The so called 'GOD' from religions

The so called 'GOD' from religions

Kiranga ,Jimena na wapinga Mungu wengine ni vyema basi mkatupa sababu zenu za kutokuwepo Mungu nje ya hv vitabu vya quran na biblia kwa kuwa hamviamini.hizi kauli za upendo,uwezo na ujuaji alionao Mungu ni maneno mlosikia sisi waabudu Mungu tukisema au nyie wenyewe mumesoma kwenye vitabu vya iman ambavyo tayari hamviamini.sasa kwa kutusaidia mungetoa sababu zingine nje ya vitabu.sijui nimeeleweka??
 
We binti,jifunze adabu kwanza,sio unatukana watu usio wajua

Swali la msingi alilouliza Kiranga hamjalijibu mpaka sasa,

Mdahalo utaendeleaje kama hamtaki kujibu maswali ya msingi?

Msingi wa swali la Kiranga ni huu;

Suppose,kuna radi imepiga katika msitu

Ikasababisha moto mkubwa[Forest fire]

Moto huo ukasambaa kwa kasi na kwenda kuteketeza kambi ya wakimbizi

Idadi kubwa ya watu waliokufa ikawa ya kina mama wenye mimba na watoto wachanga

Kama Mungu mwenye ujuzi wote yupo,basi aliliona hili tukio mapema kabla halijatokea na akajua jinsi ya kulizuia.

Mungu mwenye upendo kwa viumbe wake,asingependa hili tukio liwapate watu wake,haswa wale watoto wachanga.

Na Mungu mwenye nguvu zote,asingeshindwa kulizuia hili tukio baya

Lakini tukio limetokea,kwanini?

Mungu alitaka kulizuia lakini akashindwa?

Au alikuwa na uwezo wa kulizuia lakini hakutaka?

Au vyote kwa pamoja?
Kama radi kupiga ni matokeo ya mchakato usio na mpango hata wakimbizi kufa ni matokeo yaaiyopamgwa sasa wewe ubaya wa vifo vya radi unahusikaje na Mungu.?
Uliza kuhusu Mungu kwa yanayomhusu kadri ya world view yake. Lakini kutumia world view yako kuuliza maswali kuhusu world view nyingine usiyoikubali ni ujuha.
Pasipo Mungu hakuna Jema wala baya kuna kutii muziki na mihemko ya DNA
 
Duara yenye pembe tatu ipo?

Bachelor aliyeoa yupo?

Bikra aliyezaa yupo?

Mtoto mchanga mwenye wajukuu yupo?

Pembe tatu yenye nyuzi zaidi ya 180 ipo katika Euclidean geometry?

Hivyo vitu vyote kimantiki haviwezekani,kwa hiyo Kiranga akisema hivyo havipo ina maana havipo kwake tu?

Mungu Hayupo si kwasababu umeshindwa kutoa uthibitisho

Hayupo kwasababu anajipinga yeye mwenyewe ni sawa na Pembe tatu duara.
Uwezo wako mdogo wa kutafakari ndiyo unaona kujipinga kwa Mungu. Ni tatizo lako binafsi sio la Miungu
 
Duara yenye pembe tatu ipo?

Bachelor aliyeoa yupo?

Bikra aliyezaa yupo?

Mtoto mchanga mwenye wajukuu yupo?

Pembe tatu yenye nyuzi zaidi ya 180 ipo katika Euclidean geometry?

Hivyo vitu vyote kimantiki haviwezekani,kwa hiyo Kiranga akisema hivyo havipo ina maana havipo kwake tu?

Mungu Hayupo si kwasababu umeshindwa kutoa uthibitisho

Hayupo kwasababu anajipinga yeye mwenyewe ni sawa na Pembe tatu duara.
Ukisema Duara yenye pembe tatu IPO?Ndio pembe tatu ipo na duara IPO,mpaka ukauliza duara na ukauliza pembe tatu,ni vitu viwili tofauti,ambavyo vipo.

Ukiuliza bachelor aliyeoa,ndio ubachelor upo na kuoa kupo,alianza kuwa bachelor ndio akaoa.Bikra aliyezaa, pia yupo, alianza ubikra ndio akazaa.Kwa hiyo ubikra upo na uzazi upo.Vyote ulivyovitaja vipo.

