The rise and fall of Colonel Muamar Gadaffi

The rise and fall of Colonel Muamar Gadaffi

Hakuna ulingano wa kiungozi kati ya libya na uk. yule ni ceremonial figure hana nguvu ktka maamuzi ya kiserikali England wana uchaguzi wa pm kama israel, india, germany walivyo na Rais asiye na maamuzi ya kiserikali
nilijua mtakuja na hoja hii eti"hana executive power'....lakn ndio tulivyo na tulivyokaririshwa shuleni mkuu
 
Naona unashindwa kufanya tofauti ya mambo! Malkia/ Rais? Amekuwa malkia toka 1952, ila alikuwa Malkia rasmi (crowned) mwaka 1953.
Hata hivyo haendeshi serikali wala kuachagua mawaziri kama Gaddafi....
 
tena Afrika kwa unafiki sijui ni kwanini na sijui utaisha lini...Gaddafi wakati mapigano yakiendelea nchini libya, nchi za Afrika hakuna hata moja ambayo pengine ingeongea chochote yani kwakweli kuna mengi ya kujiuliza! huyu jamaa alikua na marafiki kibao ikiwamo Nigeria, zimbabwe na wengine tena ni hivi juzi tu alikua ni mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, lakini kimya kilitanda mpaka Gddafi anauawa tena kinyama sana! sasa cha kushangaza baada ya huyu jamaa kufa sasa ndio stori zimeanza ooh alikuwa mpiganaji ooh sijui nini! inatakiwa siku moja na sisi kama waafrika tusimame na kusema kitu mbele ya nchi za magharibi....mbwai mbwai tu bana potelea mbali
 
sharia law ni kitu gani ??? Mbona mnaburuzwa hivi???? Hakuna kitu sharia law katika dini ya kiislamu

kwamba mimi ni binadamu ninazungumza ila sina mdomo? wewe gavana umechelewa kweli kwa hiyo university of zanzibar na morogoro wanaposema wanafundisha Shariah law wanauhadaa umma?!!
 
Kwa uzoefu wangu hua nimeshuhudia nchi nyingi zilizotawaliwa na mnatawala mmoja kwa kipindi kirefu siku akiondolewa madarakani nchi za namna hiyo huwa hazitawaliki na kisha kugawanyika vipande .mifano hai ni Yugoslavia walimuondoa Tito,Zaire --Mobutu,Somalia--Siad Barre. n.k nchi kama Iraq na alfghanistan majeshi ya Marekani na washirika yalibaki kulinda baada ya watawala wa muda mrefu kuondoka. Leo tunaongelea libya ambapo Gadafi ameondolewa na NTC ikisaidiwa na jeshi la NATO, libya inaelekea huko kutotawalika na kugawanyika.
SHARIA LAW:
Kitendo cha NTC kuadopt sharia ni kofi la usoni kwa Marekani na washirika wake,sababu huwa wakipindua mtawala wa nchi wanataka wapandikize raisi ambaye anamsimamo wakati yaani moderate islam.kwa hili hapa sitaona ajabu tena NTC ikitengenezewa mazingira ya kuondolewa madarakani. Kwa ujumla NTC Wanakibarua kigumu sana kwa sababu rafiki aliewasaidia kuingia madarakani ana malengo tofauti na wanavyo dhani baadaye watamkumbuka conek Muamar Gadaffi au wataikumbuka hii mistari michache nilioiandika kama wanaelewa kiswahili manaake nacho kinakua kwa kasi ya jetfighter!. na wahi chai asanteni.
 
Safi sana maana nchi itaendeshwa kwa kila mwananchi kufuata sheria na atakayekiuka basi atakuwa anajua adhabu yake
 
Wamedai waliomuua gadafi wa kristo hii sharia wanaipata wapi wakristo
wanavuna walichopanda mkuu usiwaonee huruma hao
shule nalo nijanga lingiine la kitaifa walibya walisoma wengi wakonje
 
nilijua mtakuja na hoja hii eti"hana executive power'....lakn ndio tulivyo na tulivyokaririshwa shuleni mkuu

wewe tueleze hayo ambayo hatukufundishwa na tumeshindwa kusoma kupitia mitandao,magazeti,vitabu nk.
 
Haina haja ya kulumbana kwa jambo ambalo linaeleweka,Malkia na Rais ni vitu viwili tofauti na hata majukumu yao ni tofauti.
 
