The rise and fall of Colonel Muamar Gadaffi

The rise and fall of Colonel Muamar Gadaffi

Duu ndo nimeigundua baada ya propaganda kuzidi kipimo, maana zimekuwa tena si propaganda bali kutunywesha sumu ya nyoka live, hivi unajua unaweza pasua screen bure si kwa sababu unampenda Gadafi ila kwa sababu unalazimishwa kuuamini uongo.
 
Mkuu
NATO, US na "rebels" wao wakifanikiwa kuiangusha serikali ya Gaddafi. Wananchi wa Libya watapata serikali kibaraka. Watapata uhuru wa kusema kama sisi hapa Tanzania lakini watasaga meno.
Watatamani utawala wa Gaddafi urudi kama watu hapa JF wanavyotamani Utawala wa Mkapa urudi.
Na fisadis aka kampuni za west zitakuwa zinajichotea mabilioni yao kutoka frozen assets, reconstruction na dili la kufyonza mafuta ya Libya.

Amini kama wananchi wa US na West wangekuwa habari sahihi na kujua mafanikio ambayo Gaddafi kayapata na maendeleo ambayo kawaletea Libya, wengi wangehamia Libya
...lakini US na West waliifanya kazi ya kumgeuza Gaddafi, "mad man" kwa ustadi na sasa ndio hivyo" wana-protect civilians" na kumalizia project yao.

Kwa kuibomoa Libya na Gaddafi wanafanya kazi yenye malengo ya kuiua AU pia. Afrika itabaki katika utumwa wa West na US kwa miongo kadhaa ijayo.
hapo siwezi amini kabisa
 
Mkuu ndio umeigundua leo hii clip?

Angalia jamaa wa BBC wanavyodanganya kweli kuwe na live mapigano mwandishi wa habari awepo ktk mapigano, angalia kwenye nyeusi nimecheka kweli.


Ahmed Al Omran

tweets Jibril: Mohammed Gaddafi called one of the rebels saying he wanted to surrender, then apparently he changed his mind.

Paul Danahar BBC Middle East bureau chief
tweets: Ran with everyone else in compound. #Gaddafi forces started attacking as darkness fell. 3 bullets whistled just above my head #Libya

 
Duu ndo nimeigundua baada ya propaganda kuzidi kipimo, maana zimekuwa tena si propaganda bali kutunywesha sumu ya nyoka live, hivi unajua unaweza pasua screen bure si kwa sababu unampenda Gadafi ila kwa sababu unalazimishwa kuuamini uongo.
Nimekupata Mkuu. Nafikiri huu ni wakati muafaka wa sisi waafrica kujiuliza je ni lazima viongozi wetu wang'ang'anie madaraka mpaka waje kungolewa kwa nguvu na kuharibu mali na miundombinu ya nchi? Hivi ilikuwa lazima Gaddafi kung'ang'ania madaraka kwa kiasi alichofanya?

Kuna watu wengi wanasema Gaddafi aliwapa wananchi wake mafaa mazuri zaidi ya kwingineko kokote barani Africa. Granted, hiyo haipingiki. Lakini je yeye na familia yake pamoja na wapambe wake walijilimbikizia mihela mingapi? Hiyo kweli ni haki?

Tutaendelea na mifumo mibovu kama hii mpaka lini? Na ndio maana maadui wa bara hili wanapata mwanya wa kutusambaratisha kila kukicha. Hayo ni maoni yangu na sisemi kwamba nipo sahihi!
 
Hawa jamaa wa MATHABA wanaongoza kwa propaganda za kitoto. Nimewafwatilia kwa muda lakini sioni kama wanalo la maana wanaloongea. Wanatumia taktiki za mfumo wa habari wa kikomunisti (umepitwa na wakati). Hebu soma hivi vipengele:............................................

........................................
Halafu hapo hapo wanatembeza bakuli kinyemela.

Isn't it time that you supported us? Unlike the compromised media, we are not in the pay of advertisers who would dictate terms, nor do we use Google ads which would bring in plentiful revenue give our reader numbers, out of principle as their ads are not appropriate nor quality, nor are we owned by any zionist media barons, nor are we funded by donations from political parties, or owned by intelligence services. It is you, the reader alone, who keep us functioning. So, DONATE NOW or SUBSCRIBE.

