Gaddafi ni mlibya aliyelipukwa na wendawazimu wa ajabu kabisa, kufikiri alizaliwa kuwatawala walibya wenzake kwa umri wake wote, badala ya kukubali kukataliwa kuendelea kutawala, yeye kawaalika wageni kuja kuivuruga libya, marekani na washirika wake kwa sasa wanawatetea walibya kwa kuwapiga walibya, hayo ni matokeo ya wendawazimu wa gaddafi, alichokosea ni kuwapiga wananchi wenzake akijikweza kuwa na ubora kuliko walibya wengine, jumuiya ya kimataifa huwa haifurahii kiongozi wa nchi yoyote kuwashambulia raia wa nchi yake, maadamu wameshaanza kumlegeza nguvu za magoti, vifundo vya miguu,mabega na viwiko vya mikono, ajue mwisho wake umekaribia kama sii umefika.