Moja ya sababu waliyoitoa NATO kuhalalisha nia yao ya kusaidia kumng'oa na mwishowe kumuua Gadaffi ni kuwa jamaa amekaa madarakani muda mrefu. Kwa wengi hii linaonekana kama ni sababu muhimu, ingawa kuna sababu nyingine zaidi hasa za kiuchumi zilizowafanya hawa wazungu wamng'oe jamaa kutoka madarakani. Kuna jambo nimeona wanajf tujuzane kuhusu muda aliokaa gadaffi kama moja ya sababu ya hii mijitu kuingilia uhuru wa ndani wa nchi zinazoendelea. Kama niko sahihi, ni kwamba Malkia wa Uingereza kimsingi ni Mtawala kwa Waingereza. mambo mengi ya kisiasa kwa Waingereza kwa namna moja au nyingine ni lazima Malkia ahusishwe ktk kufikia maamuzi. kumbukumbu zinaonyesha kwamba haka kabibi kamekuwepo madarakani (umalkia) tangu mwaka 1957-i stand to be corrected-hadi sasa. Hapa najiuliza iweje Uingereza kujidai kwenda Libya kwa kisingizio cha kumuondoa mtawala aliyekaa madarakani kwa muda mrefu ili hali na wao mtawala wao amekaa madarakani kwa muda mrefu zaidi ya Gadaffi? Pamoja na ukweli kwamba Gadaffi alitawala kwa muda mrefu na hakuwa na dalili ya kuachia madaraka, nadhani Waingereza hawakupaswa kutumia kigezo cha kuwepo madarakani kuwa ni moja ya sababu za kumuondoa madarakani. Walipaswa na wao wajichunguze kwanza ndipo waje na sabau hiyo. Ni mtazamo wangu tu!
Kwani Gadafi alikuwa mfalme au,kama angekuwa mfalme asingeng'olewa ,sidhani sababu ya kukaa muda mrefu ndio imemuondoa Gadafi,huko Swaziland yupo mfalme Mswati hatujui atakaa muda gani nadhani mpaka afe na hutaona madege ya NATO yakienda kumpiga mfalme Mswati kwa kuwa eti kakaa muda mrefu
 
Hakuna ulingano wa kiungozi kati ya libya na uk. yule ni ceremonial figure hana nguvu ktka maamuzi ya kiserikali England wana uchaguzi wa pm kama israel, india, germany walivyo na Rais asiye na maamuzi ya kiserikali

Inawezekana unachosema ni ukweli ila kuna vitu nadhani mnamiss hakuna PM anayepitishwa Uk kama hana mahusiano mazuri na malkia kwa maana hiyo basi uamuzi wowote ambao utakuwa tata kwenye bunge au kwa PM mwenyewe yeye hutoa maamuzi kwa mlango wa nyuma kama alivyokuwa anafanya mwalimu Nyerere hapa kwetu lakini tulikuwa hatutaki kuelewa. Na kwa taarifa yako nchi kama Israel aliyetoa idhini ya kupigwa risasi Yitzak Rabin ni Rais wao kwa maana hapakuwa na masilahi ya wayahudi kwenye mikataba aliyofanya Rabin. Na swali rahisi ni hivi kwa jinsi Mossad walivyo smart yule kijana alimfikiaje Rabin na kumlipua kwa bastola ya kawaida kabisa huoni kama alikuwa
security pass kama yao.
 
Kwani gadafi alimwangusha nani kuingia madarakani.?fikirieni eeh.
 
Inawezekana unachosema ni ukweli ila kuna vitu nadhani mnamiss hakuna PM anayepitishwa Uk kama hana mahusiano mazuri na malkia kwa maana hiyo basi uamuzi wowote ambao utakuwa tata kwenye bunge au kwa PM mwenyewe yeye hutoa maamuzi kwa mlango wa nyuma kama alivyokuwa anafanya mwalimu Nyerere hapa kwetu lakini tulikuwa hatutaki kuelewa. Na kwa taarifa yako nchi kama Israel aliyetoa idhini ya kupigwa risasi Yitzak Rabin ni Rais wao kwa maana hapakuwa na masilahi ya wayahudi kwenye mikataba aliyofanya Rabin. Na swali rahisi ni hivi kwa jinsi Mossad walivyo smart yule kijana alimfikiaje Rabin na kumlipua kwa bastola ya kawaida kabisa huoni kama alikuwa
security pass kama yao.

Shida ya stori za vijiweni? Unajua waziri mkuu wa Uingereza anavyo chaguliwa mpaka ukahusishe Malikia na Waziri Mkuu?
 
Inawezekana unachosema ni ukweli ila kuna vitu nadhani mnamiss hakuna PM anayepitishwa Uk kama hana mahusiano mazuri na malkia kwa maana hiyo basi uamuzi wowote ambao utakuwa tata kwenye bunge au kwa PM mwenyewe yeye hutoa maamuzi kwa mlango wa nyuma kama alivyokuwa anafanya mwalimu Nyerere hapa kwetu lakini tulikuwa hatutaki kuelewa. Na kwa taarifa yako nchi kama Israel aliyetoa idhini ya kupigwa risasi Yitzak Rabin ni Rais wao kwa maana hapakuwa na masilahi ya wayahudi kwenye mikataba aliyofanya Rabin. Na swali rahisi ni hivi kwa jinsi Mossad walivyo smart yule kijana alimfikiaje Rabin na kumlipua kwa bastola ya kawaida kabisa huoni kama alikuwa
security pass kama yao.

