The rise and fall of Colonel Muamar Gadaffi

Gadafi kwa mikwara bana...hay ngoja tuone wamatumbi wanazamia sasa kwenda Europa...kama hawataishia kuzama baharini wote
 
Nashawishika kuamini kuwa yanayotokea libya yatakuwa kama ya Vietnam
Naamini kuwa ilikuwa rahisi kumwangusha Ghadafi kwa Nguvu ya umma kuliko majeshi ya magharibi..sasa Ghadafi kawapa wananchi silaha wapambane na adui mvamizi...
Inawezekana kabisa ikachukua muda mrefu na hatimae wavamizi wakashindwa.
 
Hapo nimekubali, kingine mbona wanalipua military base wakati ?
Kwenye some bases kuna SA-5 launchers so wanazishambulia hizi ili zisije kutumika kutungulia ndege pindi zitakapokuwa zinapatrol anga ya Libya.
Sasa kama ni hivyo ina maana magari nayo yana fly? hebu nieleweshe zaidi
Baadhi ya magari yanatumika kubebea Anti Aircraft Missiles au MANPADS.
 
hebu nielweshwe hapa! kwani muafrica lazima awe mweusi..?! na nywele za katani?!! see Afro Arab bahati nzuri utakuta picha za gadafi nyingi

Global Arab Network | Egyptian President calls for boosting Afro-Arab partnership | Egypt Politics
Ushawahi kukutana na Mlibya, Mmorocco au Malgeria yoyote anayejitambulisha kama muafrika? Gaddafi mwenyewe mpaka late 90s alikuwa anajichukulia ni muarabu alivyoona ndoto zake za kuunda taifa la kiarabu kwa kuungana na nchi nyingine za north afrika zimeshindikana akageukia kwenye idea ya umoja wa kiafrika akamwaga mipesa wee wakaunda AU wakampa na uenyekiti.
 
5:14pm: Turkey joins the chorus of international voices urging Col Gaddafi to relinquish power. PM Tayyip Erdogan: "Gaddafi is contradicting himself. His first words were very important when he said he does not have an official position. If he does not have an official position, then he should hand Libya over to whoever does have legitimacy."
 
Je Gaddaffi ameshafanya hivyo? Kuwapa silaha raia wote? Nimesoma kuwa amesama atafanya hivyo. Je ameshafanya hivyo?

Wanaomuunga mkono Gaddaffi watachezea kibondo cha West kisawa sawa. Ile habari ya kuzuia Gaddaffi kuua raia itasahaulika. Kuvunja human rights itakuwa inazungumzwa kama collateral damage ya ku-enforce UN resolution ya No fly zone.

wakimaliza kazi hapo wanaingia Uganda na Sudan. Hawa si wana mafuta pia?
 

ndoto za mchana.

qaddafi ameigawa nchi kikabila. kama amegawa silaha itakuwa ni kwa baadhi ya raia tu hasa makabila yanayomuunga mkono. ajiandae tu kwenda machinjioni-the hegue.
 
No fly mana halisi nin mana Gates kama alikuwa anaipinga. Help me
 

Unaweza kuwapeleka punda kwenye mto ila huwezi kuwalazimisha kunywa maji. Gaddafi kama anataka kuondoka madarakani haraka awapatie silaha raia ndiyo atajua kuwa wanamuunga mkono au wananmpinga. Hizi ni propaganda za mtu anayetapatapa. Gaddafi amejenga maadui wengi zaidi miongoni mwa wananchi wa Libya kuliko foreign countries. Alianza na kuua raia wake ambao wengi mpaka leo bado wanahasira nae, ukitaka kujua kuwa Gaddafi anatishia nyau ungeangalia siku UN inapitisha resolution walivyokuwa wanashangilia. Kwa ujumla ukiona askari unaowalipa vizuri na ambao wameapa kulinda nchi yao kwa amri yako wanakugeuka jua raia hawapo upande wako kabisa. Raia wote wanaomuunga mkono si kwa matakwa yao bali wanajua kuwa wasipofanya hivyo watauwawa.
 
Vita vya Libya ni hisabu isiyojuilikana



Großansicht des Bildes mit der Bildunterschrift: Ndege ya kijeshi ya NATO

Maamuzi ya Jumuiya ya Kimataifa kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Libya yanatajwa kuwa ni hisabati yenye mambo mengi yasiyofahamika, na kwamba nchi washirika zimeingia kwenye mgogoro zisiojua namna ya kuutoka.





