the Red Cross (ICRC) said on Tuesday.
ICRC alarmed by situation in Libya, says fears worse | Top News | Reuters
Nimeipenda hii...ukweli mtupu...Mimi nashangaa hawa North Atlantic Treaty Organization or NATO wanafanyanini huku afrika nani amewapa majukumu huku. Kwani huku ni north atlantic. Huu ni ugaidi tuu unaoendelea dunia hii kwa baazi ya nchi kutumbua hela na kuendelea kuzipa kazi masilaha yao waliyotengeneza yasiingie kutu. Sasa angalia watu wangapi wameua huko kwa mtemi ghadafi. Simtetei lakini siyo mahali pa NATO kubomu bomu nchi za watuu tuu miaka nenda rudi alafu wanakuja kujenga baadaya na kukuingiza kwa madeni. Angalia hata mtemi ghadafi alikuwa hana madeni ya hawa walafi wa IMF na wold bank. Sasa wakimtoa hapo wataweka kibaraka wao na kupeleka madeni. Kinachonishangaza zaidi pia hawa magaidi (NATO) wanayo teknology ya kumkona gadafi mahali na kummaliza chakushangaza wanashuti tuu pembeni. Nikama mchezaji bora wa mpira wa miguu amepewa penati na goli lipo wazi bila kipa na kupiga mpira nje tuu au juu ya goli.
Good observation!-Gaddafi alipokuja madarakani 1966 Libya ilikuwa nchi ya mwisho katika orodha za maendeleo duniani (repoti ya UNDP)
Repoti ya UN ya mwaka 2010 ya vigezo vya maendeleo ya binadamu (human development index inayotazama urefu wa maisha ya watu, elimu , afya, ukaribu wa huduma, na ubora wa maisha) inaiweka Libya nafasi ya 53 baina ya nchi 193. Kwa maana hiyo iko juu ya nchi kama China, Mexico na Saudi Arabia.
-Walibya wanapewa elimu ya bure tangu kindergarten hadi university na kama umepasi vizuri hata elimu ya nje chee.
-Walibya wote wanaishi kwenye nyumba wanazozimiliki.
-Libya ndiyo yenye kiasi cha chini zaidi cha vifo vya watoto wachanga barani Afrika, hata kushinda Misri, Morocco, South Africaa, mauritius.
-Gaddafi hana benki akaunti nje, lakini Libya kama nchi ina akiba ya dola 100 BILIONI ambazo Wazungu kama kawaida zao wameziiba eti kwa kuwa Gaddafi hawakilishi Walibya tena!
-Gaddafi ameinvest dola bilion 20 kutengeneza mto mkubwa zaidi uliowahi kutengenezwa na binadamu yeyote duniani, hiyo kudhamini upatikanaji wa maji daima Libya.
- (Hata kama hujui) ukiwa Mwafrika barani Afrika, basi unafaidi dola bilioni 1 za Gaddafi kila mwaka ambazo analipia satellite za Bara zima la Afrika ili Waafrika wasiingie gharama hiyo. Hizi ndizo zinazokuletea TV, mawasiliano ya simu etc.
- Gaddafi ni rais pekee wa Kiarabu anayejivunia kuwa Mwafrika (hata huvaa nguo za Kiafrika wakati wetu huvaa tai katikati ya joto la Dar!)
-Gaddafi (wengi tunajua) ndiye aliyeshinikiza kuundwa AU. Infact, alikuwa anataka shirikisho la mara moja la Afrika nzima, lakini wakuu wenu, kwa kuwahofia waume zao na maslahi yao wakasema haiwezekani banaaaaaaaa!
-Gaddafi amefanya Walibya wote sawa, waume kwa wake, ingawaje kwa culture ya Kiarabu hilo ni tusi (mabodi guard wake)
-Ameikopesha karibuni Afrika yote (hata rais wako ana deni) tena kwa masharti nafuu. Wakati mwingi ameziokoa nchi nyingi za Afrika kwa kuwapa petroli ya bure, kuwajengea viwanja au mahall ya bure kwa mikutano ya Afrika. (Waasi hawatataka hata uhusiano na watu weusi)
UPANDE MWINGINE
Hawa wanaoitwa rebels wengi wao ni watu wenye background ya Alqaeda (bila shaka utajua watafanya nini.Al-Hasidi, mmoja wa wakuu wao, ndiye aliyekuwa Kuruta mkuu wa wanaokwenda kupigana Afghanistan bega kwa bega na Osama.
-Na ni kwa sababu ya background hiyo ndiyo ingawaje wanasema viongozi wa mapinduzi ni 31 lakini wanathubutu kutaja majina ya 13 tu wakihofia kuweka wazi wengine
-Abdul Jalil, mkuu wa rebels ndiye aliyetoa amri ya kuuawa mamia ya watu weusi, eti akiwatuhumu kuwa ni mamluki, lakini ukweli ni kuwa ataka kulipiza kisasi cha siasa za Gaddafi za kupendelea Afrika. Pia alipokuwa Waziri wa Sheria katika utawala wa Gaddafi alitoa amri ya kunyongwa kwa wauguuzi (nurses) watano wa Bulgaria kwa tuhuma za kuwaambukiza ukimwi watoto wa Libya (Gaddafi akawasamehe)
- Wanasaidiwa na Wazungu, na hata wakoloni wa Libya (Italy) eti hivi sasa ndio wakombozi!
-Wanajua hwawezi kushinda uchaguzi huru utakaosimamiwa na UN kama alivopendekeza Gaddafi, wakakataa. Njia pekee ya kufika madarakani kwa kundi hili ni kwa mtutu wa bunduki
KOSA KUBW LA GADDAFI:
Yasemekana ni dikteta asiyependa demokrasia. Pia, amekaa sana.