Kumbuka huwezi kusema hakuna bila kuwapo,kama hakukuwapo basi huwezi sema hakukuwapo,ila kukikuwapo ndio utasema hakukukuwapo.
Unaposema Mungu hayupo, ndio kuthibitisha kuwa yupo.Kama angekuwa hayupo,usingesema hayupo,ni baada ya kujuwa yupo,ndio ukasema hayupo kwako,lakini kwa wengine yupo.
 
H1N1 said:
Kama radi kupiga ni matokeo ya mchakato usio na mpango hata wakimbizi kufa ni matokeo yaaiyopamgwa sasa wewe ubaya wa vifo vya radi unahusikaje na Mungu.?
We ukapimwe akili!

Matetemeko ya Ardhi yanayoua watu kila mwaka,Njaa,Tsunami na magonjwa bado Mungu hausiki

Kwahiyo yeye anafurahia kuona watu wakifa kama hivyo?
Uliza kuhusu Mungu kwa yanayomhusu kadri ya world view yake. Lakini kutumia world view yako kuuliza maswali kuhusu world view nyingine usiyoikubali ni ujuha.
Pasipo Mungu hakuna Jema wala baya kuna kutii muziki na mihemko ya DNA
Hata ya ham ya kukujibu sina

Maana kichwani mwako hakuna kitu.

Talk to the hand!
 
Aliyezaliwa kipofu wa macho,hajawahi kuona jua,atasema hakuna jua,kusema kwake hakuna jua,ni baada ya kusikia kuna jua,lakini halioni,kwa kutoliona kipofu jua na kusema hakuna jua,sio sababu ya wanaliona jua kwao pia iwe hakuna jua.

Na ni vilevile,kwa mwenye upofu wa moyo,asiyemuona Mungu kwa moyo,iwe sawa kwa wanaomuona Mungu kwa moyo,ikiwa wewe humuoni Mungu kwa moyo,sio sababu yakufanya wanamuona kwa moyo,nao iwe kwao kama wewe usimuona kwa moyo,Mungu,wakati wao wanamuona kwa Moyo.

Ni baada ya wewe kusikia wanaomuona kwa Moyo kama Mungu yupo,ndio wewe,kwa vile humuoni kwa moyo, ndio ukasema hayupo. Kwa hiyo kusema Mungu hayupo,ndio kuthibitisha kuwa yupo.
 
Kutokukubaliana kuhusu yupi Mungu wa kweli haiwezi kuwa sababu ya kutokuwepo kwake.
"Mr pembe Tatu duara"
"Inherent contradiction " inatokana kukariri kwako sifa za Mungu pasipo fikra.
Umekumbushwa ulimwengu ambaobumetokea kwa ajali hauna maovu kwa kuwa kipimo cha utambuzi wa maovu kinakuwa hakuna kwa kuwa ili uitwe uovu lazima utendwe na binadam dhidi ya binadam jappo kuna kuhangsika kwingi kutafita maana mbdala.
Kama uovu ukitendwa dhidi ya binadam na ukajua ni uovu ina maanisha umeweka thamani kwa binadmu husika na hiyo inakinzana na marlezo yenu kuhusu chanzo cha binadam.kuwa ni matokeo yasiyopangiliwa
Tatizo lako ni kukariri ndiyo sababu huwezi kuelewa mambo madogo kama ya mema na msbaya kutohusika na ninyi kwa kuwa binadam asiyeumbwa anaendeshwa na matamanio ya mwili wake na kutii matamanio ndiko humfanya atende chochote sasa ninyi msiomjua Mungu mmepata wapi ujuzi wa mema na mabaya
Zindukana wewe
Hujathibitisha kwamba mungu yupo.

Unaleta hadithi ndefu zinazojikanganya.

Thibitisha kwamba mungu yupo kwanza.
 