My take: Ni watu kama akina Ami na MpigaKelele ndio wanawasomaga na kuwapapatikia hawa jamaa MATHABA (halafu wanatulazimisha na sisi eti tuwaunge mkono!) Tafadhali enyi watu wawili jihadharini sana na propaganda zisizo na mashiko!
1.Kuhusu kuchangiwa kwa Mathaba.net

Kuomba mchango wa kuendesha website kama hiyo (Mathaba.net) ni jambo la kawaida kabisa na hawajaanza wao, wengi wanafanya hivyo. Askari kweli sasa unaniangusha kwa kukosa hoja yenye nguvu yaani unataka jamii ielewe na kuamini kuwa Wikileaks, Wikipedia,na hata JF yetu kweli nao wanafanya dhambi kwa kuomba michango kwa ajili ya kuendeleza kazi wanayoifanya?

2.Kuhusu Mathaba.net kutoa habari sahihi na za kweli

Mimi binafsi ni mshabiki mkubwa wa habari sahihi na za kweli. Usahihi na ukweli wa habari unatokana jinsi habari yenyewe inavyothibitishwa na mtoa habari mwenyewe. Mathaba.net wamekidhi vigezo hivyo, mwenyewe "Askari Kanzu" umeshuhudia juzi na jana jinsi vyombo vya habari unavyoviamini vilivyo kupeleka porini kuhusu kukamatwa kwa watoto wa Comred Gaddaf.

Kwa haya mawili hapo juu ninadhani hutakuwa na sababu ya kuamini kuwa nina fuatilia habari zisizo na mashiko kutoka Mathaba, vinginevyo nitaanza kushawishika kuamini kuwa huko kwenye "payrol" inayowajumuhisha Tebels(terrorist rebels) kutoka bengharz.
 
Nimekupata Mkuu. Nafikiri huu ni wakati muafaka wa sisi waafrica kujiuliza je ni lazima viongozi wetu wang'ang'anie madaraka mpaka waje kungolewa kwa nguvu na kuharibu mali na miundombinu ya nchi? Hivi ilikuwa lazima Gaddafi kung'ang'ania madaraka kwa kiasi alichofanya?

Kuna watu wengi wanasema Gaddafi aliwapa wananchi wake mafaa mazuri zaidi ya kwingineko kokote barani Africa. Granted, hiyo haipingiki. Lakini je yeye na familia yake pamoja na wapambe wake walijilimbikizia mihela mingapi? Hiyo kweli ni haki?

Tutaendelea na mifumo mibovu kama hii mpaka lini? Na ndio maana maadui wa bara hili wanapata mwanya wa kutusambaratisha kila kukicha. Hayo ni maoni yangu na sisemi kwamba nipo sahihi!

Gadafi ni mpuuzi tu hasa ukifuatilia remarks zake kuhusu waafrika kule Italy, kwa upande wa pili, pamoja na yote wao NATO inawahusu nini kwa Gadafi kungangania madaraka. Na kwa upande wa tatu, sio waafrika wanaongangania madaraka bali ni wao watu wa magharibi ndiyo wanaopanga viongozi nani awe nani asiwe, na si kwamba wanagagania bali wengi wao wanawekwa na wanawadaganya.

Mfano, wakitaka kufanyiza vita ktk nchi ukishindwa uchaguzi wanakwambia kaa usiondoke, ukiondoka tutakuonyesha sie ni nani wee kaa tutakupiga tough, na akikaa dakika za majeruhi wanamugeuka, basi jamaa anakuwa hana option zaidi ya kupigana hadi sekunde ya mwisho.

Huu ujanja unakwenda kwa kuambatanisha na miafrika akili zao ni mbovu kwa hiyo lazima tuwaamlie cha kufanya. Hebu endelea kuangalie ile riot ya UK kuna waafrika walikuwepo kama 6-7 walionaswa na camera yani vyombo vya habari ndo vilikuwa vinatilia msisitizo kuonyesha hao tu, wakati wazungu walikuwa mvua wana wa bypass.

