The SGR War: Wakati Kenya wakisuasua, Uganda wameamua kujenga SGR. Hii ni fursa kwa SGR ya Tanzania. Is it viable? Tuichangamkie?

Jamani ninyi mnao kaa huko Dsm mnajua idadi ya maloli yanayosafirisha mizigo mpaka mseme huenda kukawa hakuna mzigo wa kushiba? Ukikaa kahama au Tunduma ndio utajua umuhimu wa reli. Maelfu ya malori yanapita na kuharibu barabara.

Nchi kama South Africa wanabarabara nzuri hii ni sababu ya mizigo mingi kusafirshwa na reli. Kwa hiyo pamoja na kusaidia kusafirisha mizigo,hata barabara za Tanzania zitadumu kwa muda mrefu.
 
Unahitaji kuwa mwendawazimu kuongea ulichoongea.
Mkuu tindo , with due respect, wakati tukiendelea na huu mjadala, naomba tuepuke lugha za maudhi, machukizo na matukano!, tunaweza kuendelea kujadiliana in civilized manner bila kuitana wendawazimu!.
P
 
Mkuu ikigijo , hili ni swali gumu kupita uwezo wangu, linamhitaji mtaalam wa uchumi, kufanya a comparative analysis the multiplier effets ya hizo megawat 2115 na faida za SGR. Kitu ambacho mimi nilikinote tangu mwanzo, ni tatizo katika upangaji wa vipaumbele vyetu, mfano fedho zinazotumika kununua ndege, zingeingizwa kwenye kilimo, tungefaidika zaidi kuliko na ndege zilizo pack tuu pale airport.



P
 

Yes Seali linahitaji wachumi kuchambua Comparative advantage na kuona Mizigo ni Tani ngapi,Sgr uwezo wake ni upi?
Na Umeme 2115MW zikiingia kwenye grid ya Taifa tutapata Tsh ngapi kwa mwezi!
Kuhusu bombadier na hata hiyo miradi inatoendelea unafikiri wachumi au wataalam hawakushauri?
 
Kuhusu bomba nakaa kimya maana umeleta lawama kwa serikali hali ukijua haipaswi kulaumiwa. Nakaa kimya ila umebugi. Pesa za sherehe kuwekea jiwe la msingi zinakutoa roho? Kwani hazitarudi mafuta yakianza kusafirishwa?

Kwanza naomba utulize kichwa kisha utumie akili kudadavua mambo,kuendesha serikali sio jambo jepesi. Na hata mipango ya ujenzi wa miradi mikakati mikubwa kama hii ya Sgr sio jambo dogo kama wewe kupanga kujenga nyumba ya vyumba vitatu na sebule.

Inawezekana serikali ilijipanga vizuri ili ijenge Sgr kwa pesa za ndani lakini kama nilivyokuambia kuendesha serikali kuna mambo mengi na vikwazo vingi. Hivyo sioni jambo baya kupata pesa toka China maana hujui vikwazo gani vimetokea hapo kati. Na sioni haja wewe uambiwe maana ni siri ya serikali.

Kwamba JPM alipokuwa waziri wa JK ulitaka apinge mradi wa gas wa umeme? Unadhani ni rahisi? Kwanza nafikiri mpaka anaingia madarakani Kinyerezi 1&2 ziliendelea kujengwa na akazikamilisha.kwa hiyo sioni kama anapinga kuwa na gas plants.

Lakini kataa au usikatae uamuzi wa kujenga JNHP ni wa busara kuliko hizo gas plant unazozipigia debe huku zikizalisha Mw 240 kwa mafungu. Na kama tukipata Mw 2115 hazitatosheleza? Au ulitaka ukusanye MW 2115 kwa mafungu? Nani amekuambia maji ya mto rufiji,ruaha mkuu na na kilombero ni ya seasonal? Mbona tangu aingie madarakani hatujaona ukame au mgao wa umeme? Kama kuna maumivu kama watanzania tuwe wazalendo,Sgr na JNHP zikamilike na tujifunge mikanda.

