The rise and fall of Colonel Muamar Gadaffi

Kitufe cha Thanks sikioni hapa kwenye simu yangu...ila hata hapa nakutwangia THANKS MKUU.N/i heri kufa ukiwa umesimama kuliko kuishi ukiwa umepiga magoti...kama Kufa Muammal sio wa kwanza.Gaddafi wewe ni nguli na umeonyesha wazi kuwa huburuzwi.Acha hawa vibaraka wa wakoloni waendelee kujikuna kuna tu
 
Muislamu huyo wamtoe tu hana lolote.
Hata hapo Tanzania yupo Muislamu.Mbona unaishi gizani huku milo mitatu ikikushinda?Toa kwanza boriti lililopo kwenye jicho lako hilo lenye matongotongo kisha ndo uende ukatoe boriti kwenye jicho safi la mwenzio
 
katika uislamu dhambi ya unafiki imezungumziwa sana.
Leo hii viongozi wa nchi za kiafrika ambao walikuwa wanafededea misaada ya Gaddafi eti nao wako kimyaaaa...

Wamemuacha mzee wa watu anapigana huku akisaidiwa na waislamu wenzake na wanawe.

Marais waislamu mnaotawala baadhi ya nchi za kiafrika mko wapi muislam mwenzenu anashambuliwa na ile hali mmefundishwa kuwa waislamu wote ni ndugu?

huu ni mwezi shaaban na ujao ni ramadan.
Sasa ntawaona kama tende na madikodiko mengine mtayapata toka Los Angeles, au London au Milan au Paris
 
Ni vigumu kwa kiongozi yeyote duniani kufanya mema matupu. Hata Mandela hawezi kudai hilo. Cha muhimu ni kuchunguza yapi yamezidi mengine? Halafu, jee ni kwa nia gani amefanya hayo mabaya? Wakati mwingine kiongozi hufanya mabaya kwa nia njema kabisa, kama baadhi ya vitendo vya Mwalimu.
Kama unachunguza zaidi ulimwengu utaona hata kitu kibaya si kibaya wakati wote na kwa vigezo vyote. Sumu ya nyoka ni dawa ya magonjwa chungu nzima!
 
Baada ya Libya ..
Wataanza uchokozi na nani tena? ??

Naona wanafuta nchi ambazo ni
Matajiri wa mafuta...
 
kutokana na gharama za simu miaka ya 90 africa ilikuwa inailipa ulaya kwa kutumia settlite yao ya Intelsat dola 500 kwa mwaka,
gadafi aliamua kuinunulia africa setilite ili kuondokana na gharama kubwa inayoilipa ulaya kwa mwaka,
hayo mabomu tunayoyaona leo libya ni hasira za wazumgu kuwanyima dola 500 kwa mwaka!
 
Yaani ulaya waingie gharama zoote kwa dola 500???????????????
Dola 500 si unanunua suti ya bei chee?????????
 
Rosemarie, kwanza hongera kuanzisha thread ya mambo ya maana hata kama jukwaa silo.

Pili hoja ya satelite ni kweli, ila sio dola 500 kwa mwaka, ni dola 500 kwa mwaka, ni dola laki 5!, Yaani ni 500,000.

Ila sio hivyo tuu, ametaka kuanzisha muungano wa Africa, United States of Africa ili Afrika iwe na nguvu kuliko Marekani, alipanga kuanzisha Bank of Africa na African Monetary Fund ili bara Africa tusiyategemee haya mashirika makubwa ya fedha ambayo ni ya kibeberu.

Kufuatia mipango hiyo, Marekani na kimada wake Uingereza wakaamua Gadafi lazima aondoke!.

Its very sad Waafrika hatulioni hili na tunawaacha wafanye wanavyotaka!.
 
Reactions: BAK

Mbali na hilo, Gadaffi ni mshenzi anayetakiwa kufa au kufungwa maisha, unachosema ni sawa na kusema fisadi mmoja wa Tanzania kuiba na kuwapa kiduchu masikini au tuseme mtu abake mwanao alafu akupe pesa ya kula kwakuwa wewe ni masikini
 
gadafi ni gaidi dikteta na kila ukijuacho aliisuport Uganda chini ya Idd Amini ile vita dhidi yetu tz sasa utaona mwenyewe
 

mkuu pasco
dola laki tano
unalinganisha na gharama za kuendesha vita
wanazotumia nato???????

Hili la kuunganisha africa ni ndoto isiyowezekana
 

una uhakika mamito au umejisikia tu kuleta huu uzi? evidence plse!!!
 
USA na Uingereza inaweza kufanya biashara na yeyeto kokote pale kwa mapenzi ya mhusika au lulazimishwa. Gaddafi sio Tishio kabisa kwa mataifa haya. Gaddafi kauwa watu wake, kafanya ukatili, kakosea, ni mshenzi hahitaji kuhurumiwa. Mbona Mwenzake wa Misri alipoona nguvu ya umma imemzidia aliachia ngoma. Na jamaa wa Tunisia aliachia ngoma. Tusiwe wajinga kiasi hicho. Ndio maana mafisadi wamesababisha leo tupo gizani tunaogopa kuwafuata masaki na oysterbay kuwatoa ndani kwa visingizio kibao. Hakuna kijana mwenye akili timamu duniani anapenda umasikini tena wakuletea na watawala wajinga.

Wataondoka wengi sana karne hii na kizazi hiki bila kujali rangi wala geografia. Na umeme huu utamtoa ****** ikulu, tena wanavyowachokoza wamachinga suburia tu.
 
Rosemarie nakusifu kwa kuleta kitu kisichohusisha imani leo,mawazo yako ni mazuri ngoja nikusaidie kidogo,amount ni 5m dollars,na pia alilipa gharama za kutafiti uwezekano wa kuanzisha safaru moja,uendeshaji wa AU asilimia kubwa alikuwa analipa yeye,Libya ilikuwa moja ya nchi isiyodaiwa na mtu,kuna bilioni zaidi ya 150 Ulaya na Marekani za Libya kwenye mabenki na uwekezaji ambazo wanataka kuzipora kwa kisingizio cha capital freeze lakini hazirudi tena kama zile za Iraq,Mabutu na Abacha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…