Hata hivyo, kuna sehemu kweli wanangangania lakini tujiulize kwanini Tanzania kila miaka 10 ikiisha wanaondoka pamoja na ufisadi wao? hata hivyo itakuja siku mmoja atagagania kama kutakuwa na wese la kutosha kuleta NATO.
 
hapo siwezi amini kabisa

Naheshimu uamuzi wako huu.

Huyu mama at least anafuatilia ukweli.

After reminding the readers that under The Green Book form of governance, Libya has achieved what we in the United States do not enjoy: universal health care paid for by the state; universal education subsidized through the Ph.D. level by the state; oil revenue sharing; subsidized housing; subsidized automobile purchases; $50,000 marriage subsidy for newlyweds; and more. The more just happens to be what Libya has in common with six other countries that General Wesley Clarke announced were on a list for war that he saw from the Pentagon: neither Iraq, Syria, Lebanon, Somalia, Sudan, Iran, nor Libya belong to the Bank of International Settlements, the Central Bankers' bank.

From Cynthia McKinney: Who's War in Libya? | Facebook
 
... "Askari Kanzu" umeshuhudia juzi na jana jinsi vyombo vya habari unavyoviamini vilivyo kupeleka porini kuhusu kukamatwa kwa watoto wa Comred Gaddaf...
Ukifuatilia michango yangu ya jana na juzi utaona kabisa hao jamaa hawakunipeleka porini manaake angalau na mimi nina uwezo wa kuchambua wanayoandika.

Kuhusu MATHABA kutembeza bakuli: kwa nini wanajiosha eti hawapokei chochote kutoka "any zionist media barons, nor... funded by donations from political parties, or owned by intelligence services"? Wanajishtukia, siyo? Sidhani kama unaweza kuwafananisha hao jamaa na JF, Wikileaks au Wikipedia. MATHABA wamekaa kipropaganda zaidi!
 
The Truth About The Situation in Libya.
Cutting through the government propaganda and media lies
august-13-stop-bombing.jpg

"Answer Coalition"
Libya is a small country of just over 6 million people but it possesses the largest oil reserves in all of Africa. The oil produced there is especially coveted because of its particularly high quality.

The Air Force of the United States along with Britain and France has carried out 7,459 bombing attacks since March 19. Britain, France and the United States sent special operation ground forces and commando units to direct the military operations of the so-called rebel fighters – it is a NATO- led army in the field.

The troops may be disaffected Libyans but the operation is under the control and direction of NATO commanders and western commando units who serve as "advisors." Their new weapons and billions in funds come from the U.S. and other NATO powers that froze and seized Libya's assets in Western banks. Their only military successes outside of Benghazi, in the far east of the country, have been exclusively based on the coordinated air and ground operations of the imperialist NATO military forces.

In military terms, Libya's resistance to NATO is of David and Goliath proportions. U.S. military spending alone is more than ten times greater than Libya's entire annual Gross Domestic Product (GDP) which was $74.2 billion in 2010, according to the CIA's World Fact Book.

In recent weeks, the NATO military operations used surveillance-collecting drones, satellites, mounting aerial attacks and covert commando units to decapitate Libya's military and political leadership and its command and control capabilities. Global economic sanctions meant that the country was suddenly deprived of income and secure access to goods and services needed to sustain a civilian economy over a long period.

"The cumulative effect [of NATO's coordinated air and ground operation] not only destroyed Libya's military infrastructure but also greatly diminished Colonel Gaddafi's commanders to control forces, leaving even committed fighting units unable to move, resupply or coordinate operations," reports the New York Times in a celebratory article on August 22.

Read More: Answer Coalition
 
End the wars! Millions March in New York

august-13.jpg



Harlem, New York
We are facing the most serious economic crisis this country has seen in decades. Millions are out of work. Education and social services are being slashed. The government tells us there is no money.

Yet when it comes to funding the war and occupation of Iraq and Afghanistan, there is never a question of coming up with money. And now the Pentagon is launching a new war on the African continent with the bombing of Libya.

It’s time to fight back!

