Sitaki kukupa sababu nje ya vitabu vyenu.
Kwa maama mtasema si sababu za kweli.
Sababu za kitokuwepo mungu zipo katika vitabu vyenu.
Vitabu vinasema mungu wenu anajua yote, ana nguvu zote, ana upendo wote. Sawa?
Sasa basi, kama mungu ana ujuzi wote, ana upendo wote na ana uwezo wote, turudi nyuma alipokuwa anauumba ilimwengu.
Aliweza kuumba ulimwengu wa aina yoyote. Hakuna kikichomzuia.
Aliweza kuumba ulimwengu ambao manaya hayawezekani kufanyika. Yanawezekama mazuri tu.
Lakini hakuumba ulimwengu huo.
Kwa nini hakuumba ulimwengu huo na yeye alikuwa na uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote?
Kazini kwangu softwareengineer akiwa na uwezo wa kutengeneza software isiyo crash, halafu akatengeneza software inayocrash, anafukuzwa kazi kwa uzembe.
Na huyu hana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote.
Kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote tunamuwekea standards za chini zaidi ya software engineer?
Kwa nini mungu kaamua kuumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?