Unajua Bwana mambo mengine si vizuri kuzungumza zungumza kwa hisia kwamba sijui mlango wa nyuma au wa mbele. Kama mwana JF unatakiwa utoe na source of data or information;

1. Nani alikwambia Rais wa Israel ndiye aliamua Yitzak Rabin apigwe risasi? je wewe ni mmoja wa Mossad?
2. Utaratibu unaoonyesha kuwa anayegombea uwaziri mkuu uingereza lazima awe na uhusiano mzuri na malkia umeupata wapi?
3. Unazungumza habari za Nyerere kuwa alikuwa anafanya mambo mlango wa nyuma ninakutalia kama ifuatavyo:
(i) Azimio la Zanzibar; Nyerere hakulipenda lakini lilipitishwa wakati Rais akiwa Mzee Mwinyi. Nyerere alikuwa bado hai.
(ii) Ubinafisishaji wa mashirika ya umma; umefanywa wakati wa Mwinyi na Mkapa, Nyerere alikuwa hai na hakuwahi kuwakataza kubinafisisha mashirika hayo.

Mungu ibariki Tanzania

 
Vyovyote utakavyo select how u may call ! If it's CEREMONIAL FIGURE! MONARCH FIGURE! ROYAL FIGURE! or else (ecxept ENGLISH FIGURE!) Britain Quine remained a great leader 2 the teritories, wanaobisha hili ni wale ambao hamjawahi kuwepo ktk nchi hio atlist 4 one year, ni kwl kbs Quine behind the curten ana maamuzi makubwa than PM! Igree or not! Kitu ch kwnz akifanyacho elected PM ni ku'report Bcnghm palace kwanza upewe sutsfied ndy mengine yafate
 
VERY INTERESTING..... read
The media has successfully painted Gaddafi as a hard-core dictator, tyrant whatever you want to call him. However, the media as usual has also failed to show the kind, giving Gaddafi we never heard of. Gaddafi unlike most dictators I will refrain from naming them has managed to show his humane side, the very side we dream of seeing in other dictators who just talk and talk.
I consider Libyans lucky to a certain extent and one wonders with the new democratic rule they cry for will it improve or worsen life for them Yes, Gaddafi has spent millions of Libya`s money on personal ventures but is the average Libyan poor? We know others who take a country and destroy it until you feel like there is no hope of restoring this country… looting some prefer to call it. Did Gaddafi loot Libya in any way?
Now let us get to the unknown facts about the Libyan dictator Muammar Gaddafi:
download

1. There is no electricity bill in Libya; electricity is free for all its citizens.
2. There is no interest on loans, banks in Libya are state-owned and loans given to all its citizens at 0% interest by law.
3. Home considered a human right in Libya – Gaddafi vowed that his parents would not get a house until everyone in Libya had a home.


4. All newlyweds in Libya receive $60,000 Dinar (US$50,000) by the government to buy their first apartment so to help start up the family.
download

Traditional wedding in Tripoli, Libya

5. Education and medical treatments are free in Libya. Before Gaddafi only 25% of Libyans were literate. Today the figure is 83%.
6. Should Libyans want to take up farming career, they would receive farming land, a farming house, equipments, seeds and livestock to kick-start their farms – all for free.
7. If Libyans cannot find the education or medical facilities they need in Libya, the government funds them to go abroad for it – not only free but they get US$2,300/mth accommodation and car allowance.
8. In Libyan, if a Libyan buys a car, the government subsidized 50% of the price.
9. The price of petrol in Libya is $0.14 per liter.
10. Libya has no external debt and its reserves amount to $150 billion – now frozen globally.

download

Great Man-Made River project in Libya… $27 billion

11. If a Libyan is unable to get employment after graduation the state would pay the average salary of the profession as if he or she is employed until employment is found.
12. A portion of Libyan oil sale is, credited directly to the bank accounts of all Libyan citizens.
13. A mother who gave birth to a child receive US$5,000
14. 40 loaves of bread in Libya costs $ 0.15
15. 25% of Libyans have a university degree
16. Gaddafi carried out the world’s largest irrigation project, known as the Great Man-Made River project, to make water readily available throughout the desert country.
Which other dictator has done much good to his people?




tion.
 
Walibya wameingizwa mkenge na kuitupa almasi baada ya kupewa chupa. Dunia yote watu wanahangaika na kupigania hata nusu tu ya walichokuwa wanakipata wao.

Wakadanganywa kwamba hicho walichonacho ni upuuzi tu mbele ya usanii unaoitwa demokrasia, as if ndiyo inayojaza tumbo au kupeleka watoto shule.

 
Back
Top Bottom