The rise and fall of Colonel Muamar Gadaffi

The rise and fall of Colonel Muamar Gadaffi

Habari za kuaminika zinadai kuwa Kiongozi Mkuu wa Libya Muammar Gaddaf amekalia kuti kavu ,habari zinasema kuwa hali iliyofikia hairudi tena nyuma ,nae atakurupushwa na kung'olewa kama shina la muhogo,kuna brigedi za kijeshi ambazo tayari zimeungana na wananchi ,wazalendo wanasema wamefikia point of no return.

Hata hivyo upande wa Colonel Gadaf umezidisha nguvu na kutoa upinzani wa liwalo na liwe kama ni lawama iwe baadae kwa mikakati huo wanapiga risasi direct kwa wazalendo,habari zinazidi kutonya kuwa makao makuu ya Gadaf yaliopo Benghazi ambao ni mji wa pili kwa ukubwa , yameshachomwa moto na wananchi wanaelekea Tripoli ili kieleweke,kumbuka tu sasa kuna majeshi yalio pamoja na wananchi na wanatumia silaha na magari ya kijeshi katika kumng'oa Gadafi na mafisadi wenzake.

Vilevile muelewe kuwa Majeshi ya gadafi yapo katika mgawanyo,kuna kundi linaongozwa na mwanawe ,hili ndilo ambalo linasemekana halitakuwa tayari kuachia madaraka kirahisi,hapo ndipo mapambano yatakapokuwa makali.
SHIRIKA la kusimamia haki za binadamu la ‘Amnesty International’ limelitaka Baraza la Mpito Libya (NTC) kuchukua hatua za haraka kudhibiti vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na waliokuwa wanajeshi wa marehemu Kanali Muammar Gaddafi aliyeondolewa madarakani.
Katika ripoti yake iliyotoka hivi karibuni, yenye kichwa cha habari ‘Vita ya Libya, mauaji na ukatili,’ ripoti hiyo inatanabaisha kwamba vikosi vya ukombozi vimekuwa vikihusishwa na mauaji na ukatili dhidi ya binadamu.
Mauaji haya yanajumuisha mashambulizi dhidi ya raia, kampeni ya kushambulia nyumba kwa nyumba na ukiukwaji uliokithiri wa haki za binadamu.
Ripoti hiyo haikuishia hapo bali iliwanyoshea kidole hata wachache waliobaki na wanaoendelea kumuunga mkono Gaddafi (marehemu) linajihusisha na ukatili dhidi ya raia wasiokuwa na hatia.
Iliripotiwa hivi karibuni vikosi hivyo viliendesha ukatili dhidi ya raia wa Libya wenye rangi nyeusi.
"Vikosi vya baraza la mpito vinajihusisha na ubakaji, kuweka watu kizuizini bila hatia, kuwanyanyasa na kuwaua wanaohisiwa walikuwa askari wa Gaddafi ikiwa ni pamoja na kuwateka vijana wadogo na kuwaingiza vitani na raia wengine wageni kwa kuwahisi ni wafuasi wa Kanali Gaddafi," inasema sehemu ya ripoti hiyo.
Raia weusi wanaelezwa kulengwa zaidi na kampeni inayoendeshwa na vikosi vya ukombozi kwa kuhisiwa ni wanajeshi waliokuwa wa kukodi na kuwaua na kuwatesa raia wengine.
Wakiwa wanajiandaa kutoa hali halisi ya kile kinachoendelea Libya, Uongozi wa Amnesty umesema kwamba tayari umeshawasilisha ombi la kulitaka baraza la mpito la Libya kudhibiti ukatili na ubaguzi wa rangi unaoendelea kufanywa na askari wake pamoja na wale waliokuwa wakimuunga mkono Gaddafi.
“Baraza la mpito linapambana na wakati mgumu katika kupambana na askari watiifu wa Gaddafi na wafuasi wengine wanaomuunga mkono na kusababisha ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, na inavyoonekana limeshindwa kudhibiti hali hiyo.”
Mohammed al-Alagi, waziri wa sheria wa baraza la mpito nchini Libya, anasema vitendo vinavyofanywa na wafuasi wa Gaddafi visichukuliwe kama ni wahalifu wa kivita.
“Wale sio wanajeshi, ni watu wa kawaida kabisa,” alinukuliwa Mohammed al-Alagi alipozungumza na Shirika la Habari la Associated Press hivi karibuni.
Anasema unaweza kuwaita waasi na wanafanya makosa, lakini bado hawajafikia kiwango cha kuitwa “wahalifu wa kivita hata kidogo.”
Amani ya Libya hivi sasa iko shakani baada ya Gaddafi kuondoka, na hili tayari Amnesty wameshaliona. Je, Libya itakuwa na amani kama ilivyokuwa wakati wa Gaddafi?
Nikiiangalia Iraq ya marehemu Saddam Hussein ninapata picha ya inakoelekea Libya bila Gaddafi.
Gaddafi alikuwa na wafuasi wengi waliomtii na wanaoendelea kumtii hadi mwisho wa maisha yao.
Hawa ni wale walioneemeka na mfumo wa utawala wake, wakihakikishiwa makazi na mambo mengine ya msingi ya kimaisha.

Ni watu ambao walifaidika na neema nyingi katika Libya, neema ambazo pia zilizungumzwa na mashirika kadhaa ya kimataifa na kuitaja Libya kama mfano wa kuigwa duniani katika maendeleo ya kiuchumi.

Kundi hili katu halitomuunga mkono kiongozi mwingine atakayetawala hasa kwa kuwekewa mkono na nchi za Magharibi na kwao watamuona kama amepandikizwa au kibaraka.

