"I call this first Obama stupidity." Mwanasheria, hongera kwa huo mtazamo wako kuhusu sakata la Libya, lakini nadhani haumfahamu vizuri Obama. Huyu bwana ni Realist wa nguvu, na anachoangalia kwa sasa ni maslahi ya nchi yake. Hivi kweli baada ya Iraq na Afghanistan, ulitegemea raisi wa U.S.A awe mstari wa mbele kwenye vita nyingine in the Islamic World? Kama alivyosema Mammamia, kwa nini European Union, ambao wapo pua na mdomo na Libya hawafungi vibwebwe kwenye hili sakata? Au the Arab League, ambayo inawakilisha zaidi ya watu millioni 300 kutoka nchi za kiarabu?
Na kama Obama akiamua kuingia kichwakichwa, halafu hii kasheshe ikawa ya miaka kadhaa kama ilivyo Afghanistan, na bila kuepusha mauwaji ya raia kama ilivyokuwa SERBIA (SEBRENICA)ni nani atakayebeba hilo jukumu?
Serikali ya Obama bado ipo katika hatihati ya kuchaguliwa endapo hataweza kuimarisha UCHUMI wa nchi yake, ambao pamoja na mambo mengine, vita vya Afghanistan na Iraq vilichangia. Sasa kwa nini ajiongezee vita ya tatu?
Leo tunaongelea Libya, je vipi hii vurugu ikitapakaa hadi kwenye nchi kama Saudi Arabia itakuwaje? Je itabidi Obama apeleke majeshi huko?
Ningekushauri ukazipitie upya zile principles za REALISM ili kumuelewa vizuri huyu ndugu yetu, na kuelewa mstakabali wake kwenye hili suala.