The "Millions March in Harlem" event has been initiated by the December 12th Movement, and endorsed by a wide range of organizations, around the key demands:

  • Stop the bombing of Libya
  • End the sanctions on Zimbabwe
  • Stop Bloomberg’s destruction of our communities
 
Google nao wamekubali kubadilisha jina la Green Square kurudi kuwa Martyr's Square baada ya majeshi ya waasi kuuteka mji wa Tripoli.

Green Square ni jina ambalo lilibatizwa baada ya kiongozi wa nchi hio Muamar Gaddafi kutwaa madaraka mwaka 1969 kutoka jina lake la kawaida la Martyr's Square yaani mzunguko wa wajitoao mhanga. Lilikuwa na nembo ya kijani ambayo pia ilikuwemo kwenye bendera ya nchi hio ikimaanisha alama ya nguvu ya kiongozi huyo wa nchi hio.


Google walikubali pendekezo la mmoja wa wanamapinduzi la kubadilisha jina hilo hasa katika wavuti yake yenye kuonesha ramani katikati ya mji huo wa Tripoli lakini bila ya kutahadharisha juu ya uwezekano wa kutokuwepo kwa mapendekezo ya kupata majina yanayofanan na jina hilo.

Lakini mmoja wa wangalizi wa wavuti hio (Moderators) amesema kwamba jina hilo halimaanishi hasa lengo halisi bali ni kusaidia kusukuma wimbi la kusudio la kufanya mabadiliko ya kisiasa.

Jina hilo la Martyr's Square limo katika lugha za Kiarabu na Kiingereza ili kuondoa mfarakano au lugha gongana.

Mtoaji mkuu wa huduma za internet nchini humo jana laifungua njia hio muhimu ya mawasiliano na mpaka leo watu wamo mtandaoni wakirusha habari na kupeana updates.
 
Sasa watulie wajenge libya yenye democracy, ila nina wasiwasi sana na wamarekani

Yawezekana watajenga Libya yenye "DOMOcracy" kama Tanzania.

Cutting through the government propaganda and media lies

A False Pretext

The United States, United Kingdom, France, and Italy targeted the Libyan government for overthrow or "regime change" not because these governments were worried about protecting civilians or to bring about a more democratic form of governance in Libya.

The Truth About the Situation in Libya
 
Nimeshawishika kuandika hii thread kwa sababu moja tu NATO NA NCHI ZA MAGHARIBI ZIMEKIDHI MATAKWA YAO YA KUMUONDOA MADARAKANI GADAFI KWA KUIPUUZA AFRICA.


1. AU imewekwa pembeni na UN na kudhalilishwa kwenye suala la Libya. Ni wazi kutakuwa na mpasuko mkubwa miongoni mwa nchi moja moja na ndani ya AU kwa maslahi ya mataifa ya Magharibi. Hii itapanuka hadi kwenye kutuamulia watawala.

2. Naona sera ya kuwachonganisha waafrika ndani ya nchi zao ili wapore mali ghafi ya Libya imepata nafasi na fursa kubwa sana.

3. Wanataja kustabilise Libya licha ya wao kutojua kwa vipi? Hatima yake tumepata Somalia nyingine kwa lazima ya mataifa ya magharibi.

Kwa yaliyotokea Libya bila ushabiki sioni nchi hata moja itakayoweza kusimama kutetea maslahi yake bila kutilia manani maslahi ya nchi zenye mabavu ya uchumi na kijeshi

Lakini kwa kuamini vichwa vya JF naomba tubadilishane mawazo kwa kuwekana sawa kwenye hili suala tukizingatia kweli Gadafi naye alikaa madarakani muda mrefu, lakini si peke yake. Wapinzani wake wamefadhiliwa na nchi za magharibi ambazo pamoja na mengine zimehusika moja kwa moja kuharibu uwekezaji wa muda mrefu wa kimaendeleo wa Libya. Mwisho majukumu ya UN na AU kwa sasa ni wazi kuna kukizana labda tuseme ni zama mpya hizi.