Kinachotokea Iraq kwa watu kujilipua kwa mabomu huenda kikawa maradufu nchini Libya.
Saddam alitajwa kuua watu wengi wa jamii ya kikurdi na ushahidi ukawekwa hadharani, ushahidi wa mauaji yanayodaiwa kufanywa na Gaddafi bado haujawekwa hadharani, unaweza ukawepo au usiwepo na au ni chuki tu dhidi ya propaganda za chuki kutoka mataifa ya magharibi dhidi yake.

Kimantiki hili linaweza kuwapandisha hasira wafuasi wake waliobakia Libya iwapo kiongozi aliyopo atashindwa kuboresha maisha ya wananchi na uchumi kwa ujumla.

Wananchi wa Libya wanaweza kuunganisha nguvu dhidi yake, nguvu ambayo ilitumika na kumtoa Gaddafi madarakani, itamgeuka na kuwa kubwa zaidi baada ya kushindwa kuwafanyia yale waliyotarajia.

Hapa itaunganishwa nguvu ya wafuasi wa Gaddafi na wafuasi wa kiongozi huyo mpya waliokata tamaa, nguvu hizi zinaweza kuzua maafa makubwa kuliko tunayoyashuhudia nchini Iraq.
Gaddafi alichukiwa sana na nchi za Magharibi lakini Afrika itamkumbuka kwa mchango wake mkubwa aliowahi kuutoa barani humu.
Historia inatukumbusha kuwa Gaddafi alikuwa swahiba mkubwa wa rais mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela.
Mandela aliwahi kufanya ziara nchini Libya, wakati huo kukiwa na vikwazo vya kutokuruka kwa ndege katika anga la Libya. Ziara ambayo Rais wa wakati huo nchini Marekani, Bill Clinton aliipigia kelele sana.
Gaddafi alikuwa mstari wa mbele katika kuikomboa Afrika yote, akiasisi kuanzishwa kwa shirikisho la Afrika, ndoto ambazo majaaliwa yake baada ya kuondoka haijulikani nani ataziendeleza.

Gaddafi alikuwa mstari wa mbele kuzilipia michango ya kila mwaka ya Umoja wa Afrika (AU), nchi kadhaa barani Afrika lengo ni kuhakikisha kwamba umoja huo unakuwa wenye nguvu na imara, na kuwa mtetezi wa Bara la Afrika katika masuala mbalimbali kama ilivyo kwa Umoja wa Ulaya.

Bila kusahau michango ya kijamii aliyowahi kuitoa sehemu mbalimbali barani Afrika, wachambuzi wa masuala ya Mashariki ya Kati na Pembe ya Afrika wanaweka bayana kwamba Waziri Mkuu wa Baraza la Mpito nchini Libya, kwa wakati fulani aliwahi kufanya kazi na Gaddafi lakini walikuja kutofautiana baadaye na kutengana.
Si hivyo tu hata vikosi vilivyomuondoa madarakani navyo viliwahi kufanya kazi na Gaddafi. Pamoja na kwamba wamemuondoa madarakani kwa kushirikiana lakini wao pia siyo wamoja.
Haitakuwa sahihi kusema Gaddafi alifanya mambo mabaya tu. Alifanya na mazuri pia. Ni wajibu wa watawala wa sasa kuyaendeleza mazuri na kuyaacha mabaya.




h.sep3.gif



[TD="bgcolor: #ffffff"]
Libya bila Gaddafi itatawalika?
ban.blank.jpg


Khadija Kalili​
[/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF, align: center"]
amka2.gif
[/TD]
 
Ghadafi ulipendwa sana huku JF lakini wananchi wako walikuchukia sana. By the way mwanao Al Islam ni muongo, alisema atapigana hadi tone lake la mwisho lakini ulipouawa tu wewe akavunja ahadi hiyo. Sasa yupo mikononi mwa serikali mpya akisubiri kutoa entertainment katika mfululizo wa court appearances ambazo zinatarajiwa kuoneshwa katika TV: iwe ni the Hague ama Tripoli, yetu macho.
 
I wonder why people say gaddafi used to provided good services for his people sio kweli hata mshahara haujawahi kufika 1000usd na gaddafi alikuwa hapendwi na wa libya kabisa sema alikuwa babe tu na hakuna huruma yoyote ya bureau labda school lakini maji umeme alikuwa wanakula nataka kuna kulala eliza
 
sorry am using phone nasema gadaffi alikuwa real mnyonyaji nilikuwepo libya 12yrs nimeondoka 1983
 
Sasa kama umetoka 83 miaka karibuni 30 sasa, yawezekana mambo yalibadilika baada ya mwaka 1983
 
sorry am using phone nasema gadaffi alikuwa real mnyonyaji nilikuwepo libya 12yrs nimeondoka 1983

Chuo ndio ulimaliza Libya na bado unasubiri kwenda masomoni USA Dah! jf kuna story humu au watu wanasahau wayaandikayo?
 
I wonder why people say gaddafi used to provided good services for his people sio kweli hata mshahara haujawahi kufika 1000usd na gaddafi alikuwa hapendwi na wa libya kabisa sema alikuwa babe tu na hakuna huruma yoyote ya bureau labda school lakini maji umeme alikuwa wanakula nataka kuna kulala eliza

Dada muda wa kudanganyana sio huu ni kipindi kile cha ujamaaaaaaaaaaaaaaaaa. Sku hizi dunia ya utandawazi angalia link hii

mishahara ya walibya 2010

Mwaka 2010 mwalimu libya analipwa lyd 3000
Lyd (libya dinar) 1 = usd 0.8 so hizo ni kama usd 2700 na kama milion 4 ya kibongo. Iweje useme mishahara haikufika 1000 usd??

Na kama utawala ule ni wa kinyonyaji why now wanaandamana (japo havioneshw cnn na bbc)
 
Back
Top Bottom