Hata kama Sgr itakamilika kwa pesa za mkopo toka nje nani atayelipa hilo deni kama sio watanzania? Acha porojo kisa tu unapinga maendeleo.
 
Mkuu chagu wa malunde, kwanza naunga mkono hoja 100% kwa 100%, malori yanaharibu sana barabara zetu, na hili niliisha wahi kulizungumza, Reli ya SGR: Je, Tujifunze kwa wenzetu Kenya kuepusha SGR yetu kuwa ‘A White Elephant’? Wenzetu yameshawakuta...
P
 
Mkuu chagu wa malunde, thanks kwa your objectivity, kati ya kazi ngumu sana, ni kazi ya kubadili mind sets, kazi ya kuelimisha hawa wapinga maendeleo, wenye negativity ili wa change hizo negativity na kuwa positive.

P
 
Mkuu tindo , with due respect, wakati tukiendelea na huu mjadala, naomba tuepuke lugha za maudhi, machukizo na matukano!, tunaweza kuendelea kujadiliana in civilized manner bila kuitana wendawazimu!.
P

Ni kweli kabisa, kadiri mjadala unavyoenda inabidi maneno kama hayo niyaache, ili tusipotezane huko mbeleni. Nafuta kauli.
 
Kwa taarifa yako Kenya SGR tayari ishaanza kuingiza kipato,wananchi wa Kenya wamesha anza kuonja manufaa ya SGR .

Tangu mwezi wa November SGR ilikuwa imeshajaa hadi januari kwa wingi wa abiria.
Mkuu Mmawia, hakuna mtu anayejua kila kitu, kitu kama hujui sio lazima kuchangia!. SGR haiwezi kujiendesha kwa faida hata ikipata abiria 100%. The plan ya SGR ya Mombasa ni kwenda mpaka Malaba, hivyo kubeba mzigo wa Uganda, Rwanda, DRC na Southern Sudan. SGR ya Uganda ili ilete faida ni kupokea mzigo wa Rwanda, Burundi, DRC na Southern Sudan. Kitendo cha SGR ya Rwanda kuunganisha na ya Tanzania, kukaifanya SGR ya Kenya a white elephant, kwasababu bila mzigo wa Rwanda, SGR ya Uganda hailipi, bila mzigo wa Uganda, SGR ya Kenya hailipi, hivyo sasa SGR ya Kenya itaishia Naivasha and will never pay!.
Jielimishe zaidi hapa
P
 
Ni kweli kabisa, kadiri mjadala unavyoenda inabidi maneno kama hayo niyaache, ili tusipotezane huko mbeleni. Nafuta kauli.
Asante sana, huu ndio utu, ustaarabu ni kitu cha bure.
P
 
Mkuu asante sana kwa kuliweka hili suala kwa uwazi, lakini hii ilikuwa developmental proposions za Head of States kuboresha EAC infrastructures.

Lakini hakukuwa na kitu chochete East Africa Community ilikifanya kwa Head of States baada ya mapendekezo, ( polical wishes).

1) Memorundum Of Understanding (MOU)
2) Projects Technical proposals (PTP),
3) Business Plan (BP),
4) Projects Implementation Plan(PIP),
5) Projects Financing Plan(PFP).

Na sio kweli nchi zinazo subiri zinahakika ya kufanya hayo kama ilivyo pendekezwa, kama Warundi ni sisi tutakao jenga. Hata bandari na barabara ya ndani kwa Congo ili kuunganisha kwa upande wao na barabara kuu ni sisi tumependekezwa tujenge au tushirikiane kugharamia kuijenga. JAPO KWA HILI MKULU YAKO KIMYA.
 

Mkuu ahsante kwa hoja mujarabu
Kwanini tusiwe na Miradi Mkakati 1,au 2 tuu
Tuseme Stiglier na SGR vimiradi vingine vidogovidogo tuviache kwanza...
Yaani tuwekeze nguvu kubwa huko lakini tunawekeza tumiradi twingiiii mara Megawatts 30,100,240,
Mara sijui kivuko mara Yaani ni Vingi mnooo,
Feasibility study ingefanyika na kufanya hata Mradi mmoja Giant say Stieglier Sababu hata Hiyo Reli ya Umeme ungetegemea ukamilikaji wa stieglier gorge kwanza!
Tungepiga sana hapa,
Kuliko sasa hivi mara sijui Kinyerezi-1,2,3,4,5 Six huko sijui,
Zote ni mipesa hivyo...
Twende na stieglier kwanza!
 
Ni wazo jema.
 
Mkuu suala la complimenting or alternative katika Economic projects valuation halina nafasi.

Every project is a profit center. Unless tunaongea political economy.

Na sio kwa SGR tuu, every project work as a tool to accelerate economic growth of our people and the country.
 
nadhani wasiwasi wa nchi zote za magharibi ni kwamba Tanzania ikiweza kuwa vizuri kwenye uchumi itapelekea nchi nyingi sana za ukanda wetu kuwa huru kiuchumi na hii haitokuwa vizuri sana kwao maana kuna vikwazo lazima tutakuwa tuna vipunguza kutokana na uchumi wetu kuimarika na nchi za jirani

Na hili litaweza kuwafanya wao waingize propaganda kwasababu sidhani kama Tanzania tulishawahi fuata na kuwa kwenye nyayo zao muda mrefu ikipelekea hii miradi kumalizika na kilimo kikawa vizuri jumlisha na umeme imported goods zitapungua na wazee huku hawatokubali maana economic yao ina tegemea sana bara la Africa hasa sub saharan countries

Nadhani kwa hili tuombe MUNGU tufanikiwe maana adui anaweza kutokea popote na huenda hata akawa rafiki wa karibu

National interests kwa Africa ni changamoto na ni vita kubwa sana mzungu kukubali si rahisi na zijengwe kutokana na matumizi ya sisi wa Africa isije ikawa ndio njia za ku lubricate exports ya raw materials kwenda mataifa ya magharibi tutakuwa hatujafanya kitu

ikiwezekana viwanda navyo tuangalie viwepo hata processing na manufacturing industries

We Africans need to produce things we consume and consume things we produce without awareness nothing gonna change,it's a war and in these issues Africa needs to become one without any country being a traitor pasipo hivyo kuna watu wanaweza kuja kuwekwa kwenye kikaangoo kama Gaddafi na wengine being economically independent inawapa wazungu hasira sana sanaaa

There's is no a place that loves you the most like your country Africa is home we need to rebuild it again!
 
Mkuu Kishina cha Mshahara, Salary Slip , naunga mkono hoja, naunga mkono hoja, nchi inaendeshwa kwa mujibu wa katiba, sheria, taratibu na kanuni, na sio kwa utashi tuu wa kiongozi aliyepo madarakani. Mfano, haiwezekani nchi itumie bilions kuanzisha mchakato wa katiba, na baada kula ngombe mzima, na kubakisha mkia, kiongozi anafuata, ana abandon kila kitu kwa hoja sio kipaumbele changu!.

Kufuatia uzoefu huu, JPM ndie rais wa mwisho Tanzania, kuwa rais kwa kubeeb tuu, kuanzia sasa, tutahakikisha anayempokea Magufuli, anasainishwa "a continuity clause", kuyaendeleza yote ya mtangulizi wake, na anayempokea ni yule atakayeyaendeleza mazuri yote ya Magufuli, na tukijiona tuna mashaka, then, Magufuli alazimishwe kuendelea, hadi akamilishe miradi yake yote ya kimkakati, hata kama it will take some ten extra years, let it be!.
P
 
Umewahi kutembelea maeneo ya hii miradi ukaona kazi zinazofanyika?? Kama la basi tembelea kwanza then ndo uje uwazodoe hapa. Huwa nawapinga sana MATAGA ila kwenye hili napingana na wewe. Fanya kwenda kuangalia naamini utabadilisha maoni yako. Btw soon kipande cha mwanza kitaanza kujengwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…