Tafadhali naomba tupanueni mawazo, maana mtazamo wangu labda na wa wengine kama mimi umetatizika sana.
 
article-2029384-0D8B0A4D00000578-615_634x318.jpg

Vijana wa ukombozi wakishangilia ushindi baada ya kuangusha picha kubwa iliokuwa imetundikwa ukutani mwa jengo moja la ofisi.

Azizia-1_1979160c.jpg

Watu waliochoka kulala usingizi mzito wakikany'aga sanamu ya mzee Gaddafi ambae mpaka usiku huu hajulikani aliko baada ya kuitawala nchi hio kwa miaka 42!.
 
Dunia hii inawenyewe wanadamu sikuhizi tunapelekwa puta puta tuu kama makondoo. Yaani hao NATO ni North Atlantic Treaty Organization sasa nashangaa kwani libya ipo north Atlantiki na dunia nzima inasheherekea tuu kama kawaida tunadanganywa lakini tunaona bora zaidi ya kuuliza kwanini NATO hipo huko si wange wapa hayo mafweza AU waongoze hiyo campeni ya kumtoa gadafi kidemocrasia na wangetupatia maajira na mavifaa kwenye ka AU kujikimu siku zijazo. Au ndo walikuja kujipatia mazoezi kwa Gadafi ili zile silaha zao zisiote kutu. Manake hawa watu kama wangetaka kumuua gadafi wangekuwa wameshamuua kitambo kutoka huko atlantiki wanapotakiwa wawepo na mafataki yao yakisasa. Nashangaa walienda kuvunja vunja tuu kamji kawatu kalikuwa kamejichokea kama Dar lakini hawakuwa na madeni yakifisadi. Sasa wakimtoa gadafi wataweka kibaraka wao hapo wawaingize walibya katika madeni ya kifisadi na wataenda kujenga huko kama milele na walipwe tena na walibya.
 
hizo data labda ukizilinganisha na maisha ya hapa tz ndo utaona walikuwa wanafaidi,ila kuna nchi zina mambo mazur kuliko hizo-then hata umpe mwanadamu nini,kaka hana uhuru wa kuzungumza,kupinga hakuna cha maana ulichofanya,ndicho alichokuwa hatoi colonel gadaf

basi msiilalamikie ccm kwani inawapa huo uhuru wa kusema mtakayo
 
Gaddafi says withdraws from Tripoli compound

Libyan leader Muammar Gaddafi said on Wednesday that his withdrawal from his Bab al-Aziziya headquarters was a "tactical move" after the compound was levelled by 64 NATO air strikes.
Speaking in an address on a local Tripoli radio station, which was reported by Al-Orouba TV, broadcasting in conjunction with Al-Rai TV, Gaddafi also vowed "martyrdom" or victory in his fight against NATO.

Gaddafi says withdraws from Tripoli compound | News by Country | Reuters
 
Mkuu
NATO, US na "rebels" wao wakifanikiwa kuiangusha serikali ya Gaddafi. Wananchi wa Libya watapata serikali kibaraka. Watapata uhuru wa kusema kama sisi hapa Tanzania lakini watasaga meno.
Watatamani utawala wa Gaddafi urudi kama watu hapa JF wanavyotamani Utawala wa Mkapa urudi.
Na fisadis aka kampuni za west zitakuwa zinajichotea mabilioni yao kutoka frozen assets, reconstruction na dili la kufyonza mafuta ya Libya.

Amini kama wananchi wa US na West wangekuwa habari sahihi na kujua mafanikio ambayo Gaddafi kayapata na maendeleo ambayo kawaletea Libya, wengi wangehamia Libya...lakini US na West waliifanya kazi ya kumgeuza Gaddafi, "mad man" kwa ustadi na sasa ndio hivyo" wana-protect civilians" na kumalizia project yao.

Kwa kuibomoa Libya na Gaddafi wanafanya kazi yenye malengo ya kuiua AU pia. Afrika itabaki katika utumwa wa West na US kwa miongo kadhaa ijayo.


Thank U Sir Nilijua Niko mi na Jmushi tu. Naomba jamii forum watufungulie our own window. Uliyosema ni haswaa ya ukweli.
 
Back
Top Bottom