The rise and fall of Colonel Muamar Gadaffi

Kumbukumbu zangu zinanionyesha kuwa Gaddafi alipambana sana Africa iungane (United State of Africa) but alikosa support from other African leaders.
 
Ulale pema ghadafi. Ulikuwa kati ya viongozi wachache wa africa wenye maono au wanaojua kwamba umoja wa afrika ndiyo njia PEKEE kwa ukombozi wetu.
 
Afrika inarudi kwa wennyewe "wazungu" na sisi wengine tunafurahia. Sasa tusubiri hilo "DOMOkrasia" waliloahidiwa wenzetu wa Libya.

Mkuu kama ulitegemea Gaddafi pekee asimame kuitetea Afrika wakati viongozi wengine wa Kiafrika wakimzunguka, then hapa utakuwa umeachwa kwenye mataa. Tatizo ni kwamba we don't learn from this. BTY, Afrika inarudi kwa wenyewe "wazungu" kwani ilishawahi kutoka kwneye mikono ya wazungu?
 
Gadafi kwisney!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Si ndo huyu alileta majeshi yake kuunga Mnoko dictator Idd Amin kutupiga Tz???

Jamani waungwana.... huyu Mtu leo amedadilika na kuwa mwema leo??

Angalieni consistency ya ubaya wa huyu mtu!!
 

Tuliaminishwa hivyo.Hivi huoni tumo katika mazingaombwe ya kusherehekea miaka 50 ya uhuru? uhuru wa nchi isiyokuwepo?

Vumbi litakapotulia kuna wengi watakaojua kuwa chini ya Gaddafi wazungu hawakuwa ni wenye kwenda na kuchota tu huko Libya, vyenginevyo zile 150 billion (sovereign funds) zisingepatikana.,Sio kama viongozi wa nchi nyengine. Ni kweli aliachwa peke yake lakini sasa ndio viongozi wengine watatia akili au wataitikia kwa utiifu zaidi, yes sir, yes,madam.
 
Mwanaume hufa na kuzaliwa siku Moja..umekufa Kamanda wangu lala kwa Amani..NAKUPENDA GHADAFF..Umeifia Libya na Afrika..wewe ni Simba dume..Nakulilia leo hata milele
 
Ndio maana natamani vita takatifu ifike

Tuwe tunapigana na west vs waadilifu
 
Mwanaume hufa na kuzaliwa siku Moja..umekufa Kamanda wangu lala kwa Amani..NAKUPENDA GHADAFF..Umeifia Libya na Afrika..wewe ni Simba dume..Nakulilia leo hata milele
A true African and Libyan hero
 
Reactions: Ame
BARACK OBAMA ANAWEZA AKAWA MBAYA KULIKO BUSH YEYE HACHONGI SANA ANAUA TU ,OSAMA GADAFI list goes on
 
......aisee huyu Gaddafi alikuwa mroho wa madaraka balaa!!! Angalia sasa yaliomkuta.
 
Kumbukumbu zangu zinanionyesha kuwa Gaddafi alipambana sana Africa iungane (United State of Africa) but alikosa support from other African leaders.

Mkuu regional integration ina process yake. Process inaanzia kutoka chini kwenda juu. Ni kama unavyomlea mtoto. Roughly, inaanza na free trade area, then custom union, then common market, then economic union na mwisho political union. So, kwenye integration yoyote, the political union ndio inakuwa the last one. This is the difficult one. Mfano mzuri ni European Union. Wamepitia process nzima lakini ipofikia stage ya mwisho ambayo ni political union wameshindwa.

Sasa Gaddafi eti alitaka integration ianze juu kwenda chini. Yaani alikuwa anataka ku reverse the process of integration. Na unaweza kuona wazi kuwa integration aliyokuwa anataka ni political union, bila kughusia masuala ya kiuchumi na kijamii ambayo ni foundation ya integration yoyote. Kweli alikosa support from other African leaders kwa sababu waliona reality kuwa there cannot be the United States of Africa based on political interests. Inabidi kwanza kuungana kwenye mambo ya kiuchumi na kijamii.

Mkuu huwezi kuoana kwanza, then muwe wachumba and then mnaenda dating. Kama ingekuwa rahisi hivyo ungekuta tayari tuna nchi inaitwa the United States of East Africa.
 
R.I.P Kamanda Ghadhafi wagema ulimbo wataongea sana ila nimekukubali kuliko hawa Marais wetu wapo Maremote ya wazungu tu
 
......aisee huyu Gaddafi alikuwa mroho wa madaraka balaa!!! Angalia sasa yaliomkuta.

Mroho alikuchukulia nini?!! MIafrika inatia aibu..mnasherehekea kifo cha KIongozi wa nchi ya Afrika..Bush ameua watu Mamilioni mbona hajakamatwa...ujinga ukija kuisha tutajua Ghadaff alikua anafaa sana..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…