Kile kinachoitwa "Muungano wa Kimataifa", chini ya uongozi wa Ufaransa, umeanza harakati zake za kijeshi dhidi ya utawala wa Libya, lakini bila ya shaka ni jambo lenye gharama zake.
Japokuwa pana vituo vichache vya jeshi la anga ambavyo unaweza kuvishambulia nchini Libya, huko hakutamaanisha kwamba nguvu za kijeshi za nchi hiyo zimemalizwa kabisa.
Muungano huu wa kimataifa unaweza kuingia kirahisi, na yumkini ndani ya wiki moja tu, ukawa umeweza kuwasaidia watu wa Benghazi kupata huduma zote muhimu, yakiwemo maji na umeme.
Lakini Muammar Gaddafi anadhibiti asilimia 80 ya Libya, na ana mkono wake juu ya kila rasilimali ya nchi hiyo. Ikiwa Muungano huu hauko tayari kukabiliana na ukweli huu, basi mashambulizi ya angani na udhibiti wa mipakani, hautakuwa chochote zaidi ya ushindi kwa Gaddafi, na sio kinyume chake.
Bildunterschrift: Großansicht des Bildes mit der Bildunterschrift: Rais Barack Obama wa MarekaniMarekani yenyewe bado ipo kwenye njia panda: upande mmoja inataka ijiingize kabisa kabisa, upande mwengine inataka iwe kando kando tu.
Rais Barack Obama ameondoa uwezekano wa kupeleka majeshi ya ardhini au hata kujiingiza kwenye mzozo huu kwa kipindi kirefu, lakini yeye na wenzake wanataka Gaddafi apate funzo.
Ikiwa hivyo ndivyo, basi lengo la kile kinachoitwa hatua za kijeshi dhidi ya utawala wa Gaddafi halifahamiki sawa sawa.
Maana ikiwa lengo lake ni kuwalinda raia tu dhidi ya mashambulizi ya vikosi vya Gaddafi, basi vikosi vya Muungano vina, kwa uchache, muda wa mwezi mmoja, kulifanikisha hilo. Kwa hivyo, Gaddafi anao muda wa kungojea.
Bildunterschrift: Großansicht des Bildes mit der Bildunterschrift: Kiongozi wa Libya, Muammar GaddafiLakini ikiwa lengo la hatua hizo ni kuuondosha utawala wa Gaddafi, basi majeshi ya Muungano lazima yafanye mashambulizi makali, tena ndani ya kipindi kifupi dhidi ya vituo vya kijeshi vya Gaddafi.
Bila ya mashambulizi hayo, kuuondoa utawala wa Gaddafi ni jambo lisilowezekana. Na huko kutakuwa ni kujiingiza kamili kamili kijeshi.
Ila ikumbukwe kuwa, hilo halikuwa azimio Namba 1973 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, lililoidhinisha marufuku ya anga dhidi ya Gaddafi hapo juzi, na pia haukuwa uamuzi uliotajwa wazi na viongozi wa mataifa makubwa yaliyokutana mjini Paris, Ufaransa, hapo jana (19.03.2011).
Na kwa vita hivi, kuna suali jengine la kujibiwa: Umejua kuvianza, lakini je unajua lini na vipi utavimaliza?
Inatarajiwa kuwa Muungano huu wa Mataifa haujapitikiwa bado na mafunzo ya vita vya Balkan, vya Iraq na kadhia inayoendelea hadi sasa nchini Somalia. Mwisho wa hili la Libya nao, hauonekani kuwa mzuri.
Mtu angeliweza kusema kuwa, ule uamuzi wa mwanzo wa Ujerumani kujiepusha kuingia kwenye mgogoro wa kijeshi na Libya ulikuwa sahihi.
Bildunterschrift: Großansicht des Bildes mit der Bildunterschrift: Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Guido Westerwelle Huo ulitakiwa uwe mtazamo wa Umoja wa Ulaya pia. sio kuchukuliwa na andasa za siasa za ndani za Nicolas Sarkuzy wa Ufaransa, ambaye anaukimbia mbinyo wa kisiasa ndani ya nchi yake kwa kujibebesha dhima ya kuongoza shinikizo dhidi ya Libya.
Ikiwa Muungano huu wa Mataifa utakuwa na bahati njema, basi utaweza kumdhibiti Gaddafi kijeshi na kisha kuushawishi Umoja wa Mataifa umuwekee vikwazo vya silaha. Lakini ukikumbwa na bahati mbaya, basi ujitayarishe kwa hasira za mkizi kutoka kwa Gaddafi mwenye silaha.
Je Ufaransa na Italia zimejitayarisha kuyakaribisha makombora ya Gaddafi kwene miji ya Neapal au Marseille? Maana anaweza kuwa tayari kuyatuma huko.
Na kwa upande mwengine, ikiwa mashambulizi ya majeshi ya Muungano yataleta maafa makubwa kwa raia, basi si vigumu kwa maoni kwenye nchi za Kiarabu na Kiislamu kubadilika haraka sana, yakazigeukia nchi washirika.
Kwa kila hali, safari ya mkasa na yenye mwisho usiojuilikana ndio imeanza.
Mwandishi: Bernd Riegert/ZPR
Tafsiri: Mohammed Khelef
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman
 
1854: The spokesman said all Libyan armed forces units have been told to follow a ceasefire, beginning at 2100 local time
 
mnh knawaka moto huko mana leo majeshi ya marekani na uingereza yameingia huko
 
Yule bwana alokua akijifanya chizi kwa kuua watu wake kila kukicha, amepata akili baada ya kuchezea kichapo kutoka France, US na UK. BBC wameonyesha live viongozi wa jeshi wakitoa amri kwa vikosi vyote kusitisha mashambulizi ya aina zote kwa hao waliokua wanawaita 'rebels' wametoa amri kwamba badala ya kushambulia watu wahakikishe watu wote wako salama, hakuna ruhusa kushambulia mtu yeyote...Hongera Obama and the co, kumbe huyu bwana akili anayo ule uchizi ulikua wa kujifanyisha
 
It makes some sense, labda wameamua kuelekeza nguvu zao kukabiliana na misukosuko inayowaandama..
Ila kama ameamua kufanya kama njia ya kuwakomoa Wa-Yurop basi zitakuwa ni hasira za kike!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…