Aliyezaliwa kipofu wa macho,hajawahi kuona jua,atasema hakuna jua,kusema kwake hakuna jua,ni baada ya kusikia kuna jua,lakini halioni,kwa kutoliona kipofu jua na kusema hakuna jua,sio sababu ya wanaliona jua kwao pia iwe hakuna jua.
Na ni vilevile,kwa mwenye upofu wa moyo,asiyemuona Mungu kwa moyo,iwe sawa kwa wanaomuona Mungu kwa moyo,ikiwa wewe humuoni Mungu kwa moyo,sio sababu yakufanya wanamuona kwa moyo,nao iwe kwao kama wewe usimuona kwa moyo,Mungu,wakati wao wanamuona kwa Moyo.
Ni baada ya wewe kusikia wanaomuona kwa Moyo kama Mungu yupo,ndio wewe,kwa vile humuoni kwa moyo,ndio ukasema hayupo.
Kwa hiyo kusema Mungu hayupo,ndio kuthibitisha kuwa yupo.
Unaweza kuwa kipofu, ukamshika tembo mkia, ukaambiwa huyo ni tembo, ukapewa kamba, ukaishila ukaona ni kama mkia wa tembo, ukasema kamba na tembo vina umbo sawa.

Kama binadamu ana tatizo la upofu, suluhisho ni kutafuta kuona/ kujua.

Kutafuta kujua hakuji kwa kuamini tu.

Kunakuja kwa uchunguzi.

Mpaka sasa hakuna uchunguzi uliothibitisha kuwapo kwa mungu.

Wote wanaosema mungu yupo, wanasema hivyo kwa imani potofu ambazo tushazipangua hapa.

Unaweza kuthibitisha mungu yupo?
 
Hujathibitisha kwamba mungu yupo.

Unaleta hadithi ndefu zinazojikanganya.

Thibitisha kwamba mungu yupo kwanza.
Huko kusema Mingu hayupo,ndio uthibitisho wa kuwa Mungu yupo.
Huwanza kuwapo, ndio ikaja kutokuwapo.

Na unaposikia hakipo,ni kuwa kipo,lakini hakipo machoni mwako au moyoni mwako,lakini kwa wengine kipo. Na hata ukisikia fulani ampenda Fulani,sio lazima wewe umpende huyo fulani,ndio ujuwe kama Fulani ampenda Fulani. Anayejuwa Fulani ampenda Fulani,ni yule anayeziona hizo athari za huyo anayempenda na anaypendwa.

Na hivyo hivyo,kutokuona kwako athari za Mungu, sio sababu kwa wanaona nao wao kama wewe usiyeona hizo athari za kuwepo Mungu.
Kwa kusema Mungu hayupo,ndio uthibitisho tosha wa kuwa Mungu yupo.
 
Kiranga ,Jimena na wapinga Mungu wengine ni vyema basi mkatupa sababu zenu za kutokuwepo Mungu nje ya hv vitabu vya quran na biblia kwa kuwa hamviamini.hizi kauli za upendo,uwezo na ujuaji alionao Mungu ni maneno mlosikia sisi waabudu Mungu tukisema au nyie wenyewe mumesoma kwenye vitabu vya iman ambavyo tayari hamviamini.sasa kwa kutusaidia mungetoa sababu zingine nje ya vitabu.sijui nimeeleweka??
Sitaki kukupa sababu nje ya vitabu vyenu.

Kwa maama mtasema si sababu za kweli.

Sababu za kitokuwepo mungu zipo katika vitabu vyenu.

Vitabu vinasema mungu wenu anajua yote, ana nguvu zote, ana upendo wote. Sawa?

Sasa basi, kama mungu ana ujuzi wote, ana upendo wote na ana uwezo wote, turudi nyuma alipokuwa anauumba ilimwengu.

Aliweza kuumba ulimwengu wa aina yoyote. Hakuna kikichomzuia.

Aliweza kuumba ulimwengu ambao manaya hayawezekani kufanyika. Yanawezekama mazuri tu.

Lakini hakuumba ulimwengu huo.

Kwa nini hakuumba ulimwengu huo na yeye alikuwa na uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote?

Kazini kwangu softwareengineer akiwa na uwezo wa kutengeneza software isiyo crash, halafu akatengeneza software inayocrash, anafukuzwa kazi kwa uzembe.

