Nyenyere
JF-Expert Member
- Sep 9, 2010
- 14,804
- 10,715
Hakuna asiyefaham sasa chanzo cha vurugu za Libya ni Mwamerika na washirika wake,
nastaajabu kuna waafrika eti wanaojiita great thinkers wanakenua meno na kufurahia yanayoendelea libya sasa,eti ni "people's power" ,kweli?
haya ,sisi yetu macho na masikio,ila historia itawahukumu wale wote wenye tabia za akina chifu mangungo,,
Hivi na wewe unajidhania kuwa great thinker? Wewe ni sympasizer tu. Wananchi wa Libya wakikusikia hakika watakujengea kisasi. Usishabikie mambo usiyoyajua. Hao unaowalaani wameombwa na umoja wa nchi za kiislamu wamsulubu huyo mpendwa wako, tena baada ya kubembelezwa sana. Mie nafurahia sana kinachoendelea usiku huu kwani hatimaye wanchi wa Libya watapumzishwa na mgogoro usio wa lazima baada ya best yako anayelilia kufia madarakani kuchezea kichapo cha haja. Halafu nikukumbushe tu kuwa huyo nduguyo ametofautiana na wewe kwani anadai kuwa chanzo ni alqaida na wavuta bangi na madawa ya kulevya. Sasa sijui mkweli ni nani kati ya yeye na wewe?