Na huyu hana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote.

Kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote tunamuwekea standards za chini zaidi ya software engineer?

Kwa nini mungu kaamua kuumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?
 
Ukisema Duara yenye pembe tatu IPO?Ndio pembe tatu ipo na duara IPO,mpaka ukauliza duara na ukauliza pembe tatu,ni vitu viwili tofauti,ambavyo vipo.
Ukiuliza bachelor aliyeoa,ndio ubachelor upo na kuoa kupo,alianza kuwa bachelor ndio akaoa.Bikra aliyezaa,pia yupo,alianza ubikra ndio akazaa.Kwa hiyo ubikra upo na uzazi upo.Vyote ulivyovitaja vipo.
Kumbuka huwezi kusema hakuna bila kuwapo,kama hakukuwapo basi huwezi sema hakukuwapo,ila kukikuwapo ndio utasema hakukukuwapo.
Unaposema Mungu hayupo,ndio kuthibitisha kuwa yupo.Kama angekuwa hayupo,usingesema hayupo,ni baada ya kujuwa yupo,ndio ukasema hayupo kwako,lakini kwa wengine yupo.
Onvioisly either the concept of consecutive application escaoes you or you are jusf being funnily evasive.
 
Huko kusema Mingu hayupo,ndio uthibitisho wa kuwa Mungu yupo.
Huwanza kuwapo,ndio ikaja kutokuwapo.
Na unaposikia hakipo,ni kuwa kipo,lakini hakipo machoni mwako au moyoni mwako,lakini kwa wengine kipo.
Na hata ukisikia fulani ampenda Fulani,sio lazima wewe umpende huyo fulani,ndio ujuwe kama Fulani ampenda Fulani.Anayejuwa Fulani ampenda Fulani,ni yule anayeziona hizo athari za huyo anayempenda na anaypendwa.
Na hivyo hivyo,kutokuona kwako athari za Mungu,sio sababu kwa wanaona nao wao kama wewe usiyeona hizo athari za kuwepo Mungu.
Kwa kusema Mungu hayupo,ndio uthibitisho tosha wa kuwa Mungu yupo.
Kama kusema mungu hayupo kunathibitisha kwamba mungu yupo, basi kusema mungu yupo kunathibitisha kwamba mungu hayupo

Na hapa tumesema mungu yupo na hayupo.

Kwa hiyo mungu hayupo na yupo.

You have a crazy way of thinking.
 
Kikwajuni said:
Ukisema Duara yenye pembe tatu IPO?Ndio pembe tatu ipo na duara IPO,mpaka ukauliza duara na ukauliza pembe tatu,ni vitu viwili tofauti,ambavyo vipo.
Ukiuliza bachelor aliyeoa,ndio ubachelor upo na kuoa kupo,alianza kuwa bachelor ndio akaoa.Bikra aliyezaa,pia yupo,alianza ubikra ndio akazaa.Kwa hiyo ubikra upo na uzazi upo.Vyote ulivyovitaja vipo.
Kumbuka huwezi kusema hakuna bila kuwapo,kama hakukuwapo basi huwezi sema hakukuwapo,ila kukikuwapo ndio utasema hakukukuwapo.
Unaposema Mungu hayupo,ndio kuthibitisha kuwa yupo.Kama angekuwa hayupo,usingesema hayupo,ni baada ya kujuwa yupo,ndio ukasema hayupo kwako,lakini kwa wengine yupo.
Hoja kama hizi ndiyo tunazoziita non sequitur

Duara lipo,pembetatu ipo,Lakini pembetatu duara haipo

Bachelor yupo na kuoa kupo,lakini bachelor aliyeoa hayupo

Bikra yupo,kuzaa kupo
Lakini bikra aliyezaa hayupo

Ukishaa zaa,sio bikra tena

Kwani nikisema 'mzee Panknqzk' hayupo?hapo nitakuwa nimethibitisha yupo

Unajua 'mzee Panknqzk' ni nani?
 
Huyo jamaa kashindwa kujibu hoja kajitia uchizi tu.
 